Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Ugunduzi mpya unaonyesha kwamba, wale wanaume ambao huwa ni watu wa kukubali kila jambo wanaloambiwa na wake zao, huja kufikia mahali ambapo uwezo katika tendo la ndoa huisha ambapo hushindwa kabisa kushiriki jambo hilo au kulishiriki kwa taabu sana. Tatizo la uwezo wa nguvu za kiume ambalo hufahamika kitaalamu kama erectile dysfunction, huwa linawakumba zaidi wanaume ambao wametawaliwa na wake zao kuliko wale wanaume wenye kauli ya mwisho kwenye nyumba zao. Utafiti wa kitaalamu unaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya watu wenye umri kuanzia umri wa miaka 45 huwa wanakabiliwa na tatizo hili.
Takwimu zitokanazo na tafiti mbalimbali kuhusu suala hili zinaonyesha kwamba, kati ya hao nusu ya watu wote wenye umri kuanzia miaka 45, wengi ni wale ambao hawana kauli mbele ya wake zao. Pamoja na kuwa ni tatizo linaloambatana na umri, suala la mwanaume ‘kukaliwa' na mkewe limeonyesha kuwa na athari zake. Sababu zinazotajwa kuwaweka wanaume wanaotawaliwa na wake zao kwenye hatari ya kuishiwa na nguvu za kiume ni zile za kisaikolojia. Kati ya kila wanaume kumi wanaoishiwa na nguvu za kiume kutokana na sababu za kisaikolojia, sita ni kutokana na kutawaliwa na wake zao. Unaweza kushangaa ni kwa kiasi gani kiwango ni cha juu sana.
Mwanaume ambaye hana kauli kwa mkewe mara nyingi anajiamini anaposhiriki tendo na huwa hana wasiwasi, hali ambayo humuongezea uimara katika suala hilo tofauti na yule ambaye ametawaliwa. Anayetawaliwa huwa na hofu na wasiwasi kutokana na kutojiamini. "Bwanae mbona unafanya kama bata, unanichafua tu hapa………." Wanawake wanaowatawala waume zao ni rahisi kutoa kauli kama hizi wakati wanapokuwa kwenye tendo la ndoa na waume zao, kauli ambazo huwaua waume zao kisaikolojia.
Kwa hiyo wale wanawake ambao wanaona fahari kuwatawala waume zao inabidi wajue kwamba, kitendo hicho huwasababisia waume hao matatizo makubwa katika tendo. Mbaya zaidi ni kwamba wanawake hao mwanapoona waume zao ni ‘wachovu' hukimbilia nje haraka na waume hao huzidi kudhalilika.