Wanasheria na Ufisadi na Mikataba mibovu, je bado tunawahitaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria na Ufisadi na Mikataba mibovu, je bado tunawahitaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by gollocko, Feb 8, 2012.

 1. gollocko

  gollocko JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 2,830
  Likes Received: 1,544
  Trophy Points: 280
  Leo katika gazeti la majira imeripotiwa kuwa serikali iliingia mkataba na kampuni ya utafutaji gesi ya Pan African Energy Tanzania Limited ili kutafuta gesi hapa nchini na katika mkataba huo CAG (Mkaguzi mkuu wa serikali) amegundua kuna kiasi kimeongezwa kimakosa kinachofikia dola za kimarekani mil.28.

  Huu ni mwendelezo wa mikataba mibovu ambayo hulalamikiwa kila kukicha hapa Tanzania na karibu kila wizara au idara za serikali kuna utitiri wa mikataba mibovu. Cha kushangaza tuna utitiri wa wanasheria na mikataba yote hii wanasheria huusika kwa asilimia kubwa!

  Sasa najiuliza baada ya ufisadi wote huu kwenye mikataba tunayoingia kila kukicha hapa nchini bado tunahitaji wanasheria kweli?
   
 2. H

  House1932-1951 Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado tunawahitaji kama wakifuata ile kitu inaitwa maadili ya kazi zao yaani Legal ethics and moral conduct mkuu.
   
 3. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tunawahitaji sana,

  kinachotokea wanashauri vizuri lkn mikataba inaenda kuchakachuliwa mbele ya safari

  ww jiulize nani anashuhudia mikataba hiyo, je ni yule aliyeshauri au mwingine
   
Loading...