Wanasiasa katiba siyo ya vyama vyenu ni ya watanzania wote hivyo tunaomba (msiteke mjadala)

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
Nionavyo mimi mjadala unaoendelea unaonekana kutekwa zaidi na wanasiasa kwa kila mmoja kuvutia kwa chama chake na kuona alichoona yeye watu waone ndicho sahihi. Hebu wawaache wananchi kwa fursa iliyopo waseme na watoe maoni yao na si kuwateka na wakati mwingine kuwachanganya
 
Mtoa mada, nadhani vyama vingi vya siasa vina lengo na nia moja nalo ni katiba mpya. Lakini chama kimoja tu ndiyo kikwazo nacho ni CCM. Napenda nikuthibitishie usemi wangu kwa vigezo vifuatavyo: Kwanza ni kwanini muswada wa katiba mpya ujadiliwe kwenye miji mitatu ya Zanzibar, Dodoma na Dar? Pili ni kwanini muswada uandaliwe kwa lugha ya kigeni kama kweli lengo ni kutaka kuwahusisha watanzania wote. Tatu ni kwanini mijadala ifanyike kwenye sehemu zenye nafasi finyu?
 
Back
Top Bottom