Wanasiasa mnatulazimisha kuwasaidia siasa

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,952
Hello members JF!

Nawaheshimu na nitaendelea kuwaheshimu wale tutakaoweza kuheshimiana.

Moderator naomba usiniunganishe popote na hii topic yangu.

Hapo kabla,humu jukwaani palikuwa mahali huru na penye heshima ya kila mtu kuchangia kwa uhuru wake na kwa kiasi cha upeo wake.Lakini pia kwa utashi wa uhuru wake wa kuamini na kuchagua lile ambalo analisimamia katika imani yake iwe kisiasa,kidini au hata kielimu nk.
Na bila kuvunja kanuni na vifungu vya kikatiba ya JMT.

Lakini baadae na kwa taratibu,jukwaa hili likaanza kuvamiwa na watu ambao wanataka kuligeuza kama platform yenye mlengo mmoja wenye nia moja,na pia wenye kusudio moja.
Nalo ni kuwa kama tawi la wanaharakati na wanasiasa wenye mlengo tofauti na serikali.Na imegeuka kuwa yeyote yule anaye changia mawazo yake huru,na akaonekana kuwa upande wa serikali,basi huyo ataonekana humu kama mtu anayestahili matusi,kejeli au hata kuitwa majina ya ajabu ajabu tu.(moderators mpo na mko kimya).

Na humu mnataka kuligeuza jukwaa la watu wa mlengo wa anti-goverment.
Wakati mkilaumu serikali ya CCMkuwa inaminya demokrasia nchini.
Nyinyi humu mnaminya demokrasia ya uhuru wa watu wengine kutoa maoni yao.mnatukana watu ovyo bila hata kuwa na staha.

Wakati mkifanya hayo,bila kujua kwamba wengi wa wachangiaji humu,sio na wala hawajawahi kufanya siasa kuwa njia ya kuwapatia kipato cha kimaisha.(kama ambavyo wengi wa wanasiasa Tanzania mlivyo).

Wengi mlichokisomea na kufeli mitihani sio mnachokifanya(sio wanasiasa wote)kuna wanasiasa vijana wazuri na wanafanya siasa nzuri na wanastahili pongezi,ila kuna hili kundi ambalo mliingia kwenye short cut za siasa kupitia ubishi wenu mkiwa vyuoni na mkaishia kufeli masomo kwa kuendekeza aidha uwaziri,unaibu rais wa majukwaa na jumuia mbalimbali vyuoni(ambazo si za kitaaluma rasmi).kubishana na taasisi za uongozi rasmi vyuoni.

Sasa mmeshindwa siasa za kwenye ulingo wa siasa,aidha kwa kutotimia kwa malengo yenu kupitia ubanwaji wa vyanzo vya mapato kupitia nyadhifa za kisiasa(kutokana na sera za JPM).

Sasa JF inageuka taratibu kuwa likichaka la watu waliojawa na hasira za majeruhi mbalimbali kama vile vyeti hewa,mishahara hewa,wabunge na wafuasi fulani fulani wanaochukia misimamo ya Mheshimiws Rais JPM,wale ambao walikuwa wategemezi wa ndugu na jamaa zao au hata wazazi wao ambao wamekutana na rungu la JPM mahali fulani.na kuwatibulia ndoto zao kutokana na pato haramu.
Lakini pia lipo kundi la wakosa uteuliwa na watumbuliwa na ndugu zao pia.

Sasa kwa sababu humu ni hidden identity mnakuja huku mkiwa mmejaa sumu kama Cobra,mnatukana ovyo,huku mkijiaminisha kwamba kutoona members wengi kuwafuatilia basi eti hiyo ni ticket ya popular majority of the wining

Mnajidanganya,
Ukweli ni kwamba watu wengi siku hizi wanapotezea kiaina,kwa kuchoshwa na utumbo unaolazimishwa humu ndani,matusi na kejeli humu JF.
lakini pia mod's pia wamekuwa kama marefarii wa mechi za mchangani.(ushahidi ni avatar utitiri zinazojirudia rudia humu au kufunguliwa na kupotea baada ya muda mfupi).

Siku hizi ukitaka ugombaniwe na vyama fulani fulani,wewe tafuta bifu na kiongozi yeyote yule wa CCM.
Au ukitaka uteuliwe kugombea vyama fulani basi jitowe muhanga hata ugongwe na gari la mwenyekiti wa wilaya wa CCM,(kama urajeruhiwana kupona)hapo utakuwa lulu humu JF.
Hata ticket ya ndege utakatiwa ili utibiwe vizuri ukirudi utapewa ugombea.
Nasema haya kwa kuzingatia ninayoyaona kwenye siasa uchwara za kitanzania sasa hivi.

Hivyo bila kujua taratibu watu makini wanasepa humu na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Wakati huo mnajiaminisha mko top,lakini ukweli ni kwamba watu makini wanakiona kinachoendelea kufanywa na serikali hii,na wanasubiri uchaguzi ili wampe huyu mzee JPM haki yake hadi 2025

Wananchi walikuwa wakiomba huduma bora za kijamii kama haki yao ya kikatiba,kutokana na kodi wanazolipa.
Na huo ndio msingi mkuu wa JPM na sio haki za kuandamana,uhuru wa vyombo vya habari na siasa za majukwaani.
Hivyo vitu ni muhimu lakini sio kipaumbele cha common mwananchi.

Ni kipaumbele cha wanasiasa na wanufaika wa vyanzo mbalimbali vitokanavyo na mapato husika ya taasisi zao,kulingana na taasisi zinazowafadhili.

Hivyo msiwalazimishe watanzania woote kulia kilio cha kisiasa.
Mnapopata nyafhifa zenu,wengi wenu hunufaisha ndugu na jamaa zenu,huku mkitulambisha asali kwa ncha ya kisu.
Ndio maana mnapokosa kilio kinatokea pande nyiingi,lakini sio pande zoote.
Nawakilisha ukweli wangu,mkitukana shauri yenu lakini nasimama na # Magufuli 2025#

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo 2020 ndio tutaona tena mabox ya kura yakitolewa vituoni na kwenda kujazwa kura za ccm? Ndio tutaona wakurugenzi na maafisa wengine wa uchaguzi wakikimbia ofisi ili wasipokee fomu za wagombea wa upinzani? Hiyo 2020 hamna mwenye akili timamu atasimama kwenye mstari wa kura eti kupiga kura kisa kuna reli au ndege, kama hivyo vitu ndio haki ya kukaa madarakani basi wazungu wa Afrika kusaini wangepaswa kuwa madarakani mpaka leo, kwani haya unayoyaona ni maajabu leo wao wamefanya mara elfu ya haya uyaonayo leo.

Kama unaona kwenye hili jukwaa hakuna maoni unayoyapenda ww, anzisheni jukwaa lenu la kusifia na mtu yoyote atayeingia huko bila kusifia mumtoe. Kama uko kwenye boom period ya utawala huu sio lazima wote wawe kwenye mtazamo unaotaka ww. Ukiona unatukanwa sio kwasababu unamsifia JPM bali ni pale unapoona ni haki huyo jpm kusifiwa na kila mtu. Mko wengi mnaosifia kwa hayo yanayoendelea, ni kwanini mkwazike kuingia mahali ambapo hampati faraja? Anzisheni jukwaa lenu hata kwa fedha za umma ili msifie vizuri na hakuna mtu atawabugudhi.
 
Fikra zinamtuma kuwa humu kuna CCM na wakinzani halafu JF ni wale polisi wanaowabeba kwenye uhalifu wao wa kisiasa.Hoja hawana halafu wanataka dezodezo!?
 
