wanasiasa kuanza kuhubiri kuwa kunaudini tanzania ndiyo munaoujenga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wanasiasa kuanza kuhubiri kuwa kunaudini tanzania ndiyo munaoujenga!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kituro, Jan 18, 2011.

 1. k

  kituro Senior Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwakuwa miaka mingi wananchi tumekuwa tukishirikiana pamoja mambo mengi ya kijamii, nilazima wanasiasa mjue kuwa sisi tuliishi tukijua dini zetu ni pale tunapokuwa kwenye nyumba za ibada na kwenye mikutano ya kidini. hali hii ilifikia mpaka watu wa dini nyingine waliamini kuwa dini zetu zinatufundisha namna ya kuishi na watu na tuwapo kwenye jamii na shughuri nyingi za kijamii ndo unafanyia mazoezi yale uliyofundishwa. mfano ukiambiwa msikitini ya kuwa ukimuelimisha mtu mmoja namna anavyopaswa kuishi kama muislam unathawabu zako. pia kama wewe utamfundisha mtu mambo mema nae uliyemfundisha akawafundisha wengine mambo mema nao wakatenda mema hivyo kwenye yale mafundisho mema wanayoendelea kutolewa nawe unasehemuyako ya thawabu hata yakiendelea kutolewa duniani wakati wewe mwenyewe ukiwa umeshakufa, wewe utaendelea kujikusanyia dhawabu kutoka kwa mwenyezi mungu. pia ukiwafundisha mabaya nao wakawafundisha wengine mabaya, hata wewe ukifa utaendelea kujipatia sehemu yako ya mabaya hayo. haya ni mafundisho ya dini ya kiislam ambayo ni dini inayotuasa kuwa utendapo mambo ya siyompendeza mwenyezi mungu ujue kabisa kuwa unaidhurumu nafsi yako.

  Pia kwakifupi kabisa mafundisho ya yesu yanasisitiza upendo siyo kwa wakristo wenzako bali ni kwawote. yatupasa kuwapenda jirani zetu siyo wakristo tu.

  wanasiasa wanaoanza kuhubiri kuwa tanzania kunaudini yatupasa wote tuwachukie, mbona hawahubiri mambo ya rushwa, ufisadi, na mambo ya viongozi wengi kupendelea huduma nyingi kupeleka kwao!

  nduguzangu katika jf huu ni mtazamo wangu , naomba kuwasilisha!
   
Loading...