Wanasayansi wa Kijerumani wamegundua roboti wa kusaidia mbegu za kiume kuingia kwenye yai la kike

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,718
Maisha kila kukicha kwa nchi za ughaibuni ni kutaka kufanya zaidi ya mawazo ili kisicho wezekana kiwezekane.

Huku ujerumani jopo la wataalamu wamegundua kijiroboti ambacho kitawa saidia wale wanaume wasio weza kutungisha mimba kitaalamu “low sperm motility”

Majaribio haya yamejaribiwa kwa wanaume watano na kuzaa matunda katika utungishaji.

IMG_2408.jpg

Spermbot ni nini?

Imeundwa kwa kutumia sumaku nyepesi na mfano wa coil ndogo ya chuma (imeundwa madini ya na titani na nikeli),ili kufata mkia wa mbegu na kuzunguka mkia huo, hapo ita lazimisha kupeleka mbegu kwa kujizungusha kama drili ya kuchimbia ili kufika kwenye yai na kuingia kwa haraka kwenye utungaji.

Maisha na sayansi
 
Uchawi tu..😂 Hivi zile mbegu mbona huwa hazionekani watavesha vipi huo mkia hicho kiroboti chao?! Waachie natural ijiendeshe wasiilazimishe.
 
Hicho kiroboti kikisha ifikisha mbegu kwenye yai kinaiachia iendelee na mitikasi zake au kinakua sehem ya yai kinayeyuka?

Hiyo mbegu inaunganishwaje na hako ka boat? Yaani mbegu zinatolewa ndio zifanyiwe huo usmat au mwanaume anawekewa zitoke na mbegu?

Kwani hawawezi kutumia kitu kama bomba la sindano tu isukume kwa nguvu?
 
Labda hako karobot kana hole ambayo ww una shusha mzigo ndani yake alafu yenyewe inaenda kushusha panapohusika.
 
Hicho kiroboti kikisha ifikisha mbegu kwenye yai kinaiachia iendelee na mitikasi zake au kinakua sehem ya yai kinayeyuka?

Hiyo mbegu inaunganishwaje na hako ka boat? Yaani mbegu zinatolewa ndio zifanyiwe huo usmat au mwanaume anawekewa zitoke na mbegu?

Kwani hawawezi kutumia kitu kama bomba la sindano tu isukume kwa nguvu?
Utumie sindajj ya binadamu unatoa kale kenye ncha kali,
 
Uchawi tu..😂 Hivi zile mbegu mbona huwa hazionekani watavesha vipi huo mkia hicho kiroboti chao..?! Waachie natural ijiendeshe wasiilazimishe.
Nimejikuta nakucheka as if ninkuona na ninakujua. Mbona mbegu moja kutoka manii ya ng'ombe huweza kuhifadhiwa na baadae kuingiza kwa jike🤓, sasa tumesonga mbele zaidi. Kitoto kinatiwa kwenye mrija, time ikifika, kanapachikwa kwa jike na kukuzalia katoto. embryo transfer😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰

Bado tu unamaswali
 
Nimejikuta nakucheka as if ninkuona na ninakujua. Mbona mbegu moja kutoka manii ya ng'ombe huweza kuhifadhiwa na baadae kuingiza kwa jike🤓⁉️, sasa tumesonga mbele zaidi............kitoto kinatiwa kwenye mrija, time ikifika, kanapachikwa kwa jike na kukuzalia katoto...embryo transfer😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰😰

Bado tu unamaswali
Hujui kufikiri bado pole sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom