Wanasheria na wanaojua sheria toeni ufafanuzi kuhusu kinga ya Rais

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,569
50,393
Katiba imetoa kinga ya rais kutoshitakiwa kwa makosa atakayofanya wakati akitekeleza majukumu yake.

Sasa nawaulizeni enyi wanasheria na mnaojua sheria.

(a) Ikitokea rais akatoa amri ya kuua watu wake, hashitakiwi?
(b) Kama jibu la swali (a) ni NDIYO, hamuoni kuna hatari kwamba rais anaweza kutoa amri watu wa mkoa fulani/kanda fulani/mrengo fulani wa kisiasa wauawe?

(c) Kama jibu la swali ( a) ni HAPANA, hili agizo la rais kuwataka polisi wakiuwa wapandishwe vyeo, haliwezi kuwa kosa la kumtia hatiani na kumuondoa madarakani?

Naomba majibu ya kina ikibidi nipewe hata nukuu za katiba na vifungu vya sheria.
 
Kwa kadri navyowapenda watoto na ndugu zangu, Polisi yeyote aende akaue hata mmoja tu, tena akachague yule dhaifu kabisa anayeisumbua na asiye na msaada katika familia yetu amuue huyo kwa risasi sababu kaambiwa na magufuri atapandishwa cheo.

aende akaue, huyo ntamfata kaburini kwa risasi pia.
 
R.I.P Akwilina et al.
Wakati wanasheria wasomi wanaperuzi maandiko,waje watudadavulie mada muhimu kisheria
 
Katiba imetoa kinga ya rais kutoshitakiwa kwa makosa atakayofanya wakati akitekeleza majukumu yake.

Sasa nawaulizeni enyi wanasheria na mnaojua sheria.

(a) Ikitokea rais akatoa amri ya kuua watu wake, hashitakiwi?
(b) Kama jibu la swali (a) ni NDIYO, hamuoni kuna hatari kwamba rais anaweza kutoa amri watu wa mkoa fulani/kanda fulani/mrengo fulani wa kisiasa wauawe?

(c) Kama jibu la swali ( a) ni HAPANA, hili agizo la rais kuwataka polisi wakiuwa wapandishwe vyeo, haliwezi kuwa kosa la kumtia hatiani na kumuondoa madarakani?

Naomba majibu ya kina ikibidi nipewe hata nukuu za katiba na vifungu vya sheria.
Hana kinga ya ICC, lkn ndani huwezi.......................... na ndiyo maana jiwe anafanya lolote alipendalo. Lakini kama anavunja katiba na sheria, akija mwingine naye atavunja katiba na sheria amshitaki....????? looks ridiculous anyway!
 
Kumbe tutarajie watanzania wengi kupoteza maisha
 
Back
Top Bottom