Wanasheria,na wote mliopata kufanyakazi Mahakani nielimisheni

kikokotoo kipya

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
441
488
Tafadhali ninaomba kuelimishwa nini kinatokea pale mshitakiwa anapoachiwa huru na mahakama,na kisha kukamatwa tena maswali yanayonisumbua ni haya:-

1)Je Mshitakiwa na Washitaki wanaelewa hukumu mapema kabla ya kusomwa,hadi upande wa mashtaka kuandaa wakamataji mara tu baada ya hukumu kutolewa?

2)Je wanasheria wanakasi kiasi cha kutosha kuandaa mashataka mapya kwa haraka,ili kuyasoma papo kwa papo?

3)Je kuna mawasiliano yasiyo rasmi au rasmi kati ya waendesha mashitaka wanaosimamia kesi mahakamani na mamlaka inayofuta kesi ,ambayo upelekea kuandaa ukamataji tena, na taratibu zingine za kisheria?

Nimeleta uzi huu ,baada ya hukumu ya kesi ya karibuni,ya akina Harry Kitilya ,Sioi Solomoni,na Shoshe Sinare,pamoja na baadhi ya hukumu za kesi kadhaa nilizopata kusikia hapa Tanzania.Hata wakati fulani watu wakifutiwa kesi hutimka mbio kutoka mahakamani,wakihofia kukamatwa tena.
 
Back
Top Bottom