Wanasheria tunaomba ufumbuzi wa utata wa kisa hiki.
Mama mmoja (mfanyakazi ya kuajiriwai) alifiwa na mumewe (hakumwachia watoto) ila aliachiwa kiwanja ambacho kilikuwa kimejengwa uzio wa ukuta tu bila jengo lolote ndani yake. Baada ya miaka miwili mama huyo aliolewa na bwana mwingine mfanya biashara, kwa ndoa ya kikristo. Mama huyo akiwa na huyo bwana mpya akajenga nyumba ( kwa hela yake) kwenye kiwanja alichoachiwa na marehemu mumewe kisha wakahamia kwenye nyumba hiyo yeye na mumewe mpya. Wamebahatika kuzaa watoto watatu na huyo bwana. Baada ya kuishi na huyo bwana kwa miaka miwili na kuona mumewe anayumba kibiashara akamshauri aende shule ( bwana alikuwa std VII), bwana akakubaliana na mkewe akaanza shule (secondari ya Miaka 2), akafaulu kiasi chake, akaenda kozi akamaliza na akajiriwa. Wakati huo wote mama ndiye alikuwa anagharamia shule ya mumewe mpaka kupata kazi. Wakati huohuo yule mama akiwa na huyo mumewe amejenga nyumba na kununua gari kwa mikopo ambayo anakatwa kwenye mshahara wake.
Baba kaanza mapepe na vurugu kwenye ndoa, mama kaamua kuomba kutengana ambapo itapelekea kupeana talaka. Je, mumewe ni nini chake katika ndoa hiyo baada ya kutengana?