Wanasheria, wanasiasa, wampinga Rais Kikwete

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,847
Posted Date::10/12/2007
Wanasheria, wanasiasa, wampinga Rais Kikwete
Na Waandishi Wetu


BAADHI ya wanasheria na wanasiasa wamepinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete kahidi ya wapinzani iliyowataka kuacha kutoa tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali, wakisema kuwa wana haki kufanya hivyo nchi inayoendeshwa kwa utawala wa sheria.

Wakizungumza na gazeti hili jana kwa nyakati tofauti, wanasheria hao walisema sheria inalinda haki ya kutuhumu na haimlazimishi anayetoa tuhuma kuzipeleka kwenye vyombo vya dola au kuzithibitisha mahakamani.

Mwasheria wa Kampuni ya Mawakili ya Masaka ya jijini Dar es Salaam, Proscovia Chrisant, alisema kuwa sio lazima kwa anayetuhumu kwenda kuzithibitisha tuhuma zake mahakamani, badala yake anayetakiwa kwenda vyombo vya dola ni yule anayetuhumiwa na kudhani kuwa tuhuma hizo zinamshushia hadhi mbele ya jamii.

Naye Mgoha George wa Kampuni ya Mawakili ya Kakamba & Parterners ya jijini Dar es salaam, alisema kuwa wajibu wa kuthibitisha kwamba kilichosemwa ni uongo ni wa mtuhumiwa ambaye kwa vyovyote atadai fidia baada ya kupata tuhuma ambazo anaamini kuwa zinamvunjia heshima katika jamii.

Hata hivyo, alisema kuwa ni busara kwa mtuhumiwa kujichunguza kwa makini kabla ya kufikia uamuzi wa kwenda mahakamani na kudai fidai, kwani kwa kawaida tuhuma nyingi zinatolewa baada ya watu kuwa na ushahidia wa kutosha.

Mwanasheria mwingine Steven Mtetewaunga, alisema kuwa kauli ya Rais kutaka wapinzani kuacha kutoa tuhuma siyo sahihi, kwani inabeza uhuru wa kutoa maoni katika jamii.

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic, Mchungaji Christopher Mtikila alisema suala la mtoa tuhuma kwenda mahakamani au kupeleka ushahidi kwenye vyombo vya dola sio sahihi badala yake vyombo hivyo vinatakiwa kufuatilia tuhuma hizo na kutolea uamuzi.

Mtaalamu wa Masuala ya Siasa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana, ambaye ni Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala chuoni hapo alisema ipo haja ya serikali kutafuta namna ya kujisafisha dhidi ya tuhuma za ufisadi wa baadhi ya viongozi wake.

Naye Mwanasheria na Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu hicho, Dk Sengondo Mvungi, alisema kauli hiyo ya rais imepotosha kutokana na mtiririko wa matukio unaonyesha jinsi iongozi wa serikali wanavyotumia mbinu nyingi kubana hoja za wapinzani.

Wakili wa Kujitegemea Gregory Lugaila, alisema kwa katiba na sheria za Tanzania haiwezi kuitokomeza rushwa mpaka sheria itakapobadilishwa, kwa sababu iliyopo hivi sasa inalenga kuwalinda walioko madarakani.

Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Paul Chobo, alisema kisheria tuhuma zozote lazima zichunguzwe ili kubaini ukweli kwa sababu zinaweza zikawa za ukweli ama za uongo, hivyo ili kubaini ukweli ni lazima zichunguzwe.


Habari hii imendikwa na Kizitto Noya, Andrew Msechu na Jackson Odoyo

Source: Mwananchi
 
duh enzi za jk mlikuwa mnajibisha Kwa maneno vitendo kidogo tu ila enzi hizi vitendo vingi (kipigo cha mbwa koko) maneno kidogo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom