Wanasheria saidieni: Mashtaka mengi ni "Republic Versus Mshitakiwa" Je, ni Republic ipi hiyo?

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Kuna mashtaka mengi ya kesi yamekuwa yakiandikwa kwa mtindo wa "Republic Versus Mshitakiwa", bila kutaja jina la hiyo Republic, kwa uelewa wangu, hata Kenya na China nazo ni Republic. Je, Mashtaka yanayoishia kusema Republic Vs Mshitakiwa bila kutaja ni Republic ipi, yana mashiko kisheria?
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,756
2,000
Si ni Tanzania?lakini ni kesi za high court na court of appeal chini ya hapa hua hatu share na upande wa zanzibar
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,890
2,000
Kuna mashtaka mengi ya kesi yamekuwa yakiandikwa kwa mtindo wa "Republic Versus Mshitakiwa", bila kutaja jina la hiyo Republic, kwa uelewa wangu, hata Kenya na China nazo ni Republic. Je, Mashtaka yanayoishia kusema Republic Vs Mshitakiwa bila kutaja ni Republic ipi, yana mashiko kisheria?
Soma historia ya chimbuko la serikali, sheria toka Uingereza
 
tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Si ni Tanzania?lakini ni kesi za high court na court of appeal chini ya hapa hua hatu share na upande wa zanzibar
Mkuu naona hata wewe umeuliza swali, nadhani huna uhakika pia na hiyo Republic. Nadhani Mahakama zibadilike sasa ziandike Mashtaka bila Ku acha maswali.
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,739
2,000
Ukiona kesi ya hivyo ujue ni pambano kati ya serikali na raia wake walioiweka serikali madarakani.

Wanatakiwa waandike Republic of Tanzania vs [Mchochezi] maana kesi inasikilizwa TZ.

Wakati huu wa Magufuli inabidi tuzoee kesi za namna hii maana Malaika wetu ni mkamilifu.
 
Je, endapo ukashitakiwa na Mashtaka yakaandikwa kwa mtindo wa "Republic Vs Mshitakiwa" , pasipo kutaja jina la hiyo Republic, Kisha wewe Mshitakiwa ukaamua kulipinga shitaka kwenye Mahakama, Je unaweza kuwa na hoja ya msingi?
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,156
2,000
Kosa la jinai ni kosa dhidi ya Jamhuri/Republic. Hivyo anayeshitaki ni yule uliemkosea, yaani Republic. Yule mhanga wa tukio (victim) kwa mfano aliyeibiwa au kujeruhiwa au kufa maslahi yake yanabebwa na Jamhuri. Lengo la jinai ni kutoa adhabu kwa mtenda kosa la jinai, hivyo si vema tukaacha jamii au watu waadhibiane wenyewe itakuwa vurugu na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Au wababe watawatenda wanyonge bila kuadhibiwa. Chukulia mfano scopion bila mfumo huu wa kijinai yule mwadhirika angeweza kumwadhibu.
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
8,945
2,000
Nafikiri la msingi inakuwa ni wapi au basi kwenye Ardhi ipi kesi husika inafanyika.

Kwaiyo kama inafanyika Tanzania, ikisemwa kwamba ni Republic vs Mshitakiwa automatically inakuwa ni kwamba kesi husika ni kati ya Republic of Tanzania vs Mshitakiwa.
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,156
2,000
Je, endapo ukashitakiwa na Mashtaka yakaandikwa kwa mtindo wa "Republic Vs Mshitakiwa" , pasipo kutaja jina la hiyo Republic, Kisha wewe Mshitakiwa ukaamua kulipinga shitaka kwenye Mahakama, Je unaweza kuwa na hoja ya msingi?
Mahakama za Tanzania hutumia sheria za nchini. Yaani ni kuwa mahakama ya nchi nyingine kwa ujumla haiwezi kutumia sheria za nchi zingine. Nimesema kwa ujumla kwa vile somo ni pana kwani kuna wakati maamuzi ya nchi hutumika nchi nyingine hutumika nchi nyingine. Hivyo hapa Tz ikiandikwa Republic moja kwa moja ni Tz
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,739
2,000
Je, endapo ukashitakiwa na Mashtaka yakaandikwa kwa mtindo wa "Republic Vs Mshitakiwa" , pasipo kutaja jina la hiyo Republic, Kisha wewe Mshitakiwa ukaamua kulipinga shitaka kwenye Mahakama, Je unaweza kuwa na hoja ya msingi?
Mimi siyo mtaalam wa sheria lakini kwa upeo mdogo nadhani mshtakiwa anatakiwa kumjua mshtaki wake.

Kama ni Republic, basi anatakiwa ajue ni republic ipi inayomshtaki kwa kuikosea.

Unapoandika Republic pekee ni sawa na kuandika JPM, kila mtu anaweza kuidadavua kivyake na kujipa nafasi ya kukana mashtaka.

Ukisema ni republic, mshtakiwa anatakiwa ahoji.....Republic inayomshtaki ni ya Uganda, Kenya, au ya Tanzania.
 
mimiks

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
1,028
2,000
Ukiona kesi ya hivyo ujue ni pambano kati ya serikali na raia wake walioiweka serikali madarakani.

Wanatakiwa waandike Republic of Tanzania vs [Mchochezi] maana kesi inasikilizwa TZ.

Wakati huu wa Magufuli inabidi tuzoee kesi za namna hii maana Malaika wetu ni mkamilifu.
Duuh hujui kesi Za jinai anaeshtaki ni Republic wee umekalia siasa tu ukiona Republic
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,739
2,000
Duuh hujui kesi Za jinai anaeshtaki ni Republic wee umekalia siasa tu ukiona Republic
Hakuna shida juu ya hilo, kitu ambacho wengi pamoja na mleta mada wanataka kukifahamu ni je Republic ipi?
Maana huwa wanaandika Republic vs [...........], je kuna republic moja tu?

Halafu kesi za hivi mabeberu wanatumia kivuli cha u-republic kufanya yao.
 
Jun 14, 2016
41
125
Kila case ina full citation huwa hawaishii FLANI V REPUBLIC, mbeleni kuna namba ya case , mahakama na zaidi lazima waandike Either In High court of Tanzania on zanzibar, juu ya Case husika ikiambatana na Corum ya majudge ...
 
CHARMILTON

JF-Expert Member
May 30, 2015
6,739
2,000
Jina la mlalamokaji huandikwa mbele ya "jalada" la faili la kesi
Nenda mahakamani utaona hivyo

Mfano
Juma kamuibia John..Hati ya mashtata inaandikwa R v Juma lakini kwenye jalada la kesi kutaandikwa jina la mlalamikaji/mhanga pamoja na la mshtakiwa
Pia kwenye hati ya mashtaka huandikwa majina yao,wajihi,kazi,wanakoishi n.k kwenye ukurasa mwingine

Nafikiri nimeeleweka
Nimekuelewa Mkuu,....Haya mambo siyafahamu kwa taaluma wala wa uzoefu, sijawahi kukumbana nayo kabisa.
Nashukuru kwa ufafanuzi.
 
sam shami

Member
Sep 22, 2016
70
125
Kuna mashtaka mengi ya kesi yamekuwa yakiandikwa kwa mtindo wa "Republic Versus Mshitakiwa", bila kutaja jina la hiyo Republic, kwa uelewa wangu, hata Kenya na China nazo ni Republic. Je, Mashtaka yanayoishia kusema Republic Vs Mshitakiwa bila kutaja ni Republic ipi, yana mashiko kisheria?
Ukiwa kwenye mahakama za ndani neno Republic is judiciary noted as Tanzania...ni kama useme magufuli ni raisi wa Tanzania hakuna mahakama itakuomba ushahidi kwa kuwa ni judicial noted
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom