Wanasiasa: Kwa nini mnaficha majina yenu humu ndani wakati tunajua mpo?

Status
Not open for further replies.

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
12,041
2,000
Mimi - I own up. Sababu yangu ni moja. Mimi ni conservative, mwanangu ni liberal na mjukuu ni independent-kizazi kipya. Kwa kuficha jina langu tunaweza kupambana kwa hoja bila woga kwa sababu humu hapendwi mtu. Kuna wakati mambo yanakuwa mazito na moto huwaka na ninashiriki nikijua niko upande tofauti na hao wawili. Can you imagine what it would be like kama wangejua wanajibizana na nani. Oh, my God!!
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,695
2,000
Si lazima mtu yeyote ku reveal jina lake halisi hapa.
Lakini nadhani hoja yake ili base kwa prominancy ya wanasiasa na hasa wale walio famous katika nchi hii maana "ndiyo yao iwe ndiyo na hapana yao iwe hapana" Wasiwe huku wana vote kwa ccm na in a secrecy way wana vote upande wa chama shindani. Hii ni double standard.
Hapa namaanisha ni vizuri ili kujulikana misimamo yao wazi, wajulikane hapa kama wenzetu Zito na Dr. wanavyojulikana na hata katika michang yao.
Lakini wakiendelea kjificha hapa hata huko kwenye vyama wanakuwa hivyo hivyo, na kamwe tutabaki kuwa na viongozi waliojaa uoga na wasio na courage ya kupoint matatizo moja kwa moja. Na hii itatufanya kubaki kwenye taabu ile ile kila siku.
Hata hivyo tujue wapo wapiganaji wa ardhini ambao ndiyo sisi. Wengine ni wafanyakazi wa serikali na waajiriwa wa mashirika ambao kwa wao tunapata datas na kuzipenyeza kwa wanasiasa. Sasa sisi hatuna haja sana ya kujulikana. Tubaki kama wapiganaji tunaopiga mizinga tokea mbali.
Haya ni mawazo yangu tu na hayamlazimishi yeyote kujiweka wazi kwa jina hapa jf.
Siku na mimi nikitoka katika ajira na kujiunga na Si-hasa, nitaweka jina langu hapa jf na mtashangaa kuona kumbe ni mimi!
Idumu milelel jf tusonge mbele tujikomboe kutoka katika makucha ya ufisadi.
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,398
2,000
labda Hawana Majibu Ya Maswali Ya Wananchi Dhidi Ya Tuhuma Dhidi Ya Serikali Na Chama Chao. Umewasahau Wanasiasa Wengine Humu Waliojitambulisha Freeman Mbowe, John Mnyika, Kitila Mkumbo Bila Kumsahau Asha Abdala, Wote Kutoka Chadema.

Yani Hata Balozi Wa Nyumba Kumi Tu Naye Anaogopa Kujitambulisha Humu, Sasa Itakuwaje Kwa Chiligati Na Makamba Nk!

Asha

Wajitambulishe Kwenye Forum Ya Chama Kingine.....!
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,350
2,000
Nafikiri kuna hoja hapa. Tunawapima wanasiasa na viongozi wetu kwa hoja na matendo yao. Hii forum inatoa nafasi ya pekee kujua misimamo ya watu kiitikadi, kifalsafa na kisera. Inaeleweka kwa wananchi wa kawaida kama sisi kuficha majina yetu, lakini kwa kweli sio jambo zuri sana kwa viongozi na wanasiasa wetu.

Wananchi wa kawaida hawawajibiki kujulikana misimamo yao na isitoshe wana haki ya kuogopa na/au kusita kujitambulisha waziwazi kwa sababu za misingi za kikazi, n,k.,Lakini mwanasiasa na kiongozi, ambaye tayari yupo katika public domain, na moja ya kazi yake ni kutoa mchango wa mawazo katika jamii, analazimika na kwa kweli ni lazima tumjue msimamo wake wa kimawazo kwa mambo mbalimbali kama vile ufisadi, n.k.. Sasa wanapojificha wakati tunajua hawana blog na wala hawaandiki makala kwenye magazeti, tutajuaje misimamo yao? Matokeo ya kushindwa au kukataa kujitambulisha kwa njia ya mawazo ndiyo hayo yanasababisha, wakati wa uchaguzi, wanasiasa wetu wategemee kuhonga ili wachaguliwe badala ya kujinadi kwa misimamo ya kihoja. Tubadilike.
 

Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
...hoja yake ili base kwa prominancy ya wanasiasa na hasa wale walio famous...

Wengine ni wafanyakazi wa serikali na waajiriwa wa mashirika ambao kwa wao tunapata datas na kuzipenyeza kwa wanasiasa. Sasa sisi hatuna haja sana ya kujulikana.

Siku na mimi nikitoka katika ajira na kujiunga na Si-hasa, nitaweka jina langu hapa jf ...

Dr. Slaa alishutumiwa Bungeni kutoboa toboa siri za nchi, siri za ufisadi. Ni Mpiganaji. Alishatoka Serikalini. Alifaa asitaje jina?

Vipi ambao ni wanasiasa lakini sio 'famous,' Nalaila Kiula, Richard Mja, Hawa Ghasia, Kitila Mkumbo, Juma Mkate?
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,006
2,000
Nafikiri kuna hoja hapa. Tunawapima wanasiasa na viongozi wetu kwa hoja na matendo yao. Hii forum inatoa nafasi ya pekee kujua misimamo ya watu kiitikadi, kifalsafa na kisera. Inaeleweka kwa wananchi wa kawaida kama sisi kuficha majina yetu, lakini kwa kweli sio jambo zuri sana kwa viongozi na wanasiasa wetu.

Wananchi wa kawaida hawawajibiki kujulikana misimamo yao na isitoshe wana haki ya kuogopa na/au kusita kujitambulisha waziwazi kwa sababu za misingi za kikazi, n,k.,Lakini mwanasiasa na kiongozi, ambaye tayari yupo katika public domain, na moja ya kazi yake ni kutoa mchango wa mawazo katika jamii, analazimika na kwa kweli ni lazima tumjue msimamo wake wa kimawazo kwa mambo mbalimbali kama vile ufisadi, n.k.. Sasa wanapojificha wakati tunajua hawana blog na wala hawaandiki makala kwenye magazeti, tutajuaje misimamo yao? Matokeo ya kushindwa au kukataa kujitambulisha kwa njia ya mawazo ndiyo hayo yanasababisha, wakati wa uchaguzi, wanasiasa wetu wategemee kuhonga ili wachaguliwe badala ya kujinadi kwa misimamo ya kihoja. Tubadilike.

Usisahau kuwa kuna protokali zinazowakataza viongozi kuzungumzia maswala fulani hadharani iwapo wao sio wasemaji rasmi.Dr. Slaa kwa jinsi anavyoingia kama Dr. Slaa hawezi kuzungumzia undani wa hekaheka za ndani ya CHADEMA hata kama atakuwa na hamu ya kufanya hivyo, ila akijiita mf. upara ataweza kusema yale yote anayotamani yawafikie wananchi.

Unadhani msemaji wa Rais anaweza kuingia humu na kutoa maoni yake iwapo yanapingana na matamko aliyoyatoa rais?huo ni mfano tu, basi tambua yapo mengi yatakosekana iwapo viongozi wataandika majina yao na JF itapoteza maana.
 

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
18,246
2,000
kwi kwi kwi kwiiiii wanaogopa kutaja lakini wamo...unaweza kusikia kumbe SHY ni makamba kwi kwi kwi kwiiiiii
 

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,699
1,225
Ndugu Kasheshe naomba unijibu jawabu la kweli, jee na wewe umeficha jina lako au kweli unaitwa Kasheshe ?

Kwi kwi kwi, tatizo mimi sili hela za Mfuko wa John Tendwa... au zile zinazopitishwa hivi sasa Pale kwenye Jumba tukufu!!!

Hivyo sio muhimu sana ninyi kunifahamu... by the way mimi kidampa tu!...

Jina langu ndilo hilo... kule kwetu maana yake.. ni... Jabali Kuubwa... si unajua majina ya kibantu!

Ingawa siku hizi jina langu mnalifanya liwe sijui kitu gani tena na viswahili vyenu vya pwani
 

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,133
0
Ina umuhimu gani kwa hao wanasiasa kutumia jina kamili kama wanagoma kujibu hoja? Nilishangaa Mh. Dr.Slaa alipomsikiliza Asha na kuacha kujibu maswali yangu ilikuwa ni halali yake. Bado nasubiri majibu yake na nitamkumbushia akija tena mtandaoni.

Una lako jambo wewe, Dr Slaa alikujibu kuwa majibu yangu niliyotoa ni sahihi kabisa na anakubaliana nayo na akakwambia kama hujatosheka na majibu hayo uliza swali mahususi, mpaka leo hujauliza unategemea nini? Yajadili yale majibu yangu kama hujaridhika nayo na ibua maswali sio kulalama tu. Dr Slaa hawezi kupoteza muda wake kujibu maswali ambayo yameshajibiwa kwa kuwa tu Kubwa JINGA hataki kuridhika. Halafu utaacha lini tabia yako ya kuuliza maswali kwa viongozi wa CHADEMA si kwa nia ya kujua bali kwa nia ya kuwatega tu?

Asha
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
12,606
2,000
Mkuu Kasheshe,

Hoja yako si mbaya ikiwa hili jukwaa lingekuwa ni la siasa tu.

Jukwaa hili ni pana sana na pamoja na mambo mengine limejumuisha jukwaa la siasa.

Sasa labda useme kwamba katika jukwaa la siasa pawe na majina ya kweli hapo ntakuelewa.

Ila ukumbuke kuwa Forum yoyote ile ni kwa ajili ya ku-air both positive na negative views ambazo miongozi mwa wanachama itakuwa na rahisi kuelewa kiufafanuzi au kimarejeo.

Kuna baadhi ya wanachama kama mimi si wanasiasa ila nnafikiri kwamba ntaweza kutoa mchango wangu wa maoni (wa kisiasa) na maoni kwenye majukwaa mengine kama la ICT (ambalo mim ni mtaalam), bila kujali kama jina langu linamkwaza mtu au vipi.

Wale wanaokuja kwa kasi ya kutaka kuharibu kwa matusi na midubwana mingine ni jukumu la moderators kuhakikisha wanawashughulikia.

Kw mantiki hio basi naona tuendelee kutoa maoni bila kuanza kuangalia na kutathmini maoni ya fulani na huyo fulani ni nani.
 

FairPlayer

JF-Expert Member
Feb 27, 2006
4,165
1,225
Kashehe,

Unachanganya vitu. Umeona mfano hai Mbowe alipoingia kama Mbowe, nini kilifuatia?

Hakuna haja ya watu kuingia na majina yao halisi humu!

Fair Player
 

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,699
1,225
Richard na Fairplay.

Mimi niliwazungumzia wanasiasa na public figures... hawa wengine na wataalamu kama ninyi wa Tekinohama na mambo ya kisasa endeleeni na anonymous zenu by the way ninyi sio public figures.

Kwangu mimi mwanasiasa anayejiamini uwezo wake wa kuchambua mambo na uwezo wake kwa maana uzalendo wake... ni jambo jema...

Lakini watu wasiokuwa na mpango kama akina fairplay wacha tu wakae na fairplay zao..
 

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mimi naamini kwamba mtu yeyote anayejificha chini ya kivuli wakati wa Mapambano aidha ni msaliti au ni mwoga...nothing else.. na huwezi kunambia otherwise..
Mapambano ya JF ni mapambano ambayo hayatakiwi kabisa kuogopa kitu chochote kama kweli una nia hiyo iwe serikali ama rafiki. Kilicho kuzuia wewe kutotaja jina lako hapa ni sababu ambayo inaonyesha wazi kwamba hutaki ujulikane... a smooth crimina na pengine unayosema ni UONGO! hivyo unaogopa watu kupima maelezo yako na wewe mwenyewe.
Sasa ebu, turudi ktk haki mnayoipigania hapa.. Huyu Kikwete, Rostam, Karamagi na wengine wataweza vipi kuyachukulia maneno yenu umuhimu ikiwa wanaozungumza wenyewe wanajificha!..Mbona sisi tupo na majina yetu na hakuna baya ambalo limeshatokea?.. why kina Zitto, Slaa, Kitila na wengine wamekuja na majina yao na hawana tofauti kabisa na wewe hapo ulipo kwa kila hali iwe usalama ama haki ya msingi..
Unajua kusema kweli hata mimi kama ningekuwa nafasi ya Kikwete, Rostam au Patel ningekuwa nikicheka saana kuhusiana na JF kwa sababu hizi ni porojo za kijiweni tu. Hakluna mtu ambaye anaweza kuzichukulia maanani hata kidogo tofauti na habari za magazetini. Ndio maana Magazeti yetu yakiandika kitu inakuwa issue lakini sio JF hata kama habari inaanzia hapa...
Unajua hata kama kuna habari mbaya sana umeambiwa na mkeo ukauliza nani kasema?...akasema nimesikia!.. basi mara 9 kati ya kumi mwanaume hupuuza. lakini kama habari hizo zitatoka ktk shina ambalo wewe mwenyewe unaliheshimu hata kama ziwe direct kwako sio kupitia kwa mkeo utasimama na kuyasikiliza...
Kinachofanyika hapa JF ni sawa na kumwona rafiki yako akizini akaacha kumwambia isipokuwa unaeneza habari mtaani.. unapoulizwa why humwambii yeye mwenyewe jibu lako ni kwamba hutaki kuiharibu urafiki ama kuvunja ndo..
Then don't talk period!
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,695
2,000
Vipi ambao ni wanasiasa lakini sio 'famous,' Nalaila Kiula, Richard Mja, Hawa Ghasia, Kitila Mkumbo, Juma Mkate?
Waoga tupu hawa nani ana uwezo huo wakati wanafikiri iko siku nao watapata nafasi ya kufisadi? Hawa wote si unasikia wameamua kula jiwe kama vile hawapo wala hawaoni nchi ya wajukuu wao inavyomezwa?Niliwahi kumsikia Kiula anakoromea serikali hii lakini naye si fisadi? kwani anaweza kujivua hiyo? Tena aliwahi kutolewa kafara! Wengine katika orodha yako hakuna wa kujaribu hata kukooa
 

NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
560
0
Labda hawana majibu ya maswali ya wananchi dhidi ya tuhuma dhidi ya serikali na chama chao. Umewasahau wanasiasa wengine humu waliojitambulisha Freeman Mbowe, John Mnyika, Kitila Mkumbo bila kumsahau Asha Abdala, wote kutoka CHADEMA.

Yani hata balozi wa nyumba kumi tu naye anaogopa kujitambulisha humu, sasa itakuwaje kwa Chiligati na Makamba nk!

Asha

Kumbe Asha ni mwanasiasa, nilikuwa sijuia asante mamii kwa kwa hilo
 

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,113
1,250
Ni aibu ya hali ya juu mwanasiasa ambaya anasema anatetea wananchi kuficha jina lake halisi akiwemo humu JF!


Binafsi nampongeza Dr. Slaa na Mh. Zitto kwa mara nyingine kuweka majina yao wazi... na hivyo pia kujua maoni yao katika mambo mbalimbali.

Ni heshima wanasiasa kuweka wazi majina yenu ili kuifanya JF kuwa chombo cha habari cha kuheshimika... na kupunguza wale wenzetu wanaofanya hapa ni mahali pa kupiga soga!

Mwanasiasa imara huwa hana woga wa kutoa maoni yake asikike! hata hivyo pia kwa kuwa wazi ana-promote transparency kwenye jamii yake.

Kwa vyovyote vile mnapoingia hapa kuna mnavyopata na tunawasikia mkitoa hoja kule kwenye lile jumba tukufu... tunaona kabisa maoni mumeyatoa hapa... ni wajibu wenu pia kurudishia jamii kidogo (social responsibility) kwa kutoa mawazo yenu ya ujumla na ya namna gani mnapenda JF iwe!

Mukiweka majina yenu... lengo la JF kuwa ya forum/jukwaa la KiJamii itakuwa imekamilika na kwa hakika tutaonekana sisi ni wazalendo wa hali ya juu kwa taifa letu.

Mwisho wenzetu mnaopenda matusi, kejeli na personality tupunguze tena ili kuvuta watu wengi makini.

wewe kasheshe hebu tuambie! kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake?
 

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Tukianza kutafutana majina hatutaishia hapo, tutaulizana makabila, ukoo, uzawa,... Hii ni sawa na kula nyama ya mtu.....
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom