Uchaguzi 2020 Wanasheria, Tusaidieni. Je, kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea Urais kwa kutumia kigezo cha Uadilifu wa Mke wa Kaisari?

"Innocent until proven guilty", hii haijalishi aina ya kesi: hata kama ana ni kesi za jinai.
Hebu jiulize, vipi unapomuengua halafu mahakama ikamuona hana hatia katika kesi zote, Je, utarudia uchaguzi kumrudishia haki yake uliyompoka?
Serikali ya CCM imesheheni WAHUNI na WAHALIFU lukuki, kuanzia JPM hadi wasaidizi wake. Ma Dikteta ni WASHENZI na WENDAWAZIMU hasa wanaposhindwa kwa hoja, tutarajie viroja vingi sana mwaka huu.
 
Serikali ya CCM imesheheni WAHUNI na WAHALIFU lukuki, kuanzia JPM hadi wasaidizi wake. Ma Dikteta ni WASHENZI na WENDAWAZIMU hasa wanaposhindwa kwa hoja, tutarajie viroja vingi sana mwaka huu.
 
1. "Huwezi kuwa mwanaharakati na mgombea urais kwa wakati mmoja, lazima uchague moja"
2. Huwezi kuwa mchambuzi huru wa mambo ya siasa ilhali wewe ni kada mtiifu wa chama cha siasa, wewe umechagua siasa, baki huko!
3. Hata katika andishi lako unajiumauma tu, huna tena mtririko wa hoja. Para moja inapinga para iliyofuata!!
Uchambuzi wako umesha Rest in Peace!
Kikwetu mayalla ni njaa
 
Paskali hujambo? Hebu jaribu kutumia japo akili ya kawaida tu, mwenye jukumu la kudhibitisha JINAI ni chombo gani? Kwanini unaleta MAHABA yako kwa JPM na CCM kwa kuanza kuongolea mambo ambayo bado hayajathibitishwa kisheria na chombo husika? Hakika WAJUMBE wa huko kawe waliona mbali sana, kama ungebahatika kwenda Bungeni bila shaka ungesumbua sana kwa hoja za kipuuzi kama akina Kibajaji, Msukuma, Nkamia na wapuuzi wenzio wengine wenye mawazo na akili za namna hii. CCM must go.
Pascal ni mwanasheria kwa kisomo na alichokiandika si cha bahati mbaya, yuko na kundi lake la wanasheria wa CCM. Je, Lissu akienguliwa wafuasi wake wataufyata?
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali la hoja za kisheria, wanasheria wetu humu, tusaidieni, kufuatia Tundu Lissu kufutwa ubunge kwa kosa la kukiuka maadili ya uongozi wa umma, na kosa hilo ni a disqualification ya kutogombea urais, na ukijumlisha na Lissu kuwa ni mtuhumiwa wa jinai lukuki mahakama mbalimbali, ambayo akikutwa na hatia kutamuondolea sifa za kugombea urais, hivyo jee kuna uwezekano wa Tundu Lissu kuenguliwa na NEC kugombea urais kwa kutumia kigezo cha uadilifu wa mke wa Kaisari?.

Uandilifu wa mke wa Kaisari ni ile kutuhumiwa tuu, inamtosha Kaisari kutoa talaka bila any proof, mke wa Kaisari should be spotless, kule kutuhumiwa tuu ni doa!. Mgombea wa urais should also be spotless, as white as snow!, as clear as stlill water in the glass or sky!. Hatuhitaji mtu mwenye makandokando ya jinai nyuma yake!.

Miongoni mwa sifa za kugombea urais ni pamoja na kutokuwa mjinai kwa kosa la kukiuka maadili ya uongozi wa umma ambapo alikutwa na hatia na kufutwa ubunge, hivyo kupoteza sifa za kugombea urais?.

Ukiondoa hilo kosa la ukiukwaji maadili ya uongozi wa umma ambalo ni direct disqualification kugombea urais, na kwa vile TL anakabiliwa na kesi kadha za jinai ambazo zikikamilika na akikutwa na hatia, zitamuondolea sifa ya kugombea urais, hivyo akigombea na kushinda urais, kesi zake zote za jinai zinafutika, hivyo NEC kumpitisha TL kugombea urais ni kuingilia uhuru wa mahakama, contempt of the court, hivyo kanuni ya uandilifu wa mke wa Kaisari, itatumika kumuengua TL kugombea urais!, ili mahakama iwe huru kuendelea na kesi zake za jinai za uchochezi?.

Kufuatia possibility ya TL kutopitishwa na NEC, then mgombea wa pamoja wa upinzani ni Benard Membe, Tundu Lissu ni Pacemaker tuu wa Membe, his candidacy itaishia NEC kwa kuwekewa pingamizi ambalo litakubaliwa!.

Unapoamua kugombea urais, you have to choose in between kugombea urais au kuendelea kuwa mwanaharakati, you can't be both, mwanaharakati na mgombea urais. Ukichagua kuwa mgombea urais, uanaharakati unauweka pembeni, you speak, talk and behave like a president in waiting!, huwezi kusema hovyo, huwezi kutukana watu, huwezi kutoa tuhuma bila ushahidi, huwezi kuibagaza nchi yako kwenye media za mabeberu, halafu ukategemea utapitishwa tuu hivi hivi kugombea urais!.

Hata pingamizi la yumkini ya kuyumkinika kuhusiana na kesi za jinai zinazomkabili, japo Tanzania tunafuata mfumo wa haki wa common laws of England, "innocent until proven guilty", japo TL ni innocent, lakini anakabiliwa na kesi ambazo akikutwa na hatia, zitampotezea sifa za kuwa rais wa JMT, kwasababu kwa mujibu wa katiba yetu, mtuhumiwa wa jinai TL, akishinda urais, kesi zake zote za jinai zinapaswa kufutika, hivyo mtu akimjazia pingamizi based on this, pingamizi hilo linapita kwa urais kabisa!. Watanzania tunataka rais muadilifu, presidential material na sio rais mwanaharakati.

Angalizo hili ni muhimu sana kwa wana Chadema ambao wamehamasika sana na kupita kwa Tundu Lissu kuwa mgombea wa Chadema, hivyo angalizo hili litawasaidia washangilie kwa kiasi na kuweka akiba ya ushangiliaji wao, ili wasije wakapata psychological depression kutokana na too high expectations on TL, akienguliwa na NEC, kitakachofuata ni despair na psychological depression, ila kwa kila mwaka Chadema atakayelisoma bandiko hili, holi likitokea litakuwa na less impact, because they had some prior info. Wata despair tuu lakini hawatapata psychological depression.

Wanasheria wetu tusaidieni.

NB. Japo DPP hapaswi kuingiliwa na mamlaka yoyote, kama ni kweli Tanzania tunataka uchaguzi Mkuu ujao uwe huru na wa haki, na Tundu Lissu ndie mgombea pekee anayeweza kuleta challenge ya ukweli kwa mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, then nashauri DPP aitwe, aombwe kufuta kwa noble, kesi zote za jinai zinazomkabili Tundu Lissu ili Tundu Lissu awe spotless, kusitokee sababu zozote za NEC kumuengua.

Ikitokea Lissu ni kweli ameenguliwa na NEC ili kutoingilia uhuru wa mahakama, sisi waelewa wote tutaelewa, lakini its very unfortunately kwa wafuasi wake na mashabiki wake, hawataelewa!, watadhani Lissu anaonewa na hata kudhani kuwa serikali ya CCM inamuhofia sana Tundu Lissu, na kumuona ni tishio hivyo wameitumia NEC kumuengua!. Kelele zao zitakuwa sio za kitoto!.

Kwa track record ya kazi nzuri ya JPM kwa Watanzania, CCM itashinda kwa ushindi wa kishindo mapema asubuhi, hivyo tusiwape sababu za kutupigia makelele, serikali sikivu ya CCM, ihakikishe Lissu anagombea ili kuuthibitishia ulimwengu uchaguzi Mkuu wa Tanzania ni uchaguzi huru na wa haki.

Background.
Kwa wasionijua, mimi ni Kaka yake na Tundu Lissu, nilimtangulia shuleni Ilboru, na ni mimi ndie mtu wa mwanzo kumshauri Lissu agombee urais
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha uwezo zaidi ya Magufuli!

Declaration of Interest.
Mimi Pascal Mayalla, kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi, CCM, kwa good track record ya JPM aliyoyafanya kipindi cha kwanza awamu yake hii ya tano, yanajieleza wazi, hivyo JPM hana mpinzani wala mshindani, ni clear sweet victory.

Miongoni mwa sisi wana CCM wapya, tunapenda kuona sio CCM inashinda tuu, bali CCM inashinda kwa haki katika uchaguzi Mkuu ulio huru na wa haki ndio maana tumetoa ushauri huu kwa chama chetu.

Ushindi Mtamu ni Ushindani ktk Uwanja sawa, Sio Ule wa Mezani! Magufuli, Kasi yako ni Ushindi wa Kishindo CCM. Ruhusu Ushindani wa Haki, Sawa na Wazi!

Na ndio maana tunapenda sana kusitokee jambo lolote la kusababisha Lissu asigombee, ili kupunguza kelele mbele ya safari.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Sina uhakika ila nina hisi ni lazima kesi zote zi sikilizwe mahakamani na hukumu itolewe. Kwa sasa hivi hata kama ana kesi ambazo bado zina sikilizwa mahakamani, huyo ni mtu ambaye ana subiria hukumu. Vile vile mahamakama inaweza kutoa adhabu kwasababu ya kesi alizo nazo na kwa kawaida adhabu haimaanishi kwamba lazima atumikie kifungo. Mahakama inaweza ku muamrisha alipe faini na kesi inakuwa imeisha.

Nina kubaliana na wewe unapo sema kwamba mgombea wa urais ana takiwa awe "spotless" lakini siasa zetu hazija fikia hatua hio. Wenzetu walio endelea wana chukulia mambo kama hayo maanani sana na ndio maana kuwa na kesi mahakamani ina punguza kwa kiasi ki kubwa uwezekano wa mtu yeyote kushinda.

Tuli shuhudia uchaguzi ulio pita jinsi gani waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa alivyo weza kushiriki kwenye uchaguzi hata baada ya kuji uzulu kwenye uwaziri mkuu wake baada ya sakata la Richmond.

Nina kubaliana na wewe unaposema kwamba Tundu Lissu pamoja na wana CHADEMA wenzake wame kuwa waki fanya uana harakati mwingi lakini kuwa mpinzani nchini lazima kunaji husisha na kui kosoa serikali. Kwa vyovyote vile lazima uana harakati flani uwepo. Sema tu wana kosea sana jinsi wanavyo amua ku wasilisha hoja zao. Hata kama ame tukana watu au kui sema vibaya Tanzania kwenye vyombo vya habari vya nje, sidhani kama hilo ni jambo la NEC ku amua. Hilo ni jambo la wa Tanzania ku amua.

Vile vile tunaweza kuji funza kitu flani kwa ma shemeji zetu wa Kenya ambao wali mruhusu Uhuru Kenyatta kuwa rais kipindi alipokuwa na kesi ICC. Alipo kuwa ana gombea muhula wake wa pili bado kesi ilikuwa ina sikilizwa na bado alishinda uchaguzi.

Ili kupata mwanga zaidi kuhusu hili, ingekuwa vizuri kama unge orodhesha kinacho hitajika kwa mtu yeyote ku gombea urais kwa mujibu wa katiba.
 
Pascall siwez kukubishia katu, lolote laweza kutokea, kama huyu Lisu aliwai kueleza waziwazi kuwa anafuatiliwa na gari namba fulani na akasema kuna watu wametumwa ili wamdhuru wengi tuliipuza hiyo kauli kama kauli ya kisiasa na uongo ila baada ya siku Tundu Lisu akashambuliwa hadaharani na serikali ma watanzania tukashuhudia. Mbali na yote hayo serikali haikuishia hapo walaenda mbali wakamvua ubunge kwa sheria zao, leo hii NEC inaweza kuamua ikafanya hivyo na ikafanikiwa. Lakini hata kama Lisu atakuwa na makosa hakuna mtanzania ataamini ya kwamba kaenguliwa kisa kakosa sifa bali itaeleweka kuwa ni figisu za serikali ktk kuogopa ushindani. KAMA WATANZANIA WATATAKA HAKI, UCHAGUZI WA 2020 UNAWEZA UKALETA MAAFA HAPA TANZANIA. MUNGU ATUSAIDIE.
 
Back
Top Bottom