Wanasheria saidieni: Mashtaka mengi ni "Republic Versus Mshitakiwa" Je, ni Republic ipi hiyo?

Wacha weeeeh! Big up Mkuu.
Sasa Mkuu kama upo njema kwenye sheria unaonaje ile siku ya mwisho ukawa wakili wangu?:D:D:D:D:D:D:D:DMaana sidhani kama nitatendewa haki kwa kweli.
Sina mpango wa kuwa wakili yaani kwenda field tu court na kukikuta kibabu kinatamka mheshimiwa hakimu huwa "sijisikii poa" yaani sins stimu na mahakama.....
 
Sina mpango wa kuwa wakili yaani kwenda field tu court na kukikuta kibabu kinatamka mheshimiwa hakimu huwa "sijisikii poa" yaani sins stimu na mahakama.....
Hahahahaaaa........sawa Mkuu, ingawa nina mashaka kama ulielewa post yangu vema......Sababu kesi ya mwisho kila mtu atakuwa ni mshtakiwa.
 
Kuna mashtaka mengi ya kesi yamekuwa yakiandikwa kwa mtindo wa "Republic Versus Mshitakiwa", bila kutaja jina la hiyo Republic, kwa uelewa wangu, hata Kenya na China nazo ni Republic. Je, Mashtaka yanayoishia kusema Republic Vs Mshitakiwa bila kutaja ni Republic ipi, yana mashiko kisheria?
Generally makosa ya jinai mlalamikaji huwa ni serikali ambayo inatumia jina la Republic v.x hii ni kwasababu serikali inawajibu wa kuhakikisha inalinda usalama wa mali za wananchi na wananchi kwa ujumla hivyo inapotokea kuna kosa lolote la jinai serikali inasimama kma mlalamikaji na yule aliyefanyiwa kitendo anakuwa ni shahidi wa upande wa serikali
That is all from my knowledge concernig with law especially criminal law.
 
Kuna mashtaka mengi ya kesi yamekuwa yakiandikwa kwa mtindo wa "Republic Versus Mshitakiwa", bila kutaja jina la hiyo Republic, kwa uelewa wangu, hata Kenya na China nazo ni Republic. Je, Mashtaka yanayoishia kusema Republic Vs Mshitakiwa bila kutaja ni Republic ipi, yana mashiko kisheria?
Kuna kitu kinaitwa territorial jurisdiction, hii inaongelea uwezo wa mahakama kusikiliza kesi zilizo ndani ya mipaka yake.

Hvyo utakapokuta Republic v. Mshitakiwa hapa tanzania muda ambao case bado inaendelea hii moja kwa moja inamaanisha ni united republic of Tanzania.

Endapo umekuta imeandikwa Republic v. Mshitakiwa kwenye report yoyote kinachoangaliwa ni full citation ya kesi husika.
Kama law report ambapo case hiyo imekuwa reported niya Tanzania basi hiyo republic inamaanisha Tanzania.
Endapo law report hiyo niya sehemu nyingine bac itakuwa republic ya hiyo sehemu.

Nawasilisha.
 
Kuna mashtaka mengi ya kesi yamekuwa yakiandikwa kwa mtindo wa "Republic Versus Mshitakiwa", bila kutaja jina la hiyo Republic, kwa uelewa wangu, hata Kenya na China nazo ni Republic. Je, Mashtaka yanayoishia kusema Republic Vs Mshitakiwa bila kutaja ni Republic ipi, yana mashiko kisheria?

Nyaraka zozote za kesi husika huanza na jina la mahakama husika inayosikiliza kesi hiyo........MFANO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ( hapo tayari inaweleka ni jamhuri/republic ya TANZANIA na wala sio Kenya)

KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MASWA
MASWA

KESI YA JINAI NAMBA .......... YA 2017

JAMHURI
DHIDI YA

TAJIRI JASIRI

Kwa hiyo hata ndani ya TANZANIA inaweza tokea majina ya pande husika katika kesi yakafanana na zote zikawa katika mahakama moja kwa vyovyote vile namba za kesi hizo haziwezi fanana...........

Mashtaka hayo yana mashiko kabisa ...kwa nini Republic (Jamhuri)?.... makosa ya jinai yanachukuliwa kama kosa dhidi serikali na jamii nzima kwa ujumla ...mfano ..ukiua unakuwa umeikosea jamii nzima kwa ujumla ..ni jukumu la serikali kuhakikisha mfanya jinai anachukuliwa hatua shahiki kulingana na uzito wa kosa lake na sheria zilizopo.......Hivyo kwenye kesi zote za jinai serikali/republic/jamhuri huwa ni mlalamikaji... kesi husika haiwi ya aliyedhurika/mwathirika na jinai hiyo moja kwa moja kama yupo ... yeye huwa shahidi kama mashahidi wengine.....
 
Je, endapo ukashitakiwa na Mashtaka yakaandikwa kwa mtindo wa "Republic Vs Mshitakiwa" , pasipo kutaja jina la hiyo Republic, Kisha wewe Mshitakiwa ukaamua kulipinga shitaka kwenye Mahakama, Je unaweza kuwa na hoja ya msingi?

Nenda kwenye interpretatio of law act
 
Kikubwa cha kujiuliza ni kwamba upo nchi gani, umeshitakiwa nchi gani na kwa kuvunja sheria ya nchi gani na ni Mahakama ya nchi gani.

Huwezi kupelekwa Mahakamani bila kuambiwa sheria uliyovunja. Huwezi kushitskiwa Tanzania kwa kuvunja sheria ya Tanzania halafu ukahoji ni "Republic" ya wapi!

Mahakama za Tanzania haziwezi na hazijawahi kuendesha kesi kwa niaba ya Malawi, Kenya, China etc.. Mamlaka yake ni hapa Tz tu, na Republic husika ni Tz tu hakuna sarakasi zozote hapo...
 
unajua maana ya jurisdictions? na aina za jurisdictions? tuanze apo maana haiwezekani kesi ipo Tanzania alafu iwe jamuhuri ya China ni bangiiii izo
 
Republic ni jamuhuri ndo yenye mamlaka na jukumu la kulinda raia wake kwa mujibu wa katiba, kwa hiyo ukiua, ukiiba, ukibaka yan makosa yote ya jinai yenye mamlaka ya kushitaki ni Jamuhuri, na wewe uliyotendewa unakua shahidi namba 1, kwenye kesi za madai na aridhi wahusika mnabaki wale mnaodaiana na kesi za mirath unakuwa mwenyewe unayeomba Mirath au usimamizi wa mirath.kwa ufupi ndo hvyo usishangae sana zingine zinakua DPP
 
Ukiona kesi ya hivyo ujue ni pambano kati ya serikali na raia wake walioiweka serikali madarakani.

Wanatakiwa waandike Republic of Tanzania vs [Mchochezi] maana kesi inasikilizwa TZ.

Wakati huu wa Magufuli inabidi tuzoee kesi za namna hii maana Malaika wetu ni mkamilifu.
thats very fact broh na pia kesi za hvo ni kwa makosa ya jinai tu(criminal cases only)
 
Back
Top Bottom