Wanasheria tusaidieni "mpokea rushwa polisi wa Tanga kakamatwa je mtoa ile rushwa mbona hajakamatwa?

isidingo 1961

Senior Member
Nov 9, 2015
106
13
Ninawaomba wajuzi wa mambo ya Sheria ya Rushwa watujuzi Sheria ya Rushwa inasemaje kwa mntoa rushwa a mpokea rushwa.Kwa uelewa wangu mdogo nadhani iwapo mtoa rushwa hatatoa taarifa za kuombwa rushwa kwenye chombo husika basi akitoa rushwa atakuwa katenda kosa.

Mkoani Tanga kuna Polisi alikamatwa kwa kupokea rushwa na amefukuzwa kazi na anashikiliwa na PCCB. Lakini yule aliyetoa hiyo rushwa hajakamatwa je Sheria inasemaje kwa mtoa rushwa?
 
Atasema alifanya vile kama mtego na ndio maana alirekodi video hivyo kushinda kesi. Wewe unapotoa rushwa huwa unarekodi?
 
Kwa hy baada ya kazi nzuri aliyofanya bado unataka akamatwe? Au haukuwa mpango wa dereva kumkamatisha yule askari?
 
Jeri Muro alikua anakesi ya kutaka kutoa rushwa.
Jiulize aliyetaka kupokea alikamatwa?
 
Atasema alifanya vile kama mtego na ndio maana alirekodi video hivyo kushinda kesi. Wewe unapotoa rushwa huwa unarekodi?

Kwa hy baada ya kazi nzuri aliyofanya bado unataka akamatwe? Au haukuwa mpango wa dereva kumkamatisha yule askari?

Kisheria anatakiwa akamatwe, kesi iendeshwe na mahakama ndiyo ithibitishe kuwa hakutenda kosa kisheria....

Maana itabaidi ithibitishwe kama alipeleka kwenye mamlaka husika au aliirusha tu Whattsapp......na mengine ambayo mahakama inabidi kujiridhisha nayo kabla haija establish kwamba hana kosa kisheria
 
Hahaaaaa imekulaaa kwenuu wambien waache upuuzi so kilahelaa unapokeaa tu zingine makanjanjaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom