Wanasheria wa CHADEMA ratibu ukusanyaji ushahidi dhidi ya Sabaya maana ukatili mwingi walifanyiwa wanachama wa CHADEMA

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,078
2,000
Hii ina mantiki kubwa. Ukatili ulio mwingi walifanyiwa wafuasi wa Chadema, ni vema CHADEMA ikaratibu ukusanyaji wa ushahidi dhidi ya Sabaya ili haki itendeke. Waandae waathirika waweze kutoa ushahidi wa kweli na si vinginevyo. Walindwe dhidi ya vitisho vya Sabaya na genge lake etc........
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,024
2,000
Ushahidi wa kuwatoa akina Halima Mdee bungeni umewashinda ndio mtauweza wa Sabaya?

Acheni dola ishughulike na Sabaya.
 

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,703
2,000
Ila chadema huwa wanakwama kwenye mambo ya msingi sana sijui ni vipaumbele au kitu gani huwa kinawaponza.

Kuna muda (mwingi) chadema inashindwa kabisa kufanya kazi zake kama taasisi. Ni kweli wanatakiwa kujikusanyia ushahidi na ripoti za kueleweka wawasilishe kunapostahili.

Naona chadema wana kila sababu ya kukutana na Mh. Raisi
 

Noti bandia

JF-Expert Member
May 3, 2020
805
1,000
No. Ukishaleta uchadema kwenye hiyo kesi ukumbuke pia kutakuwa na u ccm. Nafikiri mwisho wa kesi ushaujua utaishaje
 

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
899
500
Nilikuwa nayasoma hayo malalamiko mpaka nikajiuliza huyu binadamu kabarikiwa au kabaguliwa kupewa ubongo wa nyuma tu. Kiburi kina mwisho wake.

Walioadhirika awe na chama au asiwe na chama wampeleke mahakani kama Sabaaya sio DC. Kila mtu na kesi tuone Kama atashinda nyumbani au atakuwa na pesa za kuendesha hayo makesi.
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
30,516
2,000
Hii ina mantiki kubwa. Ukatili ulio mwingi walifanyiwa wafuasi wa Chadema, ni vema CHADEMA ikaratibu ukusanyaji wa ushahidi dhidi ya Sabaya ili haki itendeke. Waandae waathirika waweze kutoa ushahidi wa kweli na si vinginevyo. Walindwe dhidi ya vitisho vya Sabaya na genge lake etc........
Naunga mkono hoja,huyu jambazi lazima ashughulikiwe kisheria.
 

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
1,049
2,000
Huwa wanalindana huo uchunguzi wenyewe unaweza usijue majibu yake.
Siyo rahisi kwake alikwenda mbali na tofauti Sana kwa baadhi ya mambo Mfano...nini kilimsukuma kuhusisha magari na kuyawekea namba za UN,kwenye uhalifu?!....ikithibitika ni Kweli!!?Na UN iliwalazimu watoke hadharani kukanusha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom