Wanasheria wa CHADEMA kesi hiyo msiilalie, ichangamkieni mpaka kesho

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,934
3,805
Ni wazi mchezo uliotumika kuwaingiza wabunge wateuliwa akiwemo mfungwa kwenye bunge la Tanzania hauwezi kufumbiwa macho, sasa uangaliwe utaratibu wa kufungua mashtaka dhidi ya mechi nzima utafutwe uharamu au uhalali wake.

Kama CHADEMA wanajiridhisha kuwa kuna sahihi zimefojiwa,kuna mtu amehudhurisha majina bila ya idhini ya Chama,hilo ni kosa kubwa sana la jinai ni sawa na hela ya Chdema kutolewa benki kwa kutumia nyaraka feki ikiwemo mihuri ya Chama.

Je inawezekana kufunguliwa mashitaka dhidi ya wahusika ? Au wapo juu ya sheria na hawawezi kufunguliwa mashtaka ?
Hata kama imani ya kusikilizwa ni ndogo lakini historia huandikwa na kumbukumbu kuweka kuna walioshirki vita na Adolph Hitler mpaka miaka ya karibuni iliyopita wamefikishwa mahakamani.

Chupuchupu marais na viongozi wa Tanzania wapandishwa mahakamani na utawala huu wa Magufuli ,hivyo huko tuendako si ajabu akatokea au ukatokea uongozi utaoweza kuwafikisha viongozi waliopita kizimbani na kujibu mambo kama haya yanayotokea leo.

Chadema funguweni kesi.
 
Ni sawa ili kuepuka ile kauli walioizoea masokwe kusema kwanini hamkuenda mahakamani,hii sio mnakwenda kushinda au kushinwa hayo ni matokeo ,kinachotakiwa ni rekodi ambazo huandikwa na historia.
Wakishahukumiwa na mahakama ya Jamii tosha
 
Covid 19 waungane na waunga juhudi waliotelekezwa na ccm waunde chama chao waombe ufadhili ccm
Hawa mpaka watoe kilicho nyuma ya pazia,nani aliwataarifu nani aliwatoa jela nani aliwajazia fomu,kama walitishwa wasifike kwenye kikao ni nani aliewaambia hilo na kwa nini na nani aliwaandikia zile barua ya aina moja kwa wote tofauti ni jina tu.Ni mengi sasa mahakamani ndiko kutakuwa na kaukweli flani.
 
Hahaha mahakama gani?! Wamejiondoa mahakama zote zenye kutenda haki wamebakiza za ccm, sasa uende kuishitaki ccm kwa ccm?!
hayo sio ya kwetu ni yao,huku tunafuata sheria sasa kama wao hawazifuati ni lao, Hakutazuka lawama hapo baadae kwamba hamkuenda mahakamani hata kama mahela amepeleka majina yeye anaweza kushitakiwa kwa kuwa chama hakikumkabidhi aliyatoa wapi ?
 
Hahaha utamshitaki wapi huyo Mahela?!
 
Ni wazi mchezo uliotumika kuwaingiza wabunge wateuliwa akiwemo mfungwa kwenye bunge la Tanzania hauwezi kufumbiwa macho, sasa uangaliwe utaratibu wa kufungua mashtaka dhidi ya mechi nzima utafutwe uharamu au uhalali wake.

Kama CHADEMA wanajiridhisha kuwa kuna sahihi zimefojiwa,kuna mtu amehudhurisha majina bila ya idhini ya Chama,hilo ni kosa kubwa sana la jinai ni sawa na hela ya Chdema kutolewa benki kwa kutumia nyaraka feki ikiwemo mihuri ya Chama.

Je inawezekana kufunguliwa mashitaka dhidi ya wahusika ? Au wapo juu ya sheria na hawawezi kufunguliwa mashtaka ?
Hata kama imani ya kusikilizwa ni ndogo lakini historia huandikwa na kumbukumbu kuweka kuna walioshirki vita na Adolph Hitler mpaka miaka ya karibuni iliyopita wamefikishwa mahakamani.

Chupuchupu marais na viongozi wa Tanzania wapandishwa mahakamani na utawala huu wa Magufuli ,hivyo huko tuendako si ajabu akatokea au ukatokea uongozi utaoweza kuwafikisha viongozi waliopita kizimbani na kujibu mambo kama haya yanayotokea leo.

Chadema funguweni kesi.
Ni kweli kabisa. Lazima kumbukumbu ziwekwe sawa 'for future reference if not action".
 
vyovyote itakavyokuwa kwamba hao wabunge watalindwa na speaker ndugai jumuiya ya kimtaifa inaona kila kitu ITAKUWA NI AIBU TU solution ambayo ipo ni serikali kuja kuongea na chadema na act mezani wakae kama watu wazima na kuheshimiana mambo mengine ni kuabishana tu
 
Pira ndio dk 45 za kwanza Halima team 1 vs kamati kuu 1!
mkuu umeingia shift ya asubuhi ,ebanaee sauti ya zege kawa kipenzi chenu aisee kila la heri kwa hiyo wakiwa wabunge wa ndugai/mahakama ile trillion 2 ya EU itakuja au ndo itaonekana kwamba hii nchi ina bonge la demokrasia?
 
Kwani mmesahau kua zitto leo hii mnampembejea nae alikua ni msaliti nimesimama upande wa haki!
mkuu umeingia shift ya asubuhi ,ebanaee sauti ya zege kawa kipenzi chenu aisee kila la heri kwa hiyo wakiwa wabunge wa ndugai/mahakama ile trillion 2 ya EU itakuja au ndo itaonekana kwamba hii nchi ina bonge la demokrasia?
 
hivi kipara JAMANI MMESHINDA UBUNGE ASILIMIA 99 WABUNGE VITI MAALUMU HUWA WANATOKANA NA IDADI YA WABUNGE WA CHAMA...CHADEMA INA MBUNGE MMOJA WA HUKO RUKWA TENA WALIOUKUWEPO AKIWEMO MDEE HADI JPM PALE KAWE ALITAKA KULIA AKISEMA NILEETEENI GWAJIIMA LEO MNAWATAKA WA NINI JAMENI? BUNGE LENU HATA NDU GAY ALISHATANGAZA KWAMBA THIS TIME HAKUNA KAMBI YA UPINZANI MBONA MNAHAHA CHADEMA

MLISHAIUA IACHENI MANATAKA TENA IWE NA WABUNGE 20 SPIKA ATUMIE UBABE WAKE SAMBAZENI HIVYO VITI KWA KINA TLP NA WENZAO
BY THE WAY HILO NENO HAKI USIRUDIE TENA KULITAMKA KUWA NA AIBU
 
Sijui kwa nini wanachama wa Chadema wanapenda kuchezewa akili na viongozi wao. Hata hawajiulizi kama kweli wana nia thabiti ya kutoshirikiana na serikali, walishindwaje kumdhibiti mbunge wao pekee wa kuchaguliwa asiapishwe kuwa Mbunge? Mchezo uleule unachezwa kwa hawa wateule 19. Uongozi unajua nini kimefanyika, unajaribu kudhibiti hasira za wanachama kwa kujifanya hawajui kilichotokea.
 
MUACHE ABAKI HUKO SI NDO PEKEE KACHAGULIWA AU? YEYE NO THE BEST NCHI NZIMA KAENI NAYE JAMENI MBONA MNAHAHA FANYENI KAZI SASA MAGUNZI YAMEONDOKA,DUH
 
Kama unaamini wamefukuzwa nakuonea huruma. Kinachofanywa ni "damage control" Mbowe anajua kufukuzwa kwao hakuna athari ya maamuzi ya hao 19 kuingia bungeni, ndio maana ametoa loophole ya siku 30 wateule kuandika barua za kukataa rufaa au kuomba msamaha. Maanaa yake bado ni wanachama wa Chadema.
 
Back
Top Bottom