Wanariadha wetu walioenda kwenye mashindano Kampala - Uganda

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Majuzi Mwenyekiti wa Riadha Kitaifa Ndugu Mtaka aliwaaga wanariadha wetu waliokwenda Uganda kwenye mashindanoya riadha na kutuahidi kuwa safari hii medali ni lazima na wamepelekwa wanariadha wengi kwa idadi sawa na Uganda, Kenya, Ethiopia n.k.

Leo hii mida ya mchana nilikuwa naangalia mashindano hayo kupitia luninga ya Uganda yaani (UBC) katika mashindano yaliyokwishafanyika sikuwaona wanariadha wetu katika mashindano hayo au macho yangu yalikuwa mabovu?

Katika mashindano yaliyokwishafanyika Tanzania tumeambulia patupu. Sababu kubwa nadhani ni maandalizi.

Tusikate tamaa, tujitahidi kwa mashindano yaliyobaki angalau turudi hata na medaliya fedha.
 
Back
Top Bottom