Wanasheria, Mawakili Wasomi, Onesmo Ole Nguruma na Jebra Kambole, Wako Live. ETV, Waibomoa Sheria ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Habari.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,437
113,445
Wanabodi,
Wanasheria, mawakili Wasomi. Onesmo Ole Nguruma na Jebra Kambole, wako live ETV, Kipindi cha Hamza Kasongo, Waibomoa Sheria ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Habari ambazo Mahakama ya Afrika Mashariki, imetoa hukumu kuitaka serikali ya Tanzania kuzifanyia marekebisho sheria hizo.

Wale access na ETV karibuni mfuatilie.
Walifafanua kuhusu
Shauri Namba 2 la mwaka 2017 kati ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kituo cha Sheria na Haki na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania leo tarehe 28.03.2019 limeamuliwa na mahakama ya Afrika Mashariki ambapo waleta maombi wameishinda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapema mwaka 2017, waleta maombi walifungua shauri hilo mbele ya Mahakama ya Afrika Mashariki (The East African Court of Justice) kupinga Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 (Media Services Act, 2016) ambayo ilionekana kuminya uhuru wa habari kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja kuikuka Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sheria hiyo imelalamikiwa kwa kukiuka Kifungu cha 6(d), 7(2) na 8 (1) (c) cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwakuwa haiendani na misingi ya utawala bora, demokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, haki jamii, na utambuzi, ulinzi, na udumishaji wa haki za watu na binadamu.

Hivyo upande wa waleta maombi waliomba mahakama itamke kuwa; 1. Vifungu vya 7 (3) (a) (b) (c) (f) (g) (h) (i) na (j), 13, 14, 18, 19, 20, 21, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 50, 54, 52, 53, 58, na 59 vya Sheria ya Huduma za Habari, 2016 vifutwe kwa kuwa vinaminya uhuru wa habari.
2. Mahakama itamke kwamba Vifungu tajwa hapo juu vimekiuka mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

3. Mahakama itamke kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ifanyie marekebisho na/ama ifute kabisa Sheria ya Huduma za Habari, 2016

4. Gharama za kesi pamoja na gharama zingine zinazotokana na kuendesha shauri hilo mahakamani
5. Amri nyingine ambayo mahakama itaona inafaa.

UAMUZI

Baada ya mahakama kujiridhirisha na maelezo na vielelezo mbali mbali vilivyoletwa mahakamani hapo, imeamua yafuatayo*

1. Mahakama imekubaliana na waleta maombi kwamba vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari, 2016 vilivyolalamikiwa (kama vilivyotajwa hapo juu *kasoro kifungu cha 14 na 18*) na waleta maombi vinakiuka ki Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

2. Serikali ya Tanzania inaamriwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Sheria ya Huduma za Habari inaendana na Mkataba wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki.
3. Kila mtu abebe gharama zake.

Uamuzi huu unaweka misingi mizuri kwa mahakama zingine kuhusu uhuru wa habari na haki ya kupata na kutoa taarifa
P.
 
Wajina unamtindo wa kubadilika kama ki.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Wanasheria, mawakili Wasomi. Onesmo Ole Nguruma na Jebra Kambole, wako live ETV, Kipindi cha Hamza Kasongo, Waibomoa Sheria ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Habari ambazo Mahakama ya Afrika Mashariki, imetoa hukumu kuitaka serikali ya Tanzania kuzifanyia marekebisho sheria hizo.

Wale access na ETV karibuni mfuatilie.

P.

Niko hapa nawasikiliza hawa manguli wa sheria.
 
Tuko na Prof Ka - Bundi atasawazisha mambo huko nje. Kwanza amesoma na anaelewa sheria kuliko watu wote dunia hii. Tulimwamishia hapo kwa maksudi maalum. Tuliyajua yote haya na yale ya TL.
 
Wanabodi,
Wanasheria, mawakili Wasomi. Onesmo Ole Nguruma na Jebra Kambole, wako live ETV, Kipindi cha Hamza Kasongo, Waibomoa Sheria ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Habari ambazo Mahakama ya Afrika Mashariki, imetoa hukumu kuitaka serikali ya Tanzania kuzifanyia marekebisho sheria hizo.

Wale access na ETV karibuni mfuatilie.

P.
Nilijua mkubwa utatupa update sisi ambao hatujalipia vingamuzi
 
Back
Top Bottom