Wanasiasa – hivi ‘ndugu’ lilikuwa na mapungufu gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa – hivi ‘ndugu’ lilikuwa na mapungufu gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jibaba Bonge, Mar 16, 2011.

 1. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Huko nyuma wakati wa uongozi wa Mwl. Nyerere watu wote tuliitana ‘ndugu’; raisi aliitwa ndugu raisi, Spika – ndugu spika, mbunge – ndugu mbunge, waziri – ndugu waziri na watu wasiokuwa na cheo chochote cha kisiasa pia waliitwa ndugu – ndugu fulani.
  Wabunge wetu kwa kutumia kodi zetu wakajadili mswaada bungeni na kupitisha (sijui kwa faida ya nani na kwa tija ipi?) kuwa wao (wabunge, Spika, mawaziri n.k) waitwe ‘waheshimiwa’ na raisi aitwe’ ‘mtukufu’!!! eti Mheshimiwa mbunge fulani, mtukufu raisi!!

  Ikiwa hizo title za mheshimiwa na mtukufu ni za hao wanasiasa je wale wasio katika makundi hayo ya kisiasa walipewa title gani? Kama hao waliotajwa ndiyo waheshimiwa na watukufu basi wasiokuwepo katika makundi hayo ya kisiasa hawaheshimiwi na wala siyo watukufu!
  Pamoja na title kubwa kubwa walizo jipa wameendelea kufanya madudu katika uongozi wa nchi yetuHali hii imeleta matabaka makubwa kati ya waheshimiwa na wasioheshimiwa na kuwafanya watu watafute kuitwa waheshimiwa kwa gharama yoyote.
  Hivi Title ya ‘ndugu’ kwa wanasiasa ilikuwa na mapungufu gani?
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Falsafa za nyerere zilizokufa kabla yake mwenyewe.
   
Loading...