Wanapenda Kuambiwa: Pole Mkuu, Wana wivu, Tuko Pamoja... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanapenda Kuambiwa: Pole Mkuu, Wana wivu, Tuko Pamoja...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, May 8, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mimi ni Mpenzi wa Social networks, na huwa natumia sana Facebook, Tweeter na Jamiiforums.

  Mimi ni friends na wanasiasa wengi sana hasa Vijana. Ni Rafiki za Zitto, Ni Rafiki wa Mnnyika, Regia Mtema, Nape Nnauye, Silaa na wanaharakti wengi sana.

  Nimeona katika Wall ya Nape amepost kitu kuilamu JF kwa Kejeli zilizopo dhidi yake. Nape ameandika hivi

  Nape Anasema hivi
  Baada ya kupost kwenye wall yake wachangiaji Mbali Mbali wamejikeza wengine Kumpa Pole, wengine Kumtia Moyo na wachache wameendeleza kile Nape anachofikiri ni Kejeli.

  Moja kati ya Post za kumpa Pole na Kumtia Moyo bwana Nape ni Hizi Hapa

  Lakini Vile Vile kuna watu waliokuwa na Mitizamo tofauti

  Lakini Kilichonisukuma Kuanzisha Hii Thread ni Utetezi wa Huyu Mkulu hapa

  Huyu yeye hataki Criticism za watu watumia Majina ya bandia, Kwake yeye Chochote kitachosemwa na Mtu ambaye anatumia pen name basi ni Feki.

  Mimi Ningependa kumshauri huyu Mheshimiwa kwamba Criticism za kweli huwezi kuzipata kwa watu unaowafahamu kama kwenye FB. Nimejaribu kuangalia wale wote waliokuwa wanatetea wameishia tu kutoa ambayo Ndiyo Bwana Nape na Mwenzake Silaa wangependa kuona yanaandikwa hapa JF. Maneno kama

  Komaa Mzee,
  Wana Wivu,
  Tuko Pamoja
  Wanakukatisha Tamaa

  Kwenye FB wengi wanatoa Comment za Kinafiki ili Msigombane na Vile vile hakun uhuru wa kuoa Maoni ndio maana watu wanaishia Kutoa Pole tu na kutiana Moyo

  Hakuna Watu wanaotukanwa na Kukejeliwa hapa Jamvini kama Zitto, Slaa, Mnnyika lakini sijawahi kuwaona watu hawa wakienda kutafuta Sympathy kwa Rafiki zao FB. Mimi nawashauri hawa kwamba Being a politician unayependa sana Media ni Lazima ukubali kulipa Gharama za Matamko yako yote yawe pint yawe Pumba


  Mnapendwa Kusifiwa, Mnapendwa kuzungukwa na Vyombo vya Habari, Hampendi kukosolewa, Kwenu Ninyi Mnawapenda wale wanaowaambia Pole Kinafiki na kuwachukia wale wote wanaotofautiana nanyi.
   
 2. D

  DENYO JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo la nchi hii ni unafiki ndugu yangu -unafiki unatupeleka shimoni kwa kasi, mtu anaiba unamsifia, wewe ni mtaalam wa uchumi unashindwa kumwambia rais hali ni mbaya, wewe ni rais wa nchi unashindwa kuona hali halisi ya watu wako unafiki mkubwa, tuna wataalam wengi lakini tatizo unafiki hakuna anaweza kumwambia kikwete na serikali yake hapa sio chukia hii, au huyu uliyemteua hapa sio mtaalamu chukaua huyu, kazi yao siku zote ni kusifia kusifia kutoa pole na ujinga kibao.

  Kwa hiyo sishangai kuona waliochangia kwenye wall post ya nape na kusema unafiki kiukweli hakuna anachokifanya nape chenye tija kwa mtanzania, ataweza vipi kuwaong'oa mapacha watatu waliomweka alitemteua yeye madarakani??????? Kama sio unafiki ni nini???????

  Mimi ninaamini CHADEMA wengi sio wanafiki ni kwa sababu ya falsafa ya CHADEMA na sera ambayo wanaiishi. Walk the talk-nape anaweza walk tha talk???? Wakati wanasema wanajivua gamaba ata the same time wanachakachua mswada wa katiba, harafu mtu anawapa pole huo ni unafiki --watanzania tujifunze kuwa wajasiri na kusema ukweli tuache kuwa wanafiki, baba wa taifa atakumbukwa mpaka na kizazi kijacho kwa sababu hakuwa mnafiki-kuna watu aliwaambie enzi za uhai wake hawawezi kuwa viongozi wa nchi kwa sababu aliona hawafai lakini baada ya yeye kupumzika unafiki ukachua nafasi.
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Viongozi wengi huwa hawapendwi Kukosolewa na Mbaya Zaidi Tabia yao hiyo ya Kutopenda kukosolewa Iko Wazi Sana Mbele ya Wanaowaongoza ( Yaani wanapenda kuonesha kwamba Hawapendi Criticism). Matokeo yake ni Kwamba wale wote waliochini huwa wanaogopa Kukosoa waliojuu kwa Sababu wanajua kwamba Walio Juu hawapendi kukosolowa. Wataishia Kuwasifia na Kukubaliana na Yote wanayoyataka hata kama wanaamini Viongozi wao wanakosea

  Mkuu Nape anashindwa kuelewa Kwamba kuna watu wanampaka Mafuta Kwa Mgongo wa Chupa kwenye FB kwa Kutumia Majina yao Halisi halafu Wakija Huku JF wanamchamba kwa Kutumia Pen Name ( Well because they know kwamba Bwa Mkubwa Hapendi Kukosolewa yeye kukosolowa ni Kukejeliwa)

  Kuna Kitu Kinaitwa JOHARI WINDOW Nadhani Leaders like Nape na Silaa inabidi warudi Shule wakakisome Vizuri kitawasaidia sana hasa katika Kujua WEAKNESS Zako. Kama Unasubiri Mkeo Akwambie Punguza Mdomo basi wewe endelea Kusubiri
   
 4. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna uwezekano kabisa kwamba hao waliompa moyo huko FB wamekuwa wakimponda hapa JF kwa majina bandia.
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Thats Exactly
   
 6. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  nimefunga fb account kwa ajili ya unafki, no criticism, kila siku maneno ni yale yale

  upo juu
  umependeza

  what so stupid!!!

  ukitaka real life njoo jf,nafurahi kuona kumbe wanaiogopa jf(im glad to be one of the members)
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ngoja tuangalie ataishia wapi? yu wapi makamba..
   
 8. k

  kakini Senior Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dhumuni la Facebook ni kuongeza giza Africa mimi nipo south africa na huo ndo ukweli uwezi kukuta mtu mwenye dhamana ya kuongoza wananchi yupo facebook which means they dont have meaning rather than gossip....

  GO on Nape wewe baki Facebook ndo inayokufaa maana ni ya kimbea kule huwezi kukuta vitu vya maana kama JF so keep on attaching yourself to that FB this JF is not good for your health and for your well being also nenda mkaimbiane mipasho na yule dogo mwenye domo kama beleshi February
   
 9. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  nakubaliana nawe kabisa
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nilisema kwamba hawa jamaa wanapenda Kusifiwa tuuuuu, ukiwaponda Wanakasirika na Wanatamani hata Kukunywesha sumu. Mkuu Nape Nashukururu sana KINIDELETE kwenye facebook nadhani Huo ndio uamuzi wa karibu ulioweza kuufanya nadhani kama Ungekuwa Karibu yangu Ungeweza hata nichoma Kisu lakini sitaacha kukuambia Ukweli pale unapopotoka. Kama Ulitegemea all friends watakua wanakuimbia Haleluya umekosea sana Mkuu
   
 11. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  jamani achane waendelee kumsifu ili azidi kuharibu kama hajajifunza ya igunga hatajifunza tena .naona akikutana na wale mapacha watatu hasa chenge ana kwa ana huwa anatamani kujiharishia.
   
Loading...