Hiyo 2020 ndio tutaona tena mabox ya kura yakitolewa vituoni na kwenda kujazwa kura za ccm? Ndio tutaona wakurugenzi na maafisa wengine wa uchaguzi wakikimbia ofisi ili wasipokee fomu za wagombea wa upinzani? Hiyo 2020 hamna mwenye akili timamu atasimama kwenye mstari wa kura eti kupiga kura kisa kuna reli au ndege, kama hivyo vitu ndio haki ya kukaa madarakani basi wazungu wa Afrika kusaini wangepaswa kuwa madarakani mpaka leo, kwani haya unayoyaona ni maajabu leo wao wamefanya mara elfu ya haya uyaonayo leo.

Kama unaona kwenye hili jukwaa hakuna maoni unayoyapenda ww, anzisheni jukwaa lenu la kusifia na mtu yoyote atayeingia huko bila kusifia mumtoe. Kama uko kwenye boom period ya utawala huu sio lazima wote wawe kwenye mtazamo unaotaka ww. Ukiona unatukanwa sio kwasababu unamsifia JPM bali ni pale unapoona ni haki huyo jpm kusifiwa na kila mtu. Mko wengi mnaosifia kwa hayo yanayoendelea, ni kwanini mkwazike kuingia mahali ambapo hampati faraja? Anzisheni jukwaa lenu hata kwa fedha za umma ili msifie vizuri na hakuna mtu atawabugudhi.
Unaponishangaza ni hapo unaposema eti 2020 hakuna mtu atasimama kwenye Foleni ya uchaguzi.

Mkuu Kama dunia ingekua na watu wanaofikiri na kukata tamaa hivyo dunia bado ingekua kwenye shimo la Giza totoro.

Kumbuka Mgurugenzi ni binadam kama wengine.
Asipodhibitiwa na kupata machungu atajiinua na kuangalia maslahi yake badala ya sheria kwa kuumiza wengine ili familia yake ishibe.
Eye with eye!
Kwenye mpira Refa aliyezoea kubeba timu yake , akijua kuwa timu pinzani wanajua kupigania haki yao na mashabiki wake wanajulikana kuwa hawana uvumilivu wa kuhujumiwa ni lazima refa afuate kanuni kuokoa pumzi yake.

Usifikirie hao CCM wanaofurahiya wizi wa kura hawajui kua kuiba kura ni kinyume na Vitabu vya duni,sheria za nchi na hata maadli ya binadam waliostarabika. Wanajua sana Ila wanachoangalia ni maslahi.
Mfamo Spika alituambiwa TL Mbunge kwa Mwaka mmoja amelipwa zaidi ya mil. 200 tena akiwa kitandani.
Chama tawala wanajua utam wa kushika funguo za hazina. Wanajua utam wa kushika dola.
Wapinzani bado wanashangaa shangaa wakati wenzao wanapambana.
Kila unayemuona anapambana kufa na kupona kutetea ugali wake.
Ukimuona anayegawa fomu anapigania ugali .Mlinzi anapigania ugali wake, anayegombea hasa wa chama tawala anataka agawiwe ugali wake kwa namna yoyote. Kama utakua na mgombea wa upinzani ambaye anasubiri apewe haki Mezani atapata makombo.

Usione watu wanahujumu wapinzani ni feza babu .
Wajipange kukabiliana na uovu wa kuhujumu zoezi la uchaguzi kwa namna yoyote mana wao ndio wanaotafuta nafasi za ubunge zenye maslahi na familia zao.

Kama mtu unapeleka mke wako kliniki Marekani halafu unalala kama ndezi uibiwe kura na vibaka halafu unabaki kulia badala ya kumliza mwizi ,utakua hujui umuhimu wa nafasi unayoitafuta.

Mtu unarudisha form peke yako barabarani halafu eti wanatokea vibaka wanakupora na wewe unabaki ukigaragara Chini kama mwehu badala ya kutafuta vijana wa kukusindikiza tena wakiwa na viberiti ili akijitokeza kibaka mporaji wa form basi anavuna anachopanda kama vibaka wengine.

Kila mtu alinde anachokitafuta kama ana uhakika wa kukipata.

Ni wazi kuwa Chama Kikongwe wamekua kama kundi la wapigaji wanaojipanga muda wote kufa na kupona ili tu washike nafasi za kuweza kuwapatia fedha za walipa kodi kwa UDI na uvumba. Hawa hawaangalii ubinadam wala sheria wanachojali ni kugawana nafasi za kupata hizo pesa.
Wakiachwa wanageuka kuwa kama wahalifu alimradi wapate nafsi hizo za ubunge ambazo zina maslahi makubwa.
 
Inakatisha tamaa sana...bora ubaki nyumban kwako tu aisee
 
Siwezi kujibu mmoja mmoja kwa sababu ninayo majukumu mengine,ili kuhakikisha familia yangu inapata haki yake.

Lakini hakika jiwe langu limewapata wengi wenu.
Kama kawaida ya dunia,ni vigumu kuwaridhisha binadamu wote kwa wakati mmoja.

Hili lilishindikana hata kwa enzi za mitume na manabii waliotutangulia,tunasoma katika vitabu vyote vya dini.ndio maana mpaka leo tunaomba kuendelea kusamehewa kila siku katika madhabahu na mimbari ya nyumba za ibada.

Wengi mlioko humu hamtetei wananchi kama mnavyojinadi,bali nyinyi na washirika wa mafanikio yenu.
Humu kuna kundi kubwa la wenye visasi zaidi kuliko wanasiasa wenye maslahi mapana na mwananchi wa kawaida.

Kuna mliozowea kuitumia siasa kama njia rahisi ya kufikia mafanikio kimaisha.
Ndio maana leo mbunge anathubutu kukopa milioni zaidi ya mia sita as if bunge ni saccos ya mikopo.
Hivi unamfikiriaje mbunge anayeingia bungeni na kukopa milioni zaidi ya mia sita?

Huyu atautumia muda wake mwingi kuhangaikia namna ya kutafuta vyanzo vya kumuwezesha kuipata hiyo milioni 600,ndani ya kipindi chake cha miaka mitano.

Je wananchi walimtuma akakope hiyo hela bungeni?
Au akawawakilishe wapiga kura wake kwa maslahi mapana ya jimbo lake!

Kwa hiyo na kwa sasa nimalizie hapo,kwa kuendelea kusema tuna wanasiasa na wanaharakati wengi humu JF,ambao hakika ni wasakatonge! Narudia tena ...wasakatonge hawana nafasi katika utawala wa JPM,iwe wako CCM,CHADEMA,ACT,CUF NCCR,nk.
Mheshimiwa magufuli (Hon president of URT)
Will stand for presidency 2020-2025.

#Tunasimama na JPM,2020-2025....

Asiyetaka ajitundike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi mrefu sana lakini wenye kurudia rudia mambo.Uzi wote uumejielekeza kwenye Jambo moja tu nalo ni kutaka wanaoikosoa serikali au CCM humu JF wadhibitiwe na moderators.Kimsingi huna hoja yoyote ya maana zaidi ya hasira sababu unaona hoja unazozipenda kila zikiletwa humu zinapanguliwa kirahisi sana kama kunywa maji.
Mwisho,haki ya kusifia upande unaoupenda uliyo nayo na kuifurahia humu ni haki hiyo hiyo waliyo nayo wakosoaji na hawavunji sheria yoyote ya JMT.
 
Unaponishangaza ni hapo unaposema eti 2020 hakuna mtu atasimama kwenye Foleni ya uchaguzi.
Mkuu Kama dunia ingekua na watu wanaofikiri na kukata tamaa hivyo dunia bado ingekua kwenye shimo la Giza totoro.
Kumbuka Mgurugenzi ni binadam kama wengine.
Asipodhibitiwa na kupata machungu atajiinua na kuangalia maslahi yake badala ya sheria kwa kuumiza wengine ili familia yake ishibe.
Eye with eye!
Kwenye mpira Refa aliyezoea kubeba timu yake , akijua kuwa timu pinzani wanajua kupigania haki yao na mashabiki wake wanajulikana kuwa hawana uvumilivu wa kuhujumiwa ni lazima refa afuate kanuni kuokoa pumzi yake.
Usifikirie hao CCM wanaofurahiya wizi wa kura hawajui kua kuiba kura ni kinyume na Vitabu vya duni,sheria za nchi na hata maadli ya binadam waliostarabika. Wanajua sana Ila wanachoangalia ni maslahi.
Mfamo Spika alituambiwa TL Mbunge kwa Mwaka mmoja amelipwa zaidi ya mil. 200 tena akiwa kitandani.
Chama tawala wanajua utam wa kushika funguo za hazina. Wanajua utam wa kushika dola.
Wapinzani bado wanashangaa shangaa wakati wenzao wanapambana.
Kila unayemuona anapambana kufa na kupona kutetea ugali wake.
Ukimuona anayegawa fomu anapigania ugali .Mlinzi anapigania ugali wake, anayegombea hasa wa chama tawala anataka agawiwe ugali wake kwa namna yoyote. Kama utakua na mgombea wa upinzani ambaye anasubiri apewe haki Mezani atapata makombo.
Usione watu wanahujumu wapinzani ni feza babu .
Wajipange kukabiliana na uovu wa kuhujumu zoezi la uchaguzi kwa namna yoyote mana wao ndio wanaotafuta nafasi za ubunge zenye maslahi na familia zao.
Kama mtu unapeleka mke wako kliniki Marekani halafu unalala kama ndezi uibiwe kura na vibaka halafu unabaki kulia badala ya kumliza mwizi ,utakua hujui umuhimu wa nafasi unayoitafuta.
Mtu unarudisha form peke yako barabarani halafu eti wanatokea vibaka wanakupora na wewe unabaki ukigaragara Chini kama mwehu badala ya kutafuta vijana wa kukusindikiza tena wakiwa na viberiti ili akijitokeza kibaka mporaji wa form basi anavuna anachopanda kama vibaka wengine.
Kila mtu alinde anachokitafuta kama ana uhakika wa kukipata.
Ni wazi kuwa Chama Kikongwe wamekua kama kundi la wapigaji wanaojipanga muda wote kufa na kupona ili tu washike nafasi za kuweza kuwapatia fedha za walipa kodi kwa UDI na uvumba. Hawa hawaangalii ubinadam wala sheria wanachojali ni kugawana nafasi za kupata hizo pesa.
Wakiachwa wanageuka kuwa kama wahalifu alimradi wapate nafsi hizo za ubunge ambazo zina maslahi makubwa.
Andiko lako limenitwanga viwiko(vipepsi) vya mbavuni.Umeandika vema.It's about time now we could have had an eye to an eye tactics!
 
Uzi mrefu sana lakini wenye kurudia rudia mambo.Uzi wote uumejielekeza kwenye Jambo moja tu nalo ni kutaka wanaoikosoa serikali au CCM humu JF wadhibitiwe na moderators.Kimsingi huna hoja yoyote ya maana zaidi ya hasira sababu unaona hoja unazozipenda kila zikiletwa humu zinapanguliwa kirahisi sana kama kunywa maji.
Mwisho,haki ya kusifia upande unaoupenda uliyo nayo na kuifurahia humu ni haki hiyo hiyo waliyo nayo wakosoaji na hawavunji sheria yoyote ya JMT.
Huyo mleta uzi anataka yeye na wenziye wa CCM wawe wanadekezwa,kubebwa,kuulizwa kama wamekula,wameshiba au wamependa muundo wa JF utadhani wapo picnic! Hahahahahaaa
 
Back
Top Bottom