Uchaguzi 2020 Wanasiasa acheni kututisha, sio lazima tuwachague

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,864
ACHENI KUTUTISHA, SIO LAZIMA TUWACHAGUE.

Na, Robert Heriel

Kuna wanasiasa wanatabia za hovyo sana. Hivi ninyi wagombea mnajichukuliaje? Au mnafikiri sisi tunawachukuliaje? Mnafikiri tunawaona ninyi ni watu spesho sana kuliko watu wengine? Kwa taarifa yenu, Mimi Taikon na watu wa aina yangu huwa tunawachukulia kama watu wengine. Ninyi ni watu wa kawaida kama binadamu wengine. Hamna la ziada.

Mwenye ziada ni yule anayemcha Mungu, yule anayeshika mapenzi ya Mungu, yule anayetenda haki iliyo ya Mungu. Vinginevyo hakuna la ziada kwenu.

Kuna watu wakipata mabadara wanafikiri wanaweza kuwafanya wanadamu wote wawaabudu, wawasujudie, hata uwe na nguvu zinazokaribia nguvu za Mungu aliyehai, ilimradi wewe sio Mungu basi hutatufanya sisi Mataikon kukuabudu na kukusujudu.

Hata uwe na cheo gani, uwe na mali gani, uwe na ulinzi wa aina zote, uwe na elimu zote kama unatafuta kuogopwa, kuabudiwa, kusujudiwa, hakika, mimi Taikon nitakudharau, sitakuheshimu, bila kujali utatumia vitisho gani, bila kujali Mungu atakupa nafasi gani ya kufanya maamuzi yoyote juu yangu, wewe utabaki kuwa mtu kama watu wengine.

Huwezi amulia watu kiongozi wao, huwezi amua watu wakuchagua, huwezi kuwalazimisha, huo ni wendawazimu. Huko ni kjifanya mungu mtu wakati huna umungu wowote.

Nimesikitika kusikia moja wa wagombea wa Urais kuwatishia wananchi kuwa wasipochagua kiongozi amtakaye ati watajuta, ati hatawaletea maendeleo.

Hizi ni dharau, jamii hiyo iliyoambiwa imedharauliwa, wanaume waliosikia kauli hiyo wamedharauliwa, huwezi ongea kauli za hovyo mbele ya watu wenye akili.

Wewe sio Mungu, Wanasiasa lazima muelewe, ninyi sio miungu, ninyi ni kama watu wengine. Zaidi ya yote wengi wenu mnatumikia matumbo yenu. Ati mtajuta, wewe nani bhana!

Watu hawajamchagua Mungu na wanapeta, Mungu kawaachia uhuru wa kujichagulia, aidha wamtumikie yeye au miungu, na bado hajaongea upuuzi wenu,ati tutajuta.

Tutajuta wewe ndio umeumba dunia, wewe ndio umeumba watu? Wewe ni nani utishie watu wakuchague?

Demokrasia ilianza zamani tangu kipindi cha Musa na Nabii Joshua.
Joshua anawaambia wana wa Israel waamue watakayemtumikia. Lakini yeye na nyumba yake watamtumikia Bwana, Mungu. Hakuwalazimisha, ati ni lazima wafuate uamuzi wake wa kumchagua Mungu.

Ikiwa Mungu alituumba na mwenye nguvu hajatuambia tutajuta tusipomchagua, wewe ni nani hata ututishie? Wewe ni nani? Unadhani unavyojidanganya ndivyo ulivyo? Unadhani uanvyojidanganya ndivyo utatutishia sisi kuwa tukuchague ili tusijute.

Huwezi amulia watu kiongozi wamtakaye, wewe ni nani?

Watu wanaopenda kuabudiwa hutishia watu wasiomjua Mungu.
Maisha yetu hayawategemei ninyi wanasiasa kwa chochote.

Na kama kuna mtu anadhani tutamuabudu, tutamuogopa ama tunamtegemea huyo hana akili, na wanaotegemea hao wanasiasa nao hawana akili.

Wewe utegemewe kwa kipi hasa? Unatisha watu wasiomjua Mungu. Yaani wewe ambaye hukuwepo, na siajabu kesho ukawahaupo ndio watu waweke rehani maisha yao kwako.
Labda wapumbavu kwa maana Mpumbavu alishasema moyoni mwake hakuna Mungu, ndio maana anawategemea ninyi miungu mshenzi.. Miungu ambayo usiku ukifika mnalala, miungu ambayo hamuwezi kukaa bila kula, hivi kweli ninyi ndio mtutishie.

Lazima muelewe, ninyi ni watu kama watu wengine. Tutawaheshimu kama tunavyowaheshimu wengine. Tutawaheshimu kwa kuwa mnatenda haki, mnafanya yaliyoya Mungu. Pia tutawadharau kama tunavyodharau watu wengine, tutawadharau ikiwa hamjui kutenda haki, naama hamfuati maagizo ya Mungu.

Ati mtu aogope kukukemea ukitenda uovu kisa umemuajiri sijui, sijui wewe ni boss wake, mara sijui ati usikemewe unapokosea kisa hutanipa ajira, ajiraaa! Ajira ndio inifanye nikuabudu au nikusujudie hata nishindwe kukwambia ukweli. Hiyo kwangu haipo.

Kama ni kuajiri acha kuniajiri, kama ni kuongeza sijui ni hiyo mishahara acha. Kama utakataa kujenga miundombinu acha, lakini sio ujifanye Mungu mtu wakati huna umungu wowote.
Alafu uone kama nitajuta.

Watajuta hao wanaokutumikia na kukuona Mungu wao kisa wanalinda vibarua vyao, watajuta hao wanaojipendekeza hata ufanyapo mabaya wakashindwa kukwambia ati kisa uwape teuzi, sijui ajira.

Wanasiasa muache tabia zenu za hovyo. Msije mkadhani nafasi tunazowapa zinawabadilisha kuwa Mungu. Ninyi ni watu tuu. Tutawaheshimu kwa mambo ya haki na wala sio jambo lolote. Hatutawaheshimu kisa mnatupa upendeleo, hatutawaheshimu kisa mnatuletea maendeleo, hatutawaheshimu kisa mnatuajiri au kutupa mishahara mikubwa. Tutawaheshimu kwa sababu ya haki, naam kufanya haki iliyo ya Mungu.

Huwezi jifanya Mungu alafu tukupigie makofi. Ati tutajuta! Duuuh!
Tutajuta ikiwa tutashindwa kumuabudu Mungu wetu.
Tutajuta ikiwa tutashindwa kutenda haki iliyo ya Mungu.
Tutajuta ikiwa tutaacha dhuluma itawala na haki ikandamizwe.
Tutajuta ikiwa tutawaabudu miungu mshenzi ambao tunagombania pumzi na chakula ili tuishi.

Lakini kama tunatenda haki na kuisimamia kamwe hatutajuta hata tuingie katika matatizo ya mpito.

Ujumbe huu uwafikie wale maboss wote wapumbavu wanaotaka kuabudiwa kwenye makampuni na sekta zote. Uabudiwe kwa kipi hasa? Ni hizo fedha. je ni mali, je ni cheo, hahahah! Kuna watu wapumbavu sana.

Ujumbe huu uwafikie wale wafanyakazi na watu wote wanaoabudu miungu mshenzi ambayo nayo inalala kama wao. Ati kwa kisingizio cha kazi, sijui mshahara, sijui atafukuzwa au kushushwa cheo.

Mungu ndiye anaweza kukushusha cheo hao wengine wapuuzi tuu. Na wanajua jambo hili ninalo lisema.

Zingatia; USIABUDU MIUNGU MINGINE ISIPOKUWA MUNGU ALIYEKUUMBA.
Usiogope mtu ikiwa unatenda haki, ni heri ufukuzwe kazi kuliko kumtumikia shetani anayejifanya ni mungu kumbe hana lolote.

Zingatia pia, kila mwanadamu anayetenda haki na kumcha Mungu anastahili kuheshimiwa. Tofauti na hivyo usimkopeshe mtu. Akitenda uovu mkemee, akikufukuza kazi mwambie NASHUKURU. Mtu yeyote asiyetenda haki anastahili kudharauliwa

Yaani umfanye mtu Mungu kwa pesa ipi hiyo anayoweza kukupa. Kwa ajira ipi hiyo ya maana atakayokupa. Looh!

Nakala ziwafikie hawa
1. Wanasiasa wote
2. Viongozi wote
3. Wakurugenzi wote
4. Maboss wote
5. Na wale wazazi wanaojifanya Miungu watu.

Acheni kutisha watu, dunia hii sio yenu, hamna la ziada nanyi mnajua hivyo. Mwenye la ziada ni Mungu pekeake na wale wanaomcha yeye.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kutoka Nyota ya Tibeli
0693322300
 
Back
Top Bottom