Wanasiasa acheni kuwaonea huruma watu wenye ulemavu bali wapeni haki zao

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,164
9,371
Jana na leo kumetrend ' habari na picha ya Waziri Mkuu akitoa msaada kwa binti mwenye Ulemavu.

Habari hiyo imenogeshwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa kumuonesha Waziri Mkuu akilia kwa namna alivyopata uchungu kutokana na matatizo ya binti huyo.

Tumeambiwa Mh. Rais pia amechangia kiasi cha fedhaa ili kumjengea nyumba binti huyu. Hili ni Jambo jema!

Majuzi Naibu Waziri alioneshwa akichapa viboko na kuwakamata watu wanaowatumia watu Wenye Ulemavu kuombaomba MItaani!

Viongozi hawa wote Waziri, Mkuu na Naibu wao ndio wenye dhamana na Watu Wenye Ulemavu.

Matukio haya yanafikirisha! Watu wenye ulemavu ni kundi tete ambalo linahitaji afua nyingi kuliwezesha kuishi maisha ya kawaida.

Ni ajabu kuona Waziri Mkuu analia, kumhurumia mlemavu mmoja, huku maelfu yao wako maajumbani wanatesekana familia zao! ilihali yeye ndiye Mkuu wa Serikali na Usimamizi wa Sera na Sheria yaWatu Wenye Ulemavu upo chini yake naSerikali haijafanya chochote Cha maana kwa kundi hili.

Watu wenye Ulemavu wanaombaomba barabarani kwa sababu ya Umasikini na kukosa elimu!

Hili ni jukumu la Serikali kama ilivyoelezewa kwenye Sera na Sheria. Waziri aache kulia mbele ya kamera awekeze kutekelza sheria na Sera ili awakomboe kundi Hili.

Kumjengea mlemavu mmoja nyumba,na kujimwambafai' kwenye vyombo vya Habari ni sawa na kumpa 500/ ombaomba mlemavu barabarani ,tofauti hapa Ni kuwa huyu kabahatika kukutana na Wanasiasa Wenye ukwasi!

Kuna familia nyingi zinalea watoto wenye multiple disabilities,familia hizi zinahitaji kusaidiwa ,kumhudumia mtu Kam huyu Ni gharama kubwa kwa sababu Ni lazima mwanafamilia mmoja aacheshughuli zake na kukaa nyumbani!

Serikali inashindwa Nini kuwapa Ruzuku familia Kam hizi?

Nafikiri ni wakati muafaka kwa Serikali kusimamia Sera na Sheria kuhusu kundi hili badala kuendelea kuhudumia kwa matukio ambayo mwisho wa siku inakuwa ni SIASA TU!

Serikali inaweza kweka Kodi Ndogo tu kwenye shughuli za Kiuchumi ili kuchangia Mfuko wa Watu Wenye Ulemavu.

Mfano wanywaji vileo,wakachangia hata Sh.10, kwenye madini na uwekekezaji mwingine au wabunnge wakachangia asilimia 2 mishahara na posho zao ilikutunisha Mfuko wa Watu Wenye Ulemavu, hivo kwenye muziki na michezo mingine!

Mheshimiwa Waziri Mkuu, unathaman na kundi hili. Simamia Sera na Sheria badala ya kulia mbele ya Kamera!

Watu Wenye Ulemavu wanaahitaji kutimiziwa Haki zao na sio kuonewa Huruma!
 
Back
Top Bottom