Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Wameelimika na wanajua mengi. Tunawategemea, kuwathamini na tungependa kuwaenzi. Lakini kabla hatujaanza kuwaenzi, labda tujiulize, hivi wengi wao na kampuni zao na jumuiya zao mbalimbali kweli wanathamini Taifa hili?
Najiuliza kama wanathamini uzalendo au wana uzalendo wowote ule kutokana na mlolongo wa madudu ya kifisadi kwenye mikataba mbalimbali nchi hii imepata kuingia na mashirika au kampuni mbalimbali za nje, haswa kwenye sekta ya madini na nishati.
Hivi kweli chi yetu inapokuwa inapunjwa kila pahala wako wapi hawa? Najua wanafahamu sehemu za kurekebisha na sehemu zenye makosa, wako privy na mambo mengi yanayotokea kwenye maslahi ya Taifa lakini kwanini wako kimya? Je kila mmoja anajali maslahi yake tu binafsi? Wana uzalendo wowote kweli hawa??!!!