Wanasheria acheni ushabiki mtuambie ukweli: Kuzuia Maandamano ni Sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasheria acheni ushabiki mtuambie ukweli: Kuzuia Maandamano ni Sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 6, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanaJF,
  Naomba wanasheria mtuelimishe na naomba sana tena sana muache ushabiki katika jambo hili. Hivi chama cha siasa au wananchi wanapotaka kuandamana, wanaenda polisi kuomba kibali cha kuandamana au wanaomba ulinzi? Je, polisi wanapozuia maandamano kwa sababu yoyote ile ni haki kikatiba? Ninachotaka kuelewa hapa, ni je, polisi wanayo nguvu kisheria ya kuzuia maandamano kwa 'discretion' yao tu bila kulazimika kutoa maelezo ya kina kuhusu sababu ya kuzuia? Suala jingine ni je, raia wa kawaida anawezaje kuifurahia haki ya kujieleza ambayo ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu?
   
 2. Joyum

  Joyum Senior Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nimekuwa najiuliza haya maswali bila majibu. Tunaomba wenye kujua haya mambo watujuze wana JF wanasheria
   
Loading...