Wanasaikolojia ktk majanga: Baada ya ajali ya Moto Morogoro hawakuhusishwa!

shamimuodd

JF-Expert Member
Jan 28, 2019
890
1,398
Great Thinkers,

Assalamu Alaikum wadau.

Inasikitisha, kila ninapoona video au picha au kusikia wale watu waliokuwa karibu na tukio, unahisi kabisa kuna watu tukio la Morogoro linawasumbua sana kisaikolojia. Katika pitapita zangu sijaona watalaamu wa saikolojia wakihusishwa (mfano kuwatembelea majeruhi ili kuwapa msaada wa kisaikolojia namna ya kufikiri).


Naomba tujadili je kuna umuhimu wa wanasaikolojia ktk majanga kama hili la moto la Morogoro?
 
Eti hayo majukumu wameachiwa madaktari na manesi.

Ila hii nchi ni ya ajabu sana, Wanasaikolojia wanapewa nafasi ndogo sana. Kuna watu wamesomea Psychology na Guidance and Counseling lakini ni taasisi chache sana, za serikali au za binafsi, zinazotambua uwepo wao na kuthamini kazi zao. Taasisi nyingi wala hazioni umuhimu wao.Inasikitisha kwakweli.
 
Hao wataalamu watazunguka Nchi nzima? Makanisa na Misikiti inatosha, acheni dhambi, ikitokea ajali badala ya kuokoa mnaiba wakati dereva mkanda haufunguki. Kahama Shinyanga malori (Tanker) mbili zimeanguka mbona mafuta hawakuiba?
Km ni wanasaikolojia waanze ma madereva wa Tanker wamalize matatizo ya majumbani, nyumba ndogo na tamaa kuna kitu, haiwezekani lorry liungue wakati dereva hayupo, au limwage mafuta kuna kitu waanzie hapo
 
Janga lishatokea... mambo yote yatapita tuu... na hali itakua shwari...

Yalitokea ya MV Bukoba yamepita... Yakatokea ya Nungwi yamepita... Yakatokea ya tetemeko la ardhi limepita...


Cc: mahondaw
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom