real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Mwandishi wa BBC alitembelea mkoa wa Pwani kijiji cha Nyambunda kuzungumza na wananchi juu ya mauaji hayo ambapo mpaka sasa wameuawa viongozi 32
Mwajuma Mapande ni mjane wa watoto 6 ambaye mumewe Mohamed Thabiti aliyekuwa mwenyekitiwa kijiji aliuawa na watu hao lakini hajui ni watu gani na kwa nini walimuua
Kwa sasa ameamua kuhama nyumba waliyokuwa akiishi na kuhamia kwa wakwe kwa kuhofia wauaji watairudia familia yake
Hakuna aliyekamatwa mpaka sasa lakini wauaji hao huacha ujumbe wa maneno na maandishi kuwa wanalipiza kisasi kwa mauaji yanaoyofanywa na serikali na vyombo vya dola, madai hayo yanakanushwa na mkuu wa wilaya ya Kibiti