StingRay
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 503
- 628
Kumekuwa na ubabe mkubwa mkubwa sana unaofanywa na serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuhusu kulipa madeni ya mikopo ya 'tuition fees' na kufikia hata hatua ya kutu-brand majina ya "wadaiwa sugu" mara "defaulters" nakiwango cha kulipa kikiwa kikubwa sana. Mfano mtu alikuwa anadaiwa Tshs. 3,000,000/= nakufikia kudaiwa 7,000,000/=. Huyu mtu hakuwahi kukataa wala kugoma kulipa na taarifa zilikwishafika Bodi ili akatwe lakini ni uzembe wao wamekaa muda wote bila kukata halafu leo unamwadhibu mtu kwa kitu kisichokuwa na mkataba maalumu wa namna ya kukata mkopo. Inaumiza sana hii. Lakuni pia maagizo yanataka sheria ipitishwe ili makato yawe 15% badala ya 8% ilitokuwa ikitumika mpaka leo.
Naomba Sana wanasheria mtusaidie maana tunanyongwa na serikali yetu jamani.
Naomba Sana wanasheria mtusaidie maana tunanyongwa na serikali yetu jamani.