Wanasiasa kama siku nyingine mkijua hamjajiandaa kuzungumza na Watanzania kupitia Press, msiwe mnatusumbua

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
1. Mtu ni Mwanasheria kabisa lakini Kuzungumza mbele ya Press huwezi na unabaki Kuhangaika hangaika tu.

2. Hueleweki hata unataka kusema nini mbele ya Press na unabaki Kuzunguka zunguka tu.

3. Ujengaji wako wa Hoja ni wa Kitoto ambao hata tu katika Midahalo ya Shule za Upili (Secondary) huwezi Kuukuta.

4. Hujiamini na unaonekana ni kama vile ama Umetishwa au Ahadi uliyopewa imekuchanganya Akili (Ubongo).

5. Msomi mzima wa Sheria lakini muda wote unaongea na Press uwasilishaji wako umetawaliwa na maneno ya Kihunihuni tupu.

6. Mwanasheria lakini unaogopa Maswali wakati Mwanasheria na Maswali ni kama Lionel Messi na Kufunga Magoli La Liga.

7. Sasa kama ulijua mambo mengine huwezi Kuyatolea Ufafanuzi kwani ulikuwa na Kiherehere cha Kuitisha hiyo Press yako

Nilikuwa siwaelewi wapiga Kura wa 'Cow Way' waliposema kuwa 'huwafai' kabisa, ila kwa Upuuzi uiliotukuka wa leo hii nimeamini ulikuwa hutoshi.
 
Mimi sijaona alichoongea hadi hapo anaonekana ni mtu asiefaa kuawkiongozi wa watu huwezi kutumalizia muda watu tunasubiri ufafanuzi wa mambo mazito anakuja bila facts zaidi ya porojo tu.
Baba Askofu nilikuwa 'sikukubali' ila kwa 'Upuuzi' mkubwa ulio na Kiwango cha Kimataifa natamani uwe Mbunge wa 'Cow Way' hata Milele kabisa.
 
".....Wanachopaswa kufanya ni kutafuta eneo la ofisi hapo Dodoma, wafungue bank account, ruzuku yote ya Chadema, watakabidhiwa wao, na kulisongesha hadi 2025!. Uamuzi huu wa kulisongesha una changamoto moja, baadhi ya hao 19, ni wake wa ndoa wa wana CC wa Chadema, baadhi ni wenzi wanaoishi nao kinyumba na baadhi ni 'vidumu' vya viongozi wa Chadema, kushi nyumba moja, kulala chumba kimoja, kitanda kimoja kati ya kiongozi halali na muasi, ni changamoto!, tena kuna wengine wameisha anza kujenga familia, familia zisiparanganyiwishwe na siasa za kujinga jinga kama hizi!...." By Pascal Mayalla wa JF
 
Halima umedhalulika Sana ...hoja nyepesi Kama mavi .ya Bata!
Looh ama kweli Kuna watu wamedhamiria kuua Upinzani !
Ila kwa hoja hizi .....Mbowe ataendelea kuwa Shujaa wa DEMOKRASIA!
Kuna Mtu nilikuwa namheshimu na namkubali sana, ila kwa Upuuzi wake wa Leo GENTAMYCINE natangaza rasmi Kumdharau na Kumpuuza rasmi.
 
Nadhani tulichotarajia kusikia hatujakisikia...ndio maana kelele nyingi
Kwa taarifa yako tu GENTAMYCINE sikutaka labda aseme anaihama MADECHA yake na kuhamia MCC au anamuumbua Mheshimiwa Wembo ( Mwenyekiti ) au anamkama Kanyim ( Katibu ) bali nilikuwa nataka kuona 'Logical Arguments' zake na pia anionyeshe kuwa kweli Yeye ni 'Legal Guru' na alistahili kuendelea kuwa Mshika Jimbo la 'Cow Way' lakini leo kwa Upuuzi wake kanithibitishia kuwa kumbe Baba Askofu alistahili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom