Wanasiasa machachari, wasomi na wanaharakati na wanaoipenda zanzibar tuipinge necta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa machachari, wasomi na wanaharakati na wanaoipenda zanzibar tuipinge necta

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Malaria Sugu, Apr 28, 2011.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  imefika wakati wasomi, wanasiasa machachari na wanaharakati na wale wenye uchungu na kisiwa cha zanzibar kuangalia swala zima la baraza la mitihani la taifa.
  Elimu ndio msingi wa maisha, elimu ndio nguzo kuu ya nchi.
  Muundo wa baraza la mitihani unatia shaka na unaweza ukawa ndio source ya wanafunzi wa znz kufanya vibaya.
  Licha ya kuonekana kuwa la muungano. lkn sijwahi kusikia mzanzibar kushika nafasi kubwa ndani ya baraza hilo.
  Matokeo mabaya kwa wanz mitihani inayosimamiwa na NECTA inanifanya niwashauri wanasiasa na wanaharakati wa znz kuangalia tena swala hili na kuondolewa ktk swalazima la muungano.
  kwani inakuaje mitihani inayosimamiwa na NECTA wazanzibar ndio wanaongoza kwa kufeli huku mitihani kama hivyo ikisimamiwa na NACTE waznz hufaulu vizuri?
  LKN inakuaje wanafunzi wa znz wanaosoma vyuo vikuu huwa wazuri zaidi kuliko watz bara?
  Mfano znz sasa inavyuo vikuu 4. Licha ya wahadhiri wengi kutoka tzbara kama sheria inavyotaka. lkn vyuo hivyo ndivyo vilivyochini kwa wanafunzi kufeli.
  NACTE wana ajenda ya siri na znz?
   
 2. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Si Zanzibar tu hata hapa bara kuna mikoa au mashule ambako wanafunzi hawajawahi kufanya vizuri. hivyo hatuwezi kulaumu NECTA bali kuangalia ufundishaji katika mashule husika kama wanafunzi wanapata dozi ya kutosha ikiwa pamoja na mifano na mazoezi ya kutosha kuweza kujibu mitihani ya NECTA. Katika mashule mengi moyo wa ufundishaji upo chini sana kwa walimu. pia wanafunzi hawajitumi na hapo hapo shule zinaupungufu wa mahitaji lukuki ya muhimu kwa shule. ukichanganya vyote ndiyo matokeo yake hayo.
   
 3. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Is this Home of Great Thinkers?
  Nadhani ilikupasa kuleta hoja za msingi sana kuliko hii.
  Ungeweza kuhoji ni kwanini shule za Zanzibar hazina ufaulu mzuri ?na kuomba elimu iboreshwe lakini si hayo uliyoyaandika na kuyachanganya hapo.
   
 4. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi watu wengine akili zao zikoje? Kila kuicha znz tu, ina maana hapa tz wenye roho ni wazanzibar tu? toa hoja kama mtanzania sio kama mznz. Necta kama ina mkono wake kwa wanafunzi kufeli ni tz yote wala siyo znz peke yake.
   
 5. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Hoja za kipuuzi zitaisha lini? Hivi NECTA inahusikaje kufelisha wanafunzi tena Wazanzibari? We unadhan suluhisho ni kubadili uongozi wa Necta? Walimu, vitabu , maabara vitakuja kwa kuipinga NECTA? Alafu unajiita Mzee Wa hoja, upuuzi mtupu.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  NECTA ni ya wizara ya Elimu na Wizara ya Elimu ina shule zake. Cha kushangaza kuna shule zilizo chini ya TAMISEMI ambayo haina baraza lake la mitihani....!!
   
 7. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Mkuu. Hadi leo sijajua watu wengine wana matatizo gani. Kila failure wanaitafsiri kubaguliwa dini, mara uzanzibari mara sijui nini... Hivi hata mitihani ikija mtu mwenye mawazo kama haya atafaulu kweli (japo haimaaishi waliofeli wote wako kama huyu)?
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mbona baadh ya wazanzibari wanaosoma huku bara wanafaulu?hilo nalo haujiulizi?
   
 9. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Ndugu yangu usichanganye mitihani na utawala. Sasa hivi shule zote za msingi na sekondari zimepelekwa TAMISEMI kiutawala kwa maana ya ajira, maslahi, miundombinu, n.k. NECTA ambayo ni taasisi huru (autonomous) kazi yake ni kutunga na kusimamia mitihani. Kwa hiyo si lazima TAMISEMI iwe na baraza lake la mitihani kwa sababu si kazi yake. Ni mgawanyo mzuri wa majukumu unaoleta checks and balances.
   
 10. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mleta thread amekaa kibaguzi zaidi. Great thinker hawezi kuwa na mawazo kama hayo ya kutoa hitimisho kabla ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tatizo.
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,062
  Likes Received: 7,528
  Trophy Points: 280
  Nahisi tatizo ni binaadam kuwa mzanzibar, badala ya kuingia katika kiini cha tatizo anakuja hapa kulialia, kila siku ni malalamiko tu.
  Angalia namna Znz inavyosimamia mfumo wake wa elimu, na ni kwa kiasi gani wazanzibar wenyewe wanaipa elimu kipaombele ukilinganisha na mambo mengine.
  Au mnataka viti maalum vya ufaulu? kwa taarifa tu mnajidharirisha sana kwa kutoa malalamiko mengine, inaonekana kila litokeapo tatizo hamziandai akili zenu kwa ajili ya kulichanganua na kutafuta ufumbuzi bali mnaliangalia kwa akili za kutafuta sababu za kulalamika, kwa stlye hiyo hatutafika ndugu zetu. Mmeshakuwa sasa na mjitambue kuwa na nyie ni sehemu ya wanadamu ambao mchango wao unahitajika katika Dunia hii, badala ya kuwa walalmikaji kwa kila kitu
   
Loading...