Wanasheria washauri Zanzibar kuunda tume ya mabadiliko ya katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria washauri Zanzibar kuunda tume ya mabadiliko ya katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Mar 26, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanasheria washauri Zanzibar kuunda tume ya mabadiliko ya katiba | MZALENDO.NET

  Written by administrator // 19/03/2011 // Habari-Picha, Kitaifa // 20 Comments

  [​IMG]
  Na Salma Said,
  KONGAMANO la kudajadili katiba mpya ya Tanzania linaloendelea kufanyika Zanzibar limechukua sura mpya baada ya wanasheria na wananchi kuishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuunda tume yake ya kukusanya maoni badala ya kutumia tume ya pamoja ya Muungano.
  Wito huo umetolewa jana washiriki mbali mbali wakati wakijadili mada kuhusu katiba za Tanzania na Zanzibar, changamoyo juu ya mianya na utata uliopo iliyowasilishwa na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim katika ukumbi wa Eacrotanal Mjini Unguja.
  Mwanasheria maarufu Zanzibar, Awadh Ali Said amesema Zanzibar haitonufaika na mjadala wa marekebisho wa katiba ya Muungano kama tume itafanya kazi hiyo ya kukusanya maoni Tanzania bara na Zanzibar kutokana na wananchi wake ni wachache kulinganishwa na Tanzania bara.
  Kwa msingi huo alisema ili haki itendeke na kupata maoni ya mustakabali wa muungano juu ya muundo na aina ya Muungano ni vyema kukawa na tume mbili zitakazofanya kazi hizo moja upande wa Tanzania bara na nyengine Zanzibar.
  “Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iunde tume yetu ya kukusanya maoni kwa sababu tupo wachache na tukiwa katika mkumbo wa pamoja hatutanufaika kulinga na mazingira ya Zanzibar” alisema Mwanasheria huyo huku akipigiwa makofi na washiriki wa kongamano kuonesha kuwa wanamuunga mkono.
  Alisema Zanzibar ina mambo mengi ya kujadili kuhusu maslahi ya Zanzibar ikiwemo suala la jumuiya ya afrika mashariki kutokana na kuwa kuna mambo ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya muungano kama afya, utalii na kilimo na ndio maana ipo haja kwa Zanzibar kuwa na ushiriki katika jumuiya hiyo ili iweze kutetea ipasavyo maslahi yake.
  Naye Ahmed Omar Khamis alisema rais wa kwanza Zanzibar, Mzee Amani Karume hakuwa na mchango mzuri katika kuandaa makubaliano ya muungano na ndio maana kero nyingi zinajitokeza baada ya kutozingatiwa maslahi ya kisaisa na kiuchumi.
  Hata hivyo alisema kwamba ili marekebisho ya katiba yalete faida na kuondoa kero zilizopo hivi sasa lazima kuwe na tume zitakazoweza kufanya kazi tofauti ikiwemo tume ya maoni ya Zanzibar na tume ya maoni ya Tanzania bara.
  Alisema tume zilizopita ikiwemo ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali zilifanya kazi za kukusanya maoni kuhusu muungano lakini hadi sasa hakuna utekelezaji wowote uliofanyika kutokana mambo hayo yalitawaliwa na ujanja ujanja na kutahadharisha lazima umakini uwepo katika suala hilo.
  “Tunaweza tukaletewa tume hapa kama zile za kina Jaji Kisanga na Jaji Nyalali zikatembea Tanzania nzima kukusanya maoni na matokeo ya tume hizo tukaja kuuambiwa asilimia 80 wamesema hivi na asilimia ishirini ndio wamesema hivi kwa hivyo bila ya shaka kwa kuwa sisi kidogo tutaonekana ni wachache kwa hivyo jambo la msingi hapa kuundwe tume itakayokusanya maoni kule Tanzania bara na sisi tuwe na tume yetu ambayo ikusanye kwa mujibu wa idadi yetu” alisema kijana huyo.
  Akichangia katika mjadala huo Omar Mussa Makame alisema katiba ya muungano inahitaji kuangaliwa kwa umakini kwa vile sio mwafaka rais wa Zanzibar kula kiapo cha kutii na kulinda katiba ya muungano wakati amechaguliwa kwa katiba ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar mbali na kuapishwa kulinda katiba ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano hulazimika kula kiapo mara mbili cha kulinda na kutetea katiba ya muungano akiwa kama waziri asiyekuwa na wizara maalumu katiba baraza la mawaziri la Muungano.
  Akiwasilisha mada yake Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim alisema vifungu vingi vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vina kasoro na kutoa mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano anateuwa mawaziri kwa kushauriana kwa kushirikiana na waziri mkuu bila ya kushauriana na makamu wa kwanza wa rais au rais wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Aidha alisema kwamba katiba hiyo ya Jamhuri ya Muungano imempa uwezo rais wa Jamhuri ya Muungano kuteuwa mawaziri kutoka Zanzibar na kuwapa madaraka katika wizara ambazo hazihusiani na masuala ya Muungano jambo ambalo linahitaji kujadiliwa katika marekebisho hayo ya katiba mpya.
  Mzee alisema utata wa katiba katika jamhuri ya Muungano pia upo katika ibara ya 64 wakati bunge la jamhuri limepewa uwezo wa kutunga sheria zitakazotumika hadi Zanzibar wakati katiba ya Zanzibar ibara ya 132 imeweka wazi hakuna sheria itakayotungwa ambayo haihusiani na masuala ya muungano kutumika Zanzibar hadi itakaporidhiwa na baraza la wawakilishi.
  Katibu huyo wa baraza pia alitoa mfano wa wizara ya mambo ya ndani na wizara ya ulinzi kuwa yapo mambo ndani ya wizara hizi hayamo katika orodha ya mambo ya muungano kama vile kikosi cha zima moto, magereza, na jeshi la kujengwa taifa JKT lakini wizara hizo zimekuwa zikiongozwa na wazanzibari na kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya muungano.
  Alisema hizo ni kasoro za kikatiba ambazo zinahitaji kuangaliwa pamoja na kesi za uchaguzi zinazohusu wabunge ambapo masharti ya katiba yameweka kesi hizo zisikiliziwa na mahakama kuu ya Tanzania wakati suala la mahakama halipo katika orodha ya mambo ya muungano na kila upande ina mahakama kuu yake.
  Mjadala huo wa katiba mpya unayatarishwa na jumuiya zisizokuwa na kiserikali na suala la urais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa muungano limekuwa likichukua nafasi kubwa katika mjadala huo kwa wajumbe baada ya wananchi wengi kupinga marekebisho ya 11 ya katiba yaliofuta wadhifa huo.
  Jumuiya zisizokuwa za kiserikali zilizoandaa kongamano hilo ni jumuiya ya waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA), jumuiya wa wanasheria Zanzibar(ZLS), Kituo Cha Huduma za Cheria Zanzibar (ZLSC) na Taasisi ya Utafiti wa Historia Ukanda wa Bahari ya Hindi Zanzibar (ZIORI)
  Sikiliza wachangiaji wa kongomano hilo:
  #gallery-1 { MARGIN: auto}#gallery-1 .gallery-item { TEXT-ALIGN: center; MARGIN-TOP: 10px; WIDTH: 33%; FLOAT: left}#gallery-1 IMG { BORDER-BOTTOM: #cfcfcf 2px solid; BORDER-LEFT: #cfcfcf 2px solid; BORDER-TOP: #cfcfcf 2px solid; BORDER-RIGHT: #cfcfcf 2px solid}#gallery-1 .gallery-caption { MARGIN-LEFT: 0px}[​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [​IMG] [​IMG]


  Picha zote kwa hisani ya Salma Said,
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopinga ya kuwa yako mapungufu ya wazi kwenye katiba

  Tambwe na wapiga porojo wenzake wa CCM (akiwamo Rais wake) wanataka Watanganyika tusione kuwa kuna mkanganyiko wa kikatiba kati ya nchi hizi mbili..afadhali wazanzibar mnaliweka hili wazi iwe aibu kwao

  Hongereni kwa kuyajadili haya............ japo nilipenda zaidi katika kujadili kwenu mngenuia kuleta mapendekezo wakati wa katiba mpya muondoke kwenye Muungano.......Na kama mlivyosimama ngangari kwenye katiba yenu kwa kutaka kura ya maoni, wekeni pia ungangari kwenye hili ili muamue kama mnataka kuwa sehemu ya Muungano au kuwa nchi huru inayojitegemea kabisa na uhuru wake wa kimipaka...........................! Hili linachangiwa na ule msisitizo wetu kuwa katiba ibadilike maana haina ridhaa yetu wananchi jambo sawa na Muungano ambao haukuwa na ridhaa ya wananchi...Ili uwe wa wananchi na sio wa Nyerere na Karume (au viongozi peke yao) amue kuitisha kura ya maoni ya kutaka Muungano.....

  Mkija kwetu tutawapa na sapoti hata ya nauli ya kuondokea Muungano

  Kwa ninavyowaona wazanzibar wengi wakati huu na matamshi yao ninawafananisha na kijana aliebalehe anaetaka kujitegemea lakini wazazi wake wanang'ang'ania abakie nyumbani......anaweza wageuka hata dada zake kama asipotazamwa vizuri
   
Loading...