Wanasayansi Wagundua Kondomu ya Majimaji Kwaajili ya Wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasayansi Wagundua Kondomu ya Majimaji Kwaajili ya Wanawake

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kimbweka, Aug 17, 2009.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Timu ya wanasayansi nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza kimiminika kitakachokuwa kikiwekwa kwenye uke wa mwanamke ili kuzuia ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.Wanasayansi katika chuo kikuu cha Utah nchini Marekani wamefanikiwa kutengeneza kimiminika kitakachokuwa kikitumika kama kondomu kwaajili ya kuzuia ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.

  Kondomu hiyo ya kimiminika ina uwezo wa kunasa vijidudu vyote vyenye ukubwa kuanzia nanomita 50 na kuendelea. Hii inamaanisha kuwa mbali na kuzuia virusi vya ukimwi, pia zina uwezo wa kuzuia vijidudu vidogo sana vinavyosababisha ugonjwa wa papilloma.

  Kondomu hiyo ya kimiminika kama mafuta jinsi inavyotumika ni hivi: mwanamke atachukua kimiminika hicho na kukiweka kwenye uke wake.

  Kimiminika hicho kinapokutana na majimaji ya uke ambayo huwa na kiwango fulani cha tindikali, kimiminika hicho hubakia katika hali yake ya kawaida kama kimiminika lakini mbegu za kiume zinapoingia hubadilisha kiwango cha tindikali kilichokuwepo na kukifanya kimiminika hicho kibadilike umbile lake na kuwa kitu kigumu ambacho huzizunguka mbegu za kiume.

  Baada ya tendo la kujamiiana kuisha na kiwango cha tindikali kwenye maji maji ya uke kurudia kwenye kiwango chake cha asili, mabaki ya kimiminika hicho hutoka.

  Kwa mujibu wa wanasayansi hao, kimiminika hicho kitasaidia kuzuia mimba na magonjwa mengine ya kuambukiza ya zinaa.

  "Tumetengeneza kondomu hizi za kimiminika ili kuwawezesha wanawake kujilinda na HIV bila kuwaomba wanaume zao wavae kondomu" alisema Patrick Kaiser, kiongozi wa timu ya wanasayansi iliyogundua kimiminika hicho.

  "Kondomu ya kimiminika" bado ipo kwenye majaribio kwenye chuo kikuu hicho na itachukua miaka kama mitatu kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu.

  Wanasanyasi hao kwa sasa wanajaribu kuweka madawa ya kuzuia ukimwi kwenye kimiminika hicho ili kuongeza ufanisi wake.

  Lengo la mradi wa kondomu hizo za kimiminika ni kuwawezesha wanawake katika nchi masikini za dunia ya tatu kuweza kupata kitu cha kujilinda na magonjwa ya zinaa kwa bei nafuu.
   
 2. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tumekwisha!
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hawa nao badala ya kutumia huwezo wao kufanya kampeni watu wasiziniane ovyo wao ndo kwanza wanawapa matumaini... Sasa hii inamaanisha kuwa hizi condom zilizopo sasa hazifai kitu... kazi kweli kweli!
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Sasa miaafrika ndio itakuwa hata kazi haifanyi itakuwa ni uroda kwa kwenda mbele.
   
 5. B

  Bob Nash Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hamna kitu, wazungu wameona waafrica population inazidi kukua, inataka kuwapunguza kidogo
   
 6. Mr Q

  Mr Q JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2015
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 6,056
  Likes Received: 7,078
  Trophy Points: 280
  hivi hii project iliendeleaje?

  cc Deception
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Gide MK

  Gide MK JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2015
  Joined: Oct 21, 2013
  Messages: 4,718
  Likes Received: 3,388
  Trophy Points: 280
  Dry ndiyo mpango mzima
   
Loading...