Wanasheria: Naomba kujuzwa tofauti kati ya Uhujumu uchumi na Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,072
18,258
Kwenu wasomi wansheria, sijui tofauti ya hizi kesi mbili.

Mfano mtu kafoji document ili apate mkopo bank, au auze property ambayo haipo , kwa lugha rahisi amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Je, huyu anaweza funguliwa kesi ya uhujumu uchumi?

Msaada wenu.
 
Aatafunguliwa kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, pia ana kesi ya kughushi hapo.

nb: Sijasomea sheria
 
Mkuu vipi tena mbona hivi jamaa wapo mbioni kukufikisha kisutu?
 
Kuna marekebisho ya Sheria ya kutakatisha pesa (Anti Money Laundering Act) Namba 26 ya mwaka 2019 ambayo imeongeza makosa ya rushwa, forgery kuwa ni kutakatisha fedha.

Kwa hiyo Kama imefanya forgery Ina maana umehujumu uchumi na ukapata fedha. Sasa hizo fedha ulizopata kwa njia haramu unazitumia kufanya kazi halali.
 
Mkuu nashukuru,

Hiyo sheria ni pana sana, niliwasikia ktk tv wazee wa vitengo wakifafanua, yaana hata mzee wako kijijini akipokea pesa kukarabati kibanda chache anapaswa kuhoji chanzo cha pesa, vinginevyo msala unampitia pia.
 
Nadhani tunahitaji wanasheria waje wafafanue
Hiyo sheria ni pana sana, niliwasikia ktk tv wazee wa vitengo wakifafanua, yaana hata mzee wako kijijini akipokea pesa kukarabati kibanda chache anapaswa kuhoji chanzo cha pesa, vinginevyo msala unampitia pia.
 
Hiyo sheria ni pana sana, niliwasikia ktk tv wazee wa vitengo wakifafanua, yaana hata mzee wako kijijini akipokea pesa kukarabati kibanda chache anapaswa kuhoji chanzo cha pesa, vinginevyo msala unampitia pia.
Kimsingi ssheria ya AML ya Tanzania na nchi zingine za Afrika ililenga kudhibiti fedha haramu kutoka kwa wauza mihadarati, usafirishaji wa binadamu, silaha na mafuta ya magendo ambao huwapa magaidi kama akina Alqaeda na Alshabaab.

Sheria hii Ni ya mwaka 2006 kufuatia mashambulizi ya Osama Bin Laden ya WTC pale New York mwaka 2001. Hivyo basi nchi zote wanachama wa UN walipewa kama TEMPLATE waichukue na wafanye CUSTOMIZATION kwenye nchi zao ili kudhibiti shughuli za UGAIDI.

Lakini nchi za Kiafrika hazikufanya homework ya kutosha kwa kuwa Sheria Ina hoji kila fedha ambayo mtu amepata tofauti na kipato chake kilichozoeleka.

Siku zote watunga Sheria au sera au kanuni huwa wanadhani wanawatungia WAKOSEFU Sheria za kuwabana, wanasahau kuwa nao iko siku watakuwa nje nao watakuja banwa na Sheria hizo hizo.

Kwa mfano kwenye Sheria hii kuna Lecturer mmoja wa UDSM (Dr Ringo Tenga) wa kitivo cha Sheria alihusika kuipitisha kwa kutoa maoni mwaka 2006 akiwa Mkuu wa kitivo na think tank wa Sheria nchini. Akaipitisha kuwa ni NZURI

Lakini mwaka 2017 alishikiliwa kwa Sheria hii hii ya AML ya mwaka 2006 kwa makosa ya kukwepa kodi kwenye kampuni ya mawasiliano ambayo yeye ni mwana hisa. Hapo sasa akiwa Rumande ya Keko ndipo akaanza KULALAMIKA kuwa Sheria haiko vizuri na inakiuka haki za kikatiba.

Huo ndiyo UJINGA wa waafrika
 
kwa hiyo bwn Tenga aliilalamikia sheria yake alisahau kuwa sheria msumeno
 
Exactly!! Hata Timothy Apiyo (RIP) aliyekuwa Chief Secretary wa State House enzi za J K Nyerere aliwahi kufanya makosa Kama hayo. Watendaji walileta mapendekezo ya mafao ya kustaafu. Lakini yeye akayapiga chini enzi hizo yuko ofsini na ni kijana. Hatimaye kwenye miaka ya mwishini mwa 2010 hivi kabla hajafariki aliwahi kuilalamikia Serikali kwenye ITV juu ya mafao madogo ambayo yanawafanya wastaafu waishi kwa shida na mateso. Alisahau kabisa kuwa yeye mwenyewe mwaka 1980s ndiye aliyekataa mapendekezo ya maboresho.
 
Kimsingi ssheria ya AML ya Tanzania na nchi zingine za Afrika ililenga kudhibiti fedha haramu kutoka kwa wauza mihadarati, usafirishaji wa binadamu, silaha na mafuta ya magendo ambao huwapa magaidi kama akina Alqaeda na Alshabaab.

Sheria hii Ni ya mwaka 2006 kufuatia mashambulizi ya Osama Bin Laden ya WTC pale New York mwaka 2001. Hivyo basi nchi zote wanachama wa UN walipewa kama TEMPLATE waichukue na wafanye CUSTOMIZATION kwenye nchi zao ili kudhibiti shughuli za UGAIDI.

Lakini nchi za Kiafrika hazikufanya homework ya kutosha kwa kuwa Sheria Ina hoji kila fedha ambayo mtu amepata tofauti na kipato chake kilichozoeleka.

Siku zote watunga Sheria au sera au kanuni huwa wanadhani wanawatungia WAKOSEFU Sheria za kuwabana, wanasahau kuwa nao iko siku watakuwa nje nao watakuja banwa na Sheria hizo hizo.

Kwa mfano kwenye Sheria hii kuna Lecturer mmoja wa UDSM (Dr Ringo Tenga) wa kitivo cha Sheria alihusika kuipitisha kwa kutoa maoni mwaka 2006 akiwa Mkuu wa kitivo na think tank wa Sheria nchini. Akaipitisha kuwa ni NZURI

Lakini mwaka 2017 alishikiliwa kwa Sheria hii hii ya AML ya mwaka 2006 kwa makosa ya kukwepa kodi kwenye kampuni ya mawasiliano ambayo yeye ni mwana hisa. Hapo sasa akiwa Rumande ya Keko ndipo akaanza KULALAMIKA kuwa Sheria haiko vizuri na inakiuka haki za kikatiba.

Huo ndiyo UJINGA wa waafrika
Sheria za AML zimekuwepo even before 9/11. But after 911, emphasis kwenye Terrorism financing ndo ilikuwa kubwa.

Back to the question
Uhujumu Uchumi vs Utakatishaji Fedha.

Uhujumu uchumi (Economic Offences) ni mujumisho ya makosa while kutakatisha fedha ni kosa.

Sheria ya Economic and Organized Crimes Act imeorodhesha makosa ambayo yakifanyika yanakuwa makosa ya kuhujumu uchumi, moja wapo ni utakatishaji fedha.
 
Kimsingi ssheria ya AML ya Tanzania na nchi zingine za Afrika ililenga kudhibiti fedha haramu kutoka kwa wauza mihadarati, usafirishaji wa binadamu, silaha na mafuta ya magendo ambao huwapa magaidi kama akina Alqaeda na Alshabaab.

Sheria hii Ni ya mwaka 2006 kufuatia mashambulizi ya Osama Bin Laden ya WTC pale New York mwaka 2001. Hivyo basi nchi zote wanachama wa UN walipewa kama TEMPLATE waichukue na wafanye CUSTOMIZATION kwenye nchi zao ili kudhibiti shughuli za UGAIDI.

Lakini nchi za Kiafrika hazikufanya homework ya kutosha kwa kuwa Sheria Ina hoji kila fedha ambayo mtu amepata tofauti na kipato chake kilichozoeleka.

Siku zote watunga Sheria au sera au kanuni huwa wanadhani wanawatungia WAKOSEFU Sheria za kuwabana, wanasahau kuwa nao iko siku watakuwa nje nao watakuja banwa na Sheria hizo hizo.

Kwa mfano kwenye Sheria hii kuna Lecturer mmoja wa UDSM (Dr Ringo Tenga) wa kitivo cha Sheria alihusika kuipitisha kwa kutoa maoni mwaka 2006 akiwa Mkuu wa kitivo na think tank wa Sheria nchini. Akaipitisha kuwa ni NZURI

Lakini mwaka 2017 alishikiliwa kwa Sheria hii hii ya AML ya mwaka 2006 kwa makosa ya kukwepa kodi kwenye kampuni ya mawasiliano ambayo yeye ni mwana hisa. Hapo sasa akiwa Rumande ya Keko ndipo akaanza KULALAMIKA kuwa Sheria haiko vizuri na inakiuka haki za kikatiba.

Huo ndiyo UJINGA wa waafrika
mfano wako umenikumbusha tukio moja

Kuna jamaa yangu alisimulia kwamba alifungwa miaka 6 akiwa ajamaliza kifungo yule hakimu nae alipatwa na kesi ya rushwa akafungwa pia.

wakiwa gerezani hakimu akawa anawakusanya na kuwauliza makosa yao na kuwafundisha namna ya kukata rufaa

jamaa akamueleza hakimu tukio lake hakimu akacheka sana na kumwambia mbona umeonewa wazi wazi

akamwambia hakimu ulikuwa ni wewe jamaa akaishia kuomba msamaha
 
Vyeo mwana malevya

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom