Wanasheria tusaidieni hili jambo la kuwekwa mahabusu na Polisi wetu wa Kitanzania

majutobeach

JF-Expert Member
Aug 10, 2016
212
250
Utakuta imetokea ajali ya gari na mwendesha pikipiki au chombo chochote cha Moto na katika ajali hiyo chukulia imesababishwa na marehemu kutokana na mchoro wa trafic lakini Mimi dereva ambaye sikuwa na kosa la kiuendeshaji nachukuliwa na kuwekwa mahabusu nakuambiwa kuwa nimeua.

Mfano mwendesha pikipiki kaingia kwenye lori Tena kwa nyuma lakini Mimi dereva wa lori nitachukuliwa nakuwekwa mahabusu na kusumbuliwa na hawa wezetu wenye mamlaka za kisheria na hutotoka mahabusu mpaka uwe umetoa kitu kidogo ndipo watakapo kutoa na kukueleza kuwa huna kosa mwenye kosa ni marehemu hii ni haki kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,873
2,000
majutobeach, Upelelezi umefanyika saa ngapi mpaka usema uhusiki na kifo hicho. Unawekwa ndani na utaachiwa kwa dhamana kwakuwa inawezekana upelelezi ukabaini wewe ndiyo chanzo. Sasa kama uliachiwa kienyeji watakupata vipi?

Mfano umembana bodaboda aliye kushoto yako unategemea itakuwa rahisi kutoa majibu rahisi kuwa nenda nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mohammed Khatibu

JF-Expert Member
Jun 28, 2018
596
1,000
Mkuu inatakiwa ujue kwamba kwa mazingira ya namna hiyo ni wazi kuwa polisi walikuweka mahabusu kwa ajili ya kulinda usalama wako.

Huenda raia wangekushambulia baada ya tukio Hilo la kifo.

Hata hivyo Bado unahaki ya kusaidiwa kupata njia za kuwasiliana na watu wako wa karibu au hata mwanasheria na pia polisi hawataruhusiwa kukuweka kizuizin zaidi yaasaa 48 ( 2 days)
 

Ruge

JF-Expert Member
Aug 15, 2019
2,425
2,000
majutobeach, Upelelezi umefanyika saa ngapi mpaka usema uhusiki na kifo hicho. Unawekwa ndani na utaachiwa kwa dhamana kwakuwa inawezekana upelelezi ukabaini wewe ndiyo chanzo. Sasa kama uliachiwa kienyeji watakupata vipi?

Mfano umembana bodaboda aliye kushoto yako unategemea itakuwa rahisi kutoa majibu rahisi kuwa nenda nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
boda boda anaruhusiwa kuifata gari akiwa upande wa kushoto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom