sabuwanka
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 690
- 751
Wakongwe wa jukwaa hili, nawasilimia shikamoo!
Baada ya shikamoo hiyo, tangu JPM aingie madarakani kumekuwa na wimbi la wanasiasa kuhama kutoka CHADEMA kwenda CCM, CHADEMA kwenda ACT, ACT kwenda CUF, n.k. Wengi wao walipewa ridhaa ya kuongoza katika nafasi za udiwani na ubunge ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Ikiwa kiongozi anahama kabla ya kutimiza majukumu na ahadi yake, basi lazima kutakuwa na mdororo wa mipango ya maendeleo katika kata au jimbo au nafasi aliyokuwa akisimamia maana anajua hatadumu, hapo anapita tu!
Halikadhalika, public figures kama Lowassa na Sumaye waliaminiwa na wafuasi wao, wakahamia CHADEMA, wakaaminisha umma CHADEMA ndicho chama bora kuliko vyote. Wakahama tena toka CHADEMA na kusema watabaki bila vyama.
Kabla hapajakucha, wamerudi tena CCM. Wapo akina Zitto, Maalim Seif na wengine wengi!
Je, wanasiasa hawa ni wa kuwaamini? Ni kweli wana uchungu na nchi hii kama wanavyotuaminisha? Au ni uchungu wa masilahi yao kuguswa?