illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Kuna wanasheria Nguli nchini wanajulikana kwa umahiri wao wa kupangua na kujenga hoja na wameshiriki katika kutetea wahalifu wengi wa kisiasa ambao kwa sheria hii waliitwa wachochezi, kwa makosa kama kutoa lugha za kashfa kwa mkuu wa nchi na mamlaka zingine, au zile kesi za madawa ya kulevya kuna wanasheria wengine walidiriki kabisa bila malipo yoyote kuhakikisha kwamba watuhumiwa wale wanakutwa bila hatia ama wanakutwa na kosa dogo ambalo adhabu yake inatekelezeka kiurahisi.
Kumekuwa na malalamiko mengi kwamba nchi hii kwa sasa inaendeshwa kwa kukiuka misingi ya sheria na suala hili limeibua "vichaa" wa kila aina kwenye mitandao wakijifanya wao ni wanaharakati eti wana taka kutetea na kukomboa wananchi wakati nchi hii ilishakombolewa na TANU na ASP wapumbavu na malofa in Mkapa's voice.
Nikiwa kama mwanasheria pori (bush lawyer) kuna swala ambalo naona wanasheria wetu wasomi wangejikita kwalo kuliko kusubiri watu wafanye jinai waje wawatetee, serikali yetu hii ina mihimili mikuu mitatu ambayo ni mahakama, bunge na serikali yenyewe, hii mihimili inatakiwa ijitegemee lakini kiuhalisia hicho kitu hakiwezekani mkuu wa muhimili wa mahakama ni jaji mkuu lakini kuna mtu anaitwa mwanasheria mkuu, kuna mkurugenzi wa makosa ya jinai kuna jaji kiongozi ili shuri lolote lifike mahakamani ni lazima lianzie kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai ambapo yeye ndiye huepeleka faili katika mahakama ili shauri liendelee, kwa lugha nyingine niseme ili muhimili wa mahakama ufanye kazi yake lazima itegemee muhimili wa serikali....hapa inakuwa ngumu kama shauri husika lina maslahi kwa serikali ndio utasikia faili limepotea nk, hitimisho muundo wa uongozi organization structure ya nchi haijawa wazi bali ya mtego mtego ambapo mtu mwenye kutaka mabadiliko ya nchi angeanzia hapa ambapo ndiyo mzizi wa yote tuyaonayo leo RIP DR MVUNGI