Wanaotamani kufa au kufifiia kwa upