Wanasheria wetu nisaidieni kujua pamoja na Babu Seya kusamehewa, je hatia ya kosa alilopatikana na Mahakama limefutika?

Kapilipoint

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
381
343
Kuna mtu tunabishana kuwa ukipatikana na hatia na Mahakama ikakupa ADHABU na baada ya muda fulahi ukapata msamaha Wa Mh .Rais ni kwamba utakuwa Huru ila ile hatia ya Mahakama itaendelea Kubaki kwenye kumbukumbu.Mwingine akasema Msamaha unafuta ile hatia ya Mahakama.Je Kwa mujibu Wa Sheria usahihi ni Upi?
 
Kwa Tanzania hilo linawezekana lakini kiweledi msamaha wa rais haukuondolei hatia
 
Wala huitaji wanasheria hapa.

Kusamehe hakufuti hukumu. Ni neema ama ahuweni mtu anayopewa kutokana na kujutia kosa lake. Hivyo kosa liko palepale.
 
Kuna mtu tunabishana kuwa ukipatikana na hatia na Mahakama ikakupa ADHABU na baada ya muda fulahi ukapata msamaha Wa Mh .Rais ni kwamba utakuwa Huru ila ile hatia ya Mahakama itaendelea Kubaki kwenye kumbukumbu.Mwingine akasema Msamaha unafuta ile hatia ya Mahakama.Je Kwa mujibu Wa Sheria usahihi ni Upi?
Msamaha haufuti kosa. Ukitiwa hstiani na Mahakama inabidi Mahakama ndio ikuondolee hatia na siyo msamaha. Msamaha unaondoa tu adhabu. Nakumbuka Rage wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa FAT alihukumiwa kifungo na Mahakama ya hakimj mkazi Kisutu, akafungwa. Akiwa kifungoni akakata rufaa na kabla rufaa haijatolewa hukumu akapata msamaha, hakufuta rufaa bali iliendelea hadi hukumu ya rufaa ikatoka na akawa ameshinda na hivyo kosa lake likawa limefutwa na mahakama na si kwa msamaha.
 
Back
Top Bottom