Wanaounga mkono mgomo wa Madaktari na wanaopinga madaktari kuboreshewa maslahi, hawako sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaounga mkono mgomo wa Madaktari na wanaopinga madaktari kuboreshewa maslahi, hawako sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Judgement, Jan 31, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Sikubaliani hata kidogo na wale wanaopinga ama kubeza uboreshwaji, wa maslahi ya madaktari.
  Na wakati huohuo sikubaliani mara 1000 na madaktari na vibaraka wao wawaungao mkono kwa namna wanavyouendesha mgomo huu.
  Just immagine mke/mama wa daktari augue na ihitajike probably any intensive care e.g
  Operation
  sugery formalities
  Unadhani daktari muhusika na mgonjwa huyo atamuacha afe eti kwa ajili ya mgomo ?
  Kwa macho yangu nimeshuhudia Bugando mama mja mzito akifia mapokezi baada ya kupokewa na kutelekezwa hapo kwa masaa 8, kwa kua madaktari hawapo !.
  Siku hiyohiyo tr 27.01.12 nikashuhudia watoto wawili mmoja akiwa na umri wa makisio km miaka 7 huyu alikua ameumwa na Mbwa na wa pili kisio la km miaka 10 aliegongwa gari na ameharibika karibu nusu ya kichwa.
  Hawa wote hawakupata matibabu, na yule mama mjamzito alikufa na mimba yake.
  Hivi tutumie akili ya shule ya vidudu, hawa watoto wawili, na yule alielazimishwa afie tumboni wao wanajua nini Sakata la Pinda na madaktari ?
  Wao maslahi yao nini ?
  Au hawahitaji ?
  Kuna maslahi gani yenye umuhimu juu ya ardhi zaidi ya kuishi ? (maisha)
  maslahi ya madaktari ni fedha , makaratasi yanayotengenezwa na B.O.T pale ujerumani.
  Maisha ya viumbe hawa yakanunuliwe wapi ?
  Hawa ni wauaji.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Pole judgement kwa uliyoyashuhudia, jee unashauri nini kifanyike kuhusu hawa madaktari "wauaji?.
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ushauri wangu ni kuwa HAKUNA HAKI PASIPO WAJIBU.
  Serikali ifanye haraka kuwaboreshea hawa wataalamu maslahi stahili yao vile inavyopasa.
  Na wakati huohuo Madaktari wawe kazini ndiyo WAJIBU WAO.
  Hivi sasa wanadai MASLAHI na wako nje ya WAJIBU ! Hawatekelezi WAJIBU na huku wanadai ! Serikali ikija kuboresha maslahi yao waTanzania 10,000 wamekufa ! Nini mustaqbali wa MASLAHI ya hao watakaokua wamekufa ?
  Tuta'create mayatima wangapi ? Watakaokosa care ya wazazi wao kama kuwasomesha na mahitaji yao mengine ya lazima ?
  Na wazazi wao wamefia ktk "asante mgomo" ?
   
 4. R

  RIZIKI JUMATATU Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole ndugu yangu kwa uliyoyashuhudia ni kweli hao watoto hawana hatia.
  Mimi naamini hilo ni kosa la serekali kwani ilisema itawaleta wanajeshi waje kuziba nafasi za madaktari waliogoma?
  Naomba nimshauri Mh. Pinda swala la mgomo sio sawa na la uokoaji au kujenga madaraja ambalo linahitaji mtaalamu mmoja na wengine wote ni nguvu kazi tu(wanaotumia nguvu nyingi kuliko akili) madaktari ni watu wenye ufahamu mkubwa wanatambua huko uliposema napo kuna shida ya madaktari kuliko hata huku uraiani hivyo naomba aangalie mahali pa kuweka siasa na mahali ambapo hapafai.Jamani viongozi wetu kaeni chini na hao watu kwani tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida nyie njia ya India kupitia kodi zetu mnaijua ila sisi hatuijui.
  Kwa madaktari kwao wapo vitani ni mapambano na katika mapambano yoyote watu hufa.Sasa ni jukumu la serekali kuendelea kututoa wananchi wake kafara au........?
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Nawapa pole wafiwa, walale pema peponi marehem.
  nikushauri kwa kukuuliza swali kidogo, hivi anayepaswa kuwapatia huduma bora za afya wananchi ni nani, ukijibu ni madactari you are wrong kwa sababu madactari hawajiajiri serikalini, ubora wao kitaaluma uko carefully monitored na serikali, Ukijibu SERIKALI utapata vema, na suluhu ya mgogoro huu inaanzia serikalini, kumbuka wananchi tunahitaji 'huduma bora' sio 'bora huduma' na kama walifuzu "siyo kuhitimu" masomo yao (waserikali) watakuwa wanajua, anachoweza kulazimishwa punda ni kubeba mzigo tu!! halazimishwi kunywa maji asilani. mkuu pole kwa kushuhudia uliyotueleza, huo ni ushahidi dhidi ya pinda, blandina na wenzao.
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mh. Jogi hakika uliyoyaanisha hapa yote ni sahihi.
  Hata hivyo hembu tafakari haya ntakayokwambia hapa chini.
  Binadamu tumekuzwa kuanzia utoto wetu kwamba siku zote tuwe WAKWELI na UONGO ni dhambi iwe ni kwenye itikadi ya dini zetu ama malezi ya waliotulea kauli mbiyu hii tumekuzwa nayo.
  Pamoja na hayo leo sisi nasi tumekua (tunaitwa watu wazima)
  Kuna wakati unakutana na shauri, au tatizo ambalo linatakiwa ulisemee ukweli.
  Ambavyo kuna baadhi ya issues ukizisemea ukweli side effects zake ni kubwa kulikoni na ungezinyamazia au kuzisemea uongo.
  Mfano umemuona mke wa mtu ameingizwa guest ukaenda kumwambia mumewe, result yake mwenye mke akaja na bastola akaua mke, mgoni wake, muhudumu wa guest akiwa anakwenda kuamua timbwiri nae anakutana na risasi ya shingo !
  Angalia ukweli huu na faida zake.
  Narudi kwako wewe kusema ukweli madaktari hawatendewi haki stahili (ni kweli hawatendewi namie naamini hivyo)
  Matokeo madaktari wamesikia kauli ya ukweli wako wamebeba bunduki (kwa maana ya kugoma) sasa wanaua !
  Busara iko wapi ?
   
 7. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,053
  Likes Received: 2,932
  Trophy Points: 280
  Mtazamo wangu: Nakataa katakata kuwa madaktari wanauwezo wa kurejesha uhai. kazi hiyo ni ya Mungu peke yake. Wazungu pamoja na mahospitali mazuri na malipo lukuki mwisho wa siku ni maji ya ziwa. wanaonja mauti.Duniani according to me binadamu wote wana umuhimu sawa kutegemea hali ya mazingira.
  Angalia hapa. Mzazi ambaye hana malaria mzima lakini kijana wake kafukuzwa shule asifanye mtihani atamuona mwalimu kwa wakati huo ni muhimu sana.
  Mama anayetafuta housegirl wa kumuangalizia mtoto ili aende kibaruani hatamuona daktari kuwa ni muhimu zaidi ya kabinti ka miaka 14 katakako mkubalia kazi ya uyaya kamlelee mwanaye kusudi aende kibaruani.
  tajiri mwenye magari anamthamini sana Mmasai anyemlindia magari yake yasiibiwe kwa usiku huo wala hana mpango na daktari.
  Mzibua mitaro hasa ya vinyesi ataonekana bora zaidi utakapozidiwa na maji machafu ya chooni yatakayo zagaa katika makazi yako.SO KILA MTU NI MUHIMU KUTOKANA NA MAZINGIRA. HATA DOKTA MWENYEWE SI SULUHISHO LA MATATIZO YAKE .Ndio maana akiibiwa atamtafuta afande mmoja ili amsaidie kumkamatia mwizi aliye muibia laptop yake yenye nyaraka. NAPITA WAUNGWANA.
   
 8. Mubezi

  Mubezi Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hata mimi sikubaliani na wewe,naunga mkono madaktari kugoma,mwaka jana dada yangu alikufa,alikuwa ndio amemaliza masomo muhimbili na alikuwa yupo kwenye mazoezi pale Amana,sababu ya kufa ni kukuosa pesa ya kujikim na matibabu baada ya kuugua kutokana na kufanya kazi katika mazingira atalishi,je kwanini tunaangalia upande wetu na hatuanagalii upande wa madakitari???,Je daktari sio mtu?,je yeye aumwi?,je yeye aitaji uhuma bora?,nilikuwa mwaka wa pili muhimbili pale nasoma ila baada ya dada yangu kufa niliama na nikaenda kusomea kozi nyingine mlimani,sasa tusiangalie upande mmoja pia na upande wa madaktari tuangalie mazingira yao ni magum na wengi wao wanakufa kwa magonjwa ya kuambukiza kutokana na mazingira atalishi.
   
 9. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,443
  Likes Received: 4,729
  Trophy Points: 280
  ...............Hata wewe huko sahihi.................
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana 100% na unayoyachangia kua hapa juu ya uso wa ardhi kila mwenye fani yake anao umuhimu kwa nafasi yake.
  Hili sakata la Doctors nalifananisha na mke amwambie mumewe nakupa wiki 1 uwe umenipatia mkufu usiopungua 10grm Herini, Bangili, vikuku (vyote dhahabu)
  Na aseme asipopatiwa vitu hivyo ndani ya muda huo anaondoka kwenda kwao!
  Mume anakubali kwa kumwambia haya.
  Inafika wiki mume hajafanikisha, mke anaondoka kweli, ilhali mume anamwambia usiondoke kaa naendelea kukulitafutia suluhisho suala lako.
  Mke anaweka pamba maskio na kusepa.
  Huu usepaji utakua na baraka za uhalali ?
   
 11. Mubezi

  Mubezi Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mbona kwa wabunge PESA IPO,mfano wako ni kama una wake wawili,MMOJA UNAMTIMIZIA ILA MWINGINE ASUBILI,LENGO LA PINDA LILIKUWA kulazimisha kukutana na waganga siku ya jumapili , ilikuwa kuwadanganya warudi kazini halafu jumatatu ukawatangazie wabunge nyongeza ya posho, kwani ulijua ukikutana nao baada ya nyongeza ya posho kwa wabunge hoja yako ya serikali kutokuwa na pesa ingekuwa kichekesho! haya sasa rudi kwa meza ya mazungumzo au lete askari wako waje kutibu!
   
 12. Mubezi

  Mubezi Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wabunge wakitaka POSHO ipo,madaktari wamelalamika siku nyingi na wanapewa ahadi hewa!!! Sasa mwisho umefika!!! Uvumilivu una mwisho madoctor ni watu wapole sna na welevu sio watu wa kukukrupuka tu.
   
 13. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  TATIZO lenu ni kuwaona madaktari ndiyo wenye umuhimu wa kipekee na wakimalaika!
  Hawa Polisi mnaowapa Nyumba za fullsut za bati, chumba kimoja askari mwenye mwenye watoto wa kiume na wa kike.
  Hawa wagome nchi ikapoteza amani mwenye nguvu lkn hana kipato akamvamie mwenye kipato asiye na nguvu, hao madaktari watafanyia wp kazi hata iwe unawalipa maslahi hadi ma'housegirl wao ?
   
 14. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Kwani wewe ni msemaji wa Polisi?
  2. Amani unayoizungumzika ni ipi,yaani polisi kukaa kwenye full suit wana amani? Au hujui maana ya amani uombe msaada wa kuelimishwa?
  3. Madaktari wasidai haki zao kwa sababu polisi wanaogopa kudai?
   
 15. 654

  654 Senior Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 173
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Judgement,
  What you witnessed at Bugando is what these docs see on a daily basis in their discharge of duty. I think all they are saying to the Governemnt, is create a better working environment, remunerate workers well, keep your word on time, be realistic on the professional responsibility
  Politicians have had a lee way on their health, its India whenever they fall sick, Apollo is their destination, Docs in the country are sidelined and looked down upon. You heard what the Minister was saying sic!white lies. Dr Ulimboka is not the problem in this Country, they at the Ministry know their days are numbered. Mfa maji! too sad that people die, sadly all of us will die one day, docs included, the difference is how.
  Since the Minister, Prime Minister have addressed the real issue, I think this ball is appropriately in his court. We are awaiting for his word on this saga as the nation is mourning
   
Loading...