Wanasayansi wagundua jiwe lenye ‘utajiri wa kutisha’ angani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,693
149,916
WANASAYANSI wa Kituo cha Anga cha Marekani (NASA), wamegundua jiwe kubwa lenye utajiri wa kutisha wa madini ya aina mbalimbali linaloelea angani.

Thamani ya utajiri wa madini yaliyopo katika jiwe hilo, unaelezwa kuwa ni zaidi ya uchumi wa dunia nzima.

Kutokana na ugunduzi huo, NASA wanapanga kuruka maelfu ya kilomita angani mwaka 2023 kwenda kwenye jiwe hilo ambalo kama litafanikiwa kurudishwa duniani, linaweza kuleta utajiri wa kufuru.

Likiwa katikati ya Sayari ya Mars na Jupiter, jiwe hilo linaaminika ni kiini cha ndani cha moja ya sayari zilizokufa.

Kwa mujibu wa wanasayansi, jiwe hilo ni la kipekee na limeundwa kwa madini ya metali kwa asilimia 100.

Jiwe hilo lenye umbo la duara lina urefu wa kilomita 200 na lina madini kama chuma, nickel na wanasayansi wanasema upo uwezekano mkubwa wa kuwa na madini adimu duniani kama dhahabu, platinamu na cobalt.

Jiwe hilo ambalo ni sayari mfu, lina thamani ya fedha nyingi mno, chuma peke yake kilichopo katika jiwe hilo, kinaweza kuwa na thamani ya Dola za Marekani 10,000 quadrillion, hii ni kwa mujibu wa mchunguzi mkuu wa jiwe hilo, Profesa Lindy Elkins-Tanton.

Uchumi wa dunia kwa jumla hivi sasa una thamani ya dola za Marekani 73 trilioni.

“Kwa sasa, kwenda kwa NASA katika anga za juu kunaleta dhana halisi ya ugunduzi. Safari hiyo, itawezesha kufika katika sehemu yenye kitu ambacho hakijawahi kuonekana wala kujulikana. Itatoa nafasi kwa wanasayansi kuona kitu ambacho kilikuwa kinafikirika hadi kufikia hivi sasa.

“Bado hatujaweza kufahamu mambo mengi, lakini tunadhani jiwe hili ni kiini cha metali ya sayari ndogo iliyoharibiwa kutokana na nishati kubwa, mwendo kasi wa dunia,” anaeleza Elkins-Tanton

Mpango huo wa kufika katika anga lililopo jiwe hilo, unatarajiwa kuzinduliwa mwaka 2023 na hadi kufikia mwaka 2030 chombo cha anga za juu kitakuwa kimefika eneo lililopo.

Wanasayansi ambao wametumia muda mwingi kulichunguza jiwe hili wanasema ndiyo jiwe kubwa la metali kwenye mfumo wa jua lililopo umbali wa kilomita 300 na inaaminika kuwa na kiasi kikubwa chuma na nickel.

Jiwe hilo kwa mara ya kwanza aliliona mwanaanga wa Kitaliano Annibale de Gasparis mwaka 1852 na kupewa jina la mungu wa roho wa Kigiriki Cupid.

Mwanzoni, ilidhaniwa kuwa ni jiwe la barafu lakini miaka ya 1980 wanaanga walishangazwa kuona rada ikisoma kuwa jiwe hilo lilikuwa linaundwa na metali.

Wanasansi wanaamini kuwa, jiwe hilo limepoteza ganda lake la nje, kutokana na msuguano na msukumano ambao umefanyika kwa mamilioni ya miaka.

Ili kupata ukweli zaidi kuhusiana na ugunduzi ambao bado unaacha maswali mengi, NASA itapeleka chombo chake katika eneo lililopo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kisayansi ambao unatarajiwa kuchukua muda mrefu.

Hii ni nafasi ya ugunduzi wa aina mpya ya dunia ambayo haijawahi kuonekana, si mwamba wala jiwe la barafu bali ni metali tupu,” anasema Elkins-Tanton ambaye ni Profesa katika chuo Kikuu ha Arizona nchini Marekani.

Anaongeza: "Jiwe hili ni aina pekee ya umbo ambalo limeweza kugundulika kwenye mfumo wa jua, ni njia pekee ya binadamu kuona shehemu ya kiini cha sayari iliyokufa. Mara nyingi tumekuwa tukijifunza sehemu ya ndani au kiini kwa kutembelea na kutizama sehemu za juu.

Chombo kitakachokwenda katika anga lililopo jiwe hilo, kitachukua miaka saba kufika. Pia kitakaa kwenye jiwe hilo kwa miezi sita kikijaribu kurekodi vitu mbalimbali kama muonekano, usumaku na vitu vilivyomo ndani yake.

Mpango huo ni sehemu ya mpango wa ugunduzi wa NASA utakaogharimu dola za Marekani milioni 450 wenye lengo la kujifunza kuhusu mfumo wa jua miaka milioni 10 tangu kuzaliwa kwa jua.

Mpango wa pili utazinduliwa mwaka 2021 ambao utalenga kuchunguza mabaki ya maombo ambayo yapo jirani na sayari ya Jupiter.

Chanzo:Mtanzania
 
Mkuu heshima kwako.
Nianze kwanza kutoa heshima zangu kwa Gazeti la mtanzania ila hilo la kusema uchumi wa dunia ni usd trln 73 wameteleza. ....uchumi wa dunia kwa sasa ni usd trln 276 (America yenyewe inatake 67%) na ukweli ni kwamba finance inabeba trln 194 na goods and services inabeba zilizobaki.
Hoja ya madini kama nickel na cobalt na mengine. ..kuna gharama zake. Bado dunia haijaishiwa hayo madini. ....atahari za ki mazingira na gharama za kufanya hivyo ni kubwa mno.

Sidhani kama kuna la kushangilia hapo...ila kweli Mungu mkubwa na ya Mungu ni mengi sana.
 
Wakati sisi ufipa tuko bize kusafisha mafisadi,
Wenzetu wanasafisha vyombo vyao kwenda anga za mbali
 
Naona juzi mlimsafisha aliyekwepue Raslimali za UDA Mkapa.na shares za UDART sababu ni wa kwenu.Ati ni wakunyumba.Hongera.Msije mkatuambia mnapiga vita Rushwa wala ufisadi
 
Solar system/Mfumo wa Jua. Wow!
Tafsiri safi.
 
Duuuhh kuna gape sana hapa duniani.Wakati sisi tunawaza kubadili mitaala ya elimu huku walimu ni walewale na uwezo wao ni uleule wao wanawaza kuuchukua utajiri angani.Mungu ibariki dunia, AMEN
We kazi yako ni kulaumu tu . Ukishajua Umechelewa kaza Buti Run.
 
Mkuu heshima kwako.
Nianze kwanza kutoa heshima zangu kwa Gazeti la mtanzania ila hilo la kusema uchumi wa dunia ni usd trln 73 wameteleza. ....uchumi wa dunia kwa sasa ni usd trln 276 (America yenyewe inatake 67%) na ukweli ni kwamba finance inabeba trln 194 na goods and services inabeba zilizobaki.
Hoja ya madini kama nickel na cobalt na mengine. ..kuna gharama zake. Bado dunia haijaishiwa hayo madini. ....atahari za ki mazingira na gharama za kufanya hivyo ni kubwa mno.

Sidhani kama kuna la kushangilia hapo...ila kweli Mungu mkubwa na ya Mungu ni mengi sana.
$73 trillions nadhani ni kwa jiwe moja.....labda kuna mawe 200 mkuu na each ni 73trl....
 
Back
Top Bottom