Wanasema "fanya unachokipenda" mimi nakwambia "Penda unachokifanya"

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Ukizunguka katika ulimwengu wa washauri, wasomi, waandishi wa vitabu mbalmbali na wakereketwa wa UJASILIAMALI wanatuambia "Fanya kazi unayoipenda".

Kitu wanachosahau ni ukweli kwamba, Unaweza kusubiri Hadi unaenda kaburini hujapata fursa ya KAZI UNAYOIPENDA. Hii inanikumbusha nilivyokuwa mtoto, nikiulizwa unataka kuwa nani maishani ninasema "Rubani" lkn hadi leo hiyo fursa na Wanapata watu watatu kati ya laki.

NINI KIFANYIKE?
Tafuta chochote cha kukuingizia kipato. Penda kazi unayoifanya, Tumia hiyo kazi kufanya Unavyovipenda.

Mfano,Ni mwalimu mpenzi wa kilimo ajiliwa, Pata mshahara, save, Tafuta shamba lima, Pata pesa.
Hapo hata kama unataka kusomea URUBANI utajilipia nauli mwenyewe na kujisomesha South Africa.

"Penda unachofanya" ndio "Ufanye Unachokipenda"

'' SPECIALIZATION IS FOR INSECTS ''
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom