Wanaowapa wanafunzi mimba wafanyweje?

kahigwa

Member
Nov 14, 2011
33
14
#YALIYOJIRI Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Jackson Msome ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kumsaka na kumtia mbaroni kisha kumfikisha mahakamani mtu aliyempa mimba mwanafunzi wa kidato cha 4 katika shule ya sekondari Karabagaine. Msome alitoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo na kupewa taarifa kuwa mwanafunzi huyo ni mjamzito.

Nini maoni yako kuhusu hili?
 
Hivi baba mtoto akifungwa miaka 30 nani atalea mimba na mtoto? Serekali Ina saidia chochote kwenye makuzi ya mtoto?
 
Sheria zipo ila hazifanyi kazi,sina uhakika kama kuna wafungwa waliotuhumiwa kuwapa mimba wanafunzi
 
Sipingani na swala la kumpa mwanafunzi mimba ni kosa kisheria kwa sababu kuna mambo mengi unamuharibia.

Tatizo pia lipo kwa hao wanafunzi wenyewe... wanafunzi wa siku hizi hawana aibu wala soni kupapatikia wanaume... wengine wanadiriki hata kujiweka kama siyo wanafunzi na kuanzisha mahusiano ya kimapenzi... akija pata mimba ndiyo utakuja sikia alikuwa mwanafunzi...

Hao wanafunzi wengine wanatafuta kabisa number za wanaume wakalale nao... wengine wanajitambia kwa wenzao idadi ya wanaume waliokuwa nao... Dunia ya sasa siyo salama tena..
 
Hivi kwa nini swala la mimba ndio linapigiwa kelele, badala ya kuelekeza nguvu nyingi kuwaelimisha watoto madhara ya ngono katika umri mdogo? Anaweza zuia mimba na kupata magonjwa ya zinaa, hapa mtoto anakuwa salama? Na hawa wanaume waelimishwe madhara ya kufnya ngon na watoto wadogo ni kuleta hasara kwao na kwa taifa kumfunga baba wa mtoto na kumfukuza shule binti ni kuendelea kunyanyasa mtoto alie zaliwa kwa kuwa na mama aliekosa elimu na kukosa malezi ya baba ambae amefungwa. Sioni kama kufunga ni kumsaidia binti na kiumbe kilicho tumboni.
 
WAKAMATWE,WAPIMWE UBIKIRA,SIO TU MIMBA. Kufanya tu mapenzi(hata kuingiza nusu kichwa tu) ,adhabu yake miaka si chini ya 10
 
Back
Top Bottom