Wanasiasa kutoa amri za kukamata watu, Wanasheria tupeni msaada

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,866
Naangalia gazeti la leo likisema Mkurugenzi aagiza polisi kumkamata Meya, Waziri aagiza waliohujumu Miundombinu kukamatwa. Hizo ni amri zingine ni majukwaani. Waziri aagiza mkandarasi akamatwe, nk.

Hawa ni wanasiasa na watendaji wa serikali wakitoa amri kwa vyombo vya dola. Je, kisheria nani hasa ana mamlaka ya kuamrisha vyombo vya dola?

Naona kama mawaziri wote wana madaraka ya kutoa amri za kukamata watu wanaohisi ni wahalifu! Miaka yote nimejua hiyo nguvu iko kwa Rais na Wakuu wa Wilaya na Mikoa, hawa mawaziri vipi?
 
Back
Top Bottom