Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,017
2,000
Wakati unamshauri agombee hakuwa na hizo kesi unavosema. Kwani NEC na mahakama kwa mujibu wa sheria nani zaidi maana kuna kifungu kinasema NEC haiwezi kuhojiwa sasa kwanini iogope mahakama ambayo haiwezi kuihoji NEC inayo mamlaka yote ya kumpitisha kwakuwa yenyewe haiwajibiki kwa mahakama yoyote hapa Tanzania.
Hoja nyingine sheria imetamka wazi kabisa sababu zinazoweza kumfanya mgombea kutokuwa na Sifa na haijasema endapo atakuwa ameshitakiwa kwa kosa la jinai sasa hiyo sababu ambayo haipo kisheria itatumikaje kumuengua mgombea. Ni ukweli kabisa kuwa kama NEC itaamuwa kutofuata sheria ya uchaguzi na kumuengua Lisu ili kufurahisha mgombea wa CCM itakapotokea taharuki yoyote NEC ifahamu kuwa ndiyo itakuwa imesababisha The Hague itawahusu wahusika.
Ndugu, hapa duniani chini ya jua, kila kitu kinaweza kuhojiwa hata kama kimewekwa kwenye sheria kwamba hakiwezi kuhojiwa...
Kumbuka, kinachohojiwa si mshindi bali utaratibu mbovu uliopelekea ushindi...
NEC Wakimtangaza mshindi, kitakacho hojia si mshindi bali process nzima, hii ikifanyika, hata ushindi pia utakuw nullified.

utaratibu ukiwa mbovu, kwa mfano una au ume breach- principles of natural justice, right to fair hearing, equal treatment, transparency na mlolongo wote huo... basi uchaguzi mzima utakuwa batili...

kinacho natakiwa kufanywa na wadau ni kuifungulia kesi NEC na ku- prove kwamba ime breach fundamental freedoms, rights and responsibilities.. Hii ikifanyika maana yake ni kwamba NEC Hawatakuwa na uwezo kwa kuendelea na mchakoto wao wa uchaguzi kwa maana watakuwa hawana legitimacy ya kumtangaza mgombea kwa kwa kuwa process nzima ilikiuka rules of natural justice, breached fundamental rights na pia freedoms to free and fair election... Ubatili huo ukiwa proved, basi hata kile walicho kitangaza hakitakuwa na maana kisheria...

Angalizo:

NEC chondechonde: Watanzania tumeamuka toka usingizini, na nunajua ni nini kinachoendela....
tafadhalini saana ndugu zetu NEC, wapeni vyama vyote haki sawa, vinginevyo ni majibishano na vurugu mechi zisizo na maana na sintofahamu nyingi...

Judge Kaijage, najua unasoma humu: Wewe wajua kwamba United nation security council ni supreme kila kona duniani humu, lakini maamuzi yao huwa hupingwa na hata mahakama katika regional bodies... kumbuka kesi ya Kadi -- kadi case (1 and 2, academic summary yake inapatikana hapa:
kadi 1: Kadi v. Council and Commission - Case Brief for Law Students | Casebriefs
kadi 2: Kadi Case – Constitutional Core Values and International Law – Finding the Balance? )
Usiipeleke nchi katika sintofahamu kwa kuwa mtaalam wa kutafsifi sheria.. kazi hiyo ulisha istaafu na sasa uko pembeni bench; wale ulio waacha ndio wenye kazi hiyo...

Chonde chonde Kaijage...
 

soine

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
1,915
2,000
"Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais" (Pascal Mayalla, 2020).

Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka.

Askofu Bagonza alijibu vizuri sana hoja ya uanaharakati na uongozi. It is just a head and tail on a same coin!
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Mkuu sijasoma Uzi mzima,Ila Tanzania ingekuwa na vyombo huru na taasisi imara,sidhani Kama Magu angetakiwa hata kuchukua form maana ananuka jinai Kila sehemu ya mwili wake, ila kwa kuwa serikali ya Tanzania imeporwa kutoka kwa watanzania na kumilikishwa kwa ccm,acha Mpinzani yeyote wa hawa waroho na walevi wa madaraka ccm apewe hizo jinai zenu
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,592
2,000
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la hoja za kisheria, wanasheria wetu humu, tusaidieni, kufuatia Tundu Lissu kuwa ni mtuhumiwa wa jinai ambayo akikutwa na hatia kutamuondolea sifa za kugombea urais, hivyo jee kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea urais kwa kutumia kigezo cha uadilifu wa mke wa Kaisari?.

Uandilifu wa mke wa Kaisari ni ile kutuhumiwa tuu, inamtosha Kaisari kutoa talaka bila any proof, mke wa Kaisari should be spotless, kule kutuhumiwa tuu ni doa!. Mgombea wa urais should also be spotless, as while as snow!, as clear as sky!. Hatuhitaji mtu mwenye makandokando ya jinai nyuma yake!.

Miongoni mwa sifa za kugombea urais ni pamoja na kutokuwa mjinai uliyakutwa na hatia.

Kwa vile TL anakabiliwa na kesi kadha za jinai ambazo zikikamilika na akikutwa na hatia, zitamuondolea sifa ya kugombea urais, hivyo akigombea na kushinda urais, kesi zake zote za jinai zinafutika, hivyo NEC kumpitisha TL kugombea urais ni kuingilia uhuru wa mahakama, contempt of the court, hivyo kanuni ya uandilifu wa mke wa Kaisari, itatumika kumuengua TL kugombea urais!, ili mahakama iwe huru kuendelea na kesi zake za jinai za uchochezi?.

Kufuatia possibility ya TL kutopitishwa na NEC, then mgombea wa pamoja wa upinzani ni Benard Membe, Tundu Lissu ni Pacemaker tuu wa Membe, his candidacy itaishia NEC kwa kuwekewa pingamizi ambalo litakubaliwa!.

Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Hata pingamizi la yumkini ya kuyumkinika kuhusiana na kesi za jinai zinazomkabili, japo Tanzania tunafuata mfumo wa haki wa common laws of England, "innocent until proven guilty", japo TL ni innocent, lakini anakabiliwa na kesi ambazo akikutwa na hatia, zitampotezea sifa za kuwa rais wa JMT, kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu, mtuhumiwa wa jinai TL, akishinda urais, kesi zake zote za jinai zinapaswa kufutika, hivyo mtu akimjazia pingamizi based on this, pingamizi hilo linapita kwa urais kabisa!. Watanzania tunataka rais muadilifu, presidential material na sio rais mwanaharakati.

Angalizo hili ni muhimu sana kwa wana Chadema ambao wamehamasika sana na kupita kwa Tundu Lissu kuwa mgombea wa Chadema, hivyo angalizo hili litawasaidia washangilie kwa kiasi na kuweka akiba ya ushangiliaji wao, ili wasije wakapata psychological depression kutokana na too high expectations on TL, akienguliwa na NEC, kitakachofuata ni despair na psychological depression, ila kwa kila mwaka Chadema atakayelisoma bandiko hili, holi likitokea litakuwa na less impact, because they had some prior info. Wata despair tuu lakini hawatapata psychological depression.

Wanasheria wetu tusaidieni.

NB. Japo DPP hapaswi kuingiliwa na mamlaka yoyote, kama ni kweli Tanzania tunataka uchaguzi Mkuu ujao uwe huru na wa haki, na Tundu Lissu ndie mgombea pekee anayeweza kuleta challenge ya ukweli kwa mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, then nashauri DPP aitwe, aombwe kufuta kwa noble, kesi zote za jinai zinazomkabili Tundu Lissu ili Tundu Lissu awe spotless, kusitokee sababu zozote za NEC kumuengua.

Ikitokea Lissu ni kweli ameenguliwa na NEC ili kutoingilia uhuru wa mahakama, sisi waelewa wote tutaelewa, lakini its very unfortunately kwa wafuasi wake na mashabiki wake, hawataelewa!, watadhani Lissu anaonewa na hata kudhani kuwa serikali ya CCM inamuhofia sana Tundu Lissu, na kumuona ni tishio hivyo wameitumia NEC kumuengua!. Kelele zao zitakuwa sio za kitoto!.

Kwa track record ya kazi nzuri ya JPM kwa Watanzania, CCM itashinda kwa ushindi wa kishindo mapema asubuhi, hivyo tusiwape sababu za kutupigia makelele, serikali sikivu ya CCM, ihakikishe Lissu anagombea ili kuuthibitishia ulimwengu uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni uchaguzi huru na wa haki.

Background.
Kwa wasionijua, mimi ni Kaka yake na Tundu Lissu, nilimtangulia shuleni Ilboru, na ni mimi ndie mtu wa mwanzo kumshauri Lissu agombee urais
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Declaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla, kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, kwa good track record ya JPM aliyoyafanya kipindi cha kwanza awamu yake hii ya tano, yanajieleza wazi, hivyo JPM hana mpinzani wala mshindani, ni clear sweet victory.

Miongoni mwa sisi wana CCM wapya, tunapenda kuona sio CCM inashinda tuu, bali CCM inashinda kwa haki katika uchaguzi Mkuu ulio huru na wa haki ndio maana tumetoa ushauri huu kwa chama chetu.

Ushindi Mtamu ni Ushindani ktk Uwanja sawa, Sio Ule wa Mezani! Magufuli, Kasi yako ni Ushindi wa Kishindo CCM. Ruhusu Ushindani wa Haki, Sawa na Wazi!

Na ndio maana tunapenda sana kusitokee jambo lolote la kusababisha Lissu asigombee, ili kupunguza kelele mbele ya safari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Pascal sio kwamba umeileta hii hoja kwa bahati mbaya, ila umeileta kwa madhumuni kamili baada ya kuona kinachoendelea kwenye mizunguko ya Lisu. Na sehemu kubwa umeongozwa na wivu wa kisiasa, maana unajua fika Magufuli hana uwezo wa siasa za ushindani, na hatakaa aziweze. Hivyo hii post yako imekuja kuweka uamuzi ambao tayari Magufuli anao. Lakini kwa hiki kinachoendelea kwa muda huu mfupi, sio wewe, sio Magufuli sio wanaccm, wote mmejua kuwa watu wengi hawaipendi ccm, na hakuna uwezekano wowote wa wananchi wa nchi hii kukubali kurudi kwenye mfumo wa vyama vingi kwa ridhaa yao.
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Mbona kama umeshahukumu?
Wakuu,hivi yule aliye mtafutia mama yake mme,yule aliyemwambia DAs wa kisarawe akagombee wanaume na DC ofisini,yule aliyewauliza wananchi wa huko Kanda ya Kati wanataka kupanuliwa wapi,anacheo gani nchi hii,Mimi ni nimezaliwa Leo wakuu naombeni msaada
 

Mr.mzumbe

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
998
1,000
Wewe ni CCM. Kwa kuwa ni CCM tena yulw uliyefanya vibaya na wajumbe,basi hii hoja yako haina mashiko hata kidogo.

Chochote ulichoandika ni kujipendekeza kwa jiwe tu hasikusahau kwenye teuzi zako. Acha njaaa ndugu yangu.
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Aliwahi kusema anatishiwa vyombo vya usalama vikadharau kilichotokea tunakifahamu. Sasa wewe ni nani useme hatishiwi wakati kila siku akina Musiba wanasema hadharani kabisa na hawaulizwi chochote. Hii nchi bwana
Hivi hakuna wananchi wenye uwezo wa kujichukulia Sheria mkononi na kumpa msiba haki yake?yaani hata kumsingizingia mwizi tu kujustify kupigwa kiberiti watu imewashinda?
 

basiri

Senior Member
Aug 31, 2018
150
250
Background
Wewe ni kaka Ake TL
Wewe ndie ulimshauri agombee urais
Haaa haaa kwahyo ulimshauri ili aje kuenguliwa mbona hujamshauri aende akagombee ubunge?
Why hujamshauri atulie amalize kwanza kesi zake mahakamani?
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,228
2,000
Nina mawili kwako comrade. Not a legal perspective but simply logical:

1. Ushauri kwako binafsi for your own well being:
Huu uzi wako umedhamiria kuwachochea wapinzani na usijeshangaa kuwa unaweza kuwa qualified huko baadaye na ICC kama "instigation to trigger partsan-driven hate and violence". Kwa hiyo usione ajabu kwa wewe kujikuta u miongoni mwa watakaoburuzwa ICC when sh..t hits the fan!

2. Matumizi ya lugha yenye staha kwa presidential candidate:
Hapa chini nime-quote jinsi ulivyomshambulia Tundu Lissu kwa kauli zake ulizoziita hazifai kwa mtu anayewania urais. Lakini inaonekana umejisahaulisha kidogo kuhusu kauli zinazotolewa na JPM huku akiwa rais ambazo actually nyingi ni worse kuliko za Lissu ambaye hata siyo rais. So, ushauri huu au hili karipio lako ungelielekeza kwa mwenyekiti wa chama chetu CCM kwanza kabla hujaanza kuwashambulia kina Lissu. Ondoa boriti lililoko ndani ya jicho lako badala ya kung'ang'ania kuondoa kibanzi kilichomo ndani ya jicho la mwingine.

Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Ni hayo tu, comrade!
 

Areus

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
240
500
Pascal mayala Ni mwandishi wa habari na Ni mwanachama wa CCM. Sijajua miiko ya kazi yenu ipoje ya uandishi wa habari na kazi za siasa hasa kudeclare wewe Ni mwanachama wa chama Fulani.

TAALUMA zetu zisaidie kuijenga Tanzania yetu. Vyama sio Taifa
 

Kenge (Eng)

JF-Expert Member
Dec 7, 2006
543
250
Kutuhumiwa sio kosa na jinai ni pale tu unapotiwa hatiani.

Iweje sasa ulete mamneno mfu ya mke wa Kaisari?

Zama zile busara ya mfalme ilikuwa inatawala na hatupo tena huko, vingine kila mja akituhumiwa tu nje ya ulingo.

Every body will remain innocent till when will be found GUILTY and Convicted by the LAW (Court)..
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,824
2,000
Leo umedhalilika na ndio tatizo la nchi hii. Haki haitendwi wala kuonekana inatendwa.

Mahakama ndio chombo pekee cha kumtia mtu hatiania. Kabla ya hapo presumption ya innocence ndio kiongozi!! Kwa kuwa mpaka anachukua form na kabla ya kupitisha wagombea - mahakama ilikuwa haijamtia hatiani, hakuna jambo linaweza kufanywa kwa kufikirika tu.

Unataka aondolewe kuhombea halafu mahakama imuachie baadae na wakti huo akose kugombea kwa sababu uchaguzi umepita?? Ni vipi akaachiwa anagombea na hata akishinda atolewe kwa mujibu wa sheria??

Katiba imeainisha aina ya makosa yanayoweza kumnyima sifa mgombea. Nayo yanahusiana na uhaini na kodi. Au kama aliwahi kuadhibiwa kwa kifungo zaidi ya miezi 6. Katiba haitaji mtu spotless - usitengeneze sheria as you go along.

Kwa mawazo haya - hamtaki ushindani. Mnataka Rais aliyepita bila kupingwa???
 

muokotamatunda

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
953
1,000
ila dunia bwana!,yaani unapigwa ma risasi,mungu anakuokoa,unapona,unarudi nyumbani unazabwa mi KESI,jamani haya Mambo Yana warahisishia wananchi kujua na Kuona kwamba haki hamna na kukosa imani na serikali yao,Yani ukiwa na mtazamo tofauti ni NONGWA!
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,686
2,000
Sasa Paskali unaenda mbele na kurudi nyuma? Kwamba wewe ndio ulimshauri agombee urais halafu unakuja tena kuleta hoja za kuenguliwa kwake. Hujioni kama ni mnafiki fulani hivi mahiri ambaye unataka kuwa Mr. Nice upendwe na kila mtu?

Declaration yako kuwa "kwa sasa ni kada wa ccm", inalenga nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom