Wanasayansi wagundua sayari nyengine 10 zenye uhai

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_96557759_isolatedworld-sm.jpg



Wataalam wa maswala ya angani wametangaza ugunduzi wa sayari nyengine kumi angani ambazo huenda zinaweza kusaidia uhai.

Wanasayansi wa shirika linaloshughulikia maswala ya angani NASA wanasema kuwa data mpya iliochunguzwa kutoka kwa darubini ya Kepler inaonyesha sayari kumi zenye miamba ambazo zipo hatua chache kutoka kwa mkusanyiko wa nyota.

Sayari hizo ambazo zinatoshana na dunia, zote zipo nje ya jua katika mkusanyiko huo wa nyota.

Darubini hiyo ya Kepler sasa imegundua jumla ya sayari 50 katika maeneo tofauti yenye uhai angani.

Chanzo: BBC Swahili
 
Tubaki kufuatilia makinikia na madini hayo Airspace tuyaache kwanza wakina Prof John Thornton na wenzake.
 
Tatizo umbali, mi nawashangaa sana wachawi hawataki kutoa ushirikiano kwenye safari nje ya dunia!! Teknolojia yao pengine ingefaa maana kama mtu anatoka Lindi na anakwenda kuwanga Mwanza na kurudi kwake Lindi usiku huo huo, wangetufaa sana.
 
Back
Top Bottom