Wanasayansi wagundua dawa inayorefusha maisha

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Dawa inayotumika kwa matibabu ya kawaida huenda ikategua kitendawili cha kurefusha maisha na kuzuia uzee.

Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya, ambao ulibainisha kwamba viwango vya chini vya dawa aina ya Lithium vilisaidia kurefusha maisha ya nzi waliowekwa kwenye maabara.

Wanasayansi wamesema utafiti huu unatoa matumaini ya kutoa dawa kuwasaidia watu kuishi maisha marefu na yenye afya.

Lithium inatumika katika matibabu ya matatizo ya akili, kama mfadhaiko, na kusongwa na mawazo.
maisha.jpg

Hata hivyo ina madhara makubwa ikiwa itatumika kwa viwango vya juu.

Haijulikani jinsi Lithium inavyotibu matatizo ya akili, lakini alipopewa nzi, dawa hiyo ilisaidia kurefusha maisha yao.

Hata hivyo watafiti wamesisitiza lazima dawa hii kutumiwa kwa viwango vya chini zaidi, kwani viwango vya juu vinaweza kuleta maafa.

Dkt Ivana Bjedov mmoja wa watafiti kutoka taasisi ya matibabu ya saratani amesema dawa hii itasaidia afya kwa wazee sawa na kuzuia magonjwa kama vile ugonjwa wa kutetemeka 'Parkinson'.

Kando na matatizo ya akili Lithium imetumika kutibu maumivu makali ya kichwa 'Migraines' na ugonjwa wa jongo unaomfanya mtu kuvimba viungo hasa wakati wa baridi.


Chanzo:
BBC
 
Kurefusha maisha ya nn tena wakati tumeambiwa mwisho wa mwaka sayari ingine inaangukia dunia aaaghh!!!!
 
utafiti ufanywe katika inzi uhusishwe na binadamu hao wawapi ndio hao walisema dunia itagongana na sayari ingine nini mwezi uliopita?
 
Kifo ni lazima, utale usitake waache kujishibisha upepo, ubatili mtupu
 
These are scientists who do not have the concept of morality. Even if they have discovered such a medicine, the question must be Is it Right for them to do that?
What kind of the world will it be if people are not dying, what about population explosion in the world?
This is just a shameful and immoral scientific research whoever funded it,owes an apology to the world and humanity.
Let nature takes its own course on this issue. I cannot think if it is a desirable world where people are not dying.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom