Wanaotuhumiwa kwa rushwa na uporaji wa rasilimali wasigombee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaotuhumiwa kwa rushwa na uporaji wa rasilimali wasigombee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by armanisankara, Aug 26, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Antony Kanyama, amesema kuwaacha wanachama wanaoguswa na rushwa au uporaji wa rasilimali za Taifa kuendelea kuwania uongozi ndani ya chama unakikosesha ushindi katika chaguzi zinazowashirikisha wapinzani.

  Kanyama ambaye ni mwanasheria kitaaluma, alitoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec), kupitia Wilaya ya Dodoma Mjini.

  “Watu wanaoguswa na rushwa tuwaache na wale wanaodaiwa kuguswa na uporaji wa raslimali za taifa nao tuwaache,” alisema Kanyama.

  Alisema mfumo wa uendeshaji wa chama hicho ambacho kimekuwa kikitawala tangu nchi ipate uhuru, kimekuwa kikijiendesha kwa mtindo wa chama kimoja wakati kuna nchi ina mfumo wa vyama vingi.

  “Kosa ni kubaki kumchagua mwanachama anayekubalika ndani ya cha tu na si anayekubalika ndani na nje ya chama, tukifika katika chaguzi zetu hawa tunaowachagua ndio watakaokwenda kuwanadi wagombea wetu na kwa kuwa hawakubaliki tunashindwa," alisema Kanyama aliyefuatana na wanachama wa tawi la la makao makuu ya chama hicho.

  Alisema mahitaji ya watu wa nje ya chama yanapaswa kuzingatiwa kwa maslahi ya chama na kwamba iwapo atapata nafasi hiyo Nec atashauri hilo wanachama wanaochaguliwa katika chaguzi za ndani wasiwe wale ambao hawakubaliki nje.

  Pia alisema iwapo atachaguliwa atakishauri chama kutafuta mfumo mwingine wa kura za maoni ambao umeacha madonda miongoni mwa wanachama na hivyo kuweka makundi.

  “Wanachama wanazuiwa kugharamikia uchaguzi lakini unatoa mwanya kwa wanachama kununua uchaguzi, nikiipata nafasi hii nitashauri mfumo utakaowezesha kuondokana na jambo hili,”alisema Kanyama aliyeonyesha kujiamini na jambo analolizungumza.

  Akimkabidhi fomu hizo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dodoma Mjini, Alhaji Saad Kusilawe, alisema maandamano makubwa wakati wa kuchukua na kurejesha fomu ndani ya chama hicho ndiyo cha mgawanyiko.

  “Kwa staili ya maandamano wale wanachama waliogawinyika kutokana na idadi ya wagombea ndio wanaokuja kugawanyika…Hili likiendelea litaanzisha makundi kwanini jina la fulani limerudi na la fulani halijarudi,”alisema.

  Aliufananisha uchaguzi huo na gari ambalo limetembea umbali mrefu, linalohitaji kufanyiwa service ili liweze kufanya kazi.

  Aliwataka wanachama wote kushikamana kwa kuwa wote wanaogombea ni wanachama wa CCM na kusaidia mara baada ya kupatikana kwa kiongozi mara baada ya uchaguzi.

  Jumla ya wanachama sita wameomba kuwania nafasi mbili za kuwakilisha wilaya ya Dodoma Mjini katika Halmashauri Kuu ya Taifa Nec.

  Wengine ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Dodoma Mjini, Ephrahim Madege, Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM mkoani hapa, Haidary Gulamali, Daudi Nyinge na Peter Mang’ati.
  CHANZO: NIPASHE

   
Loading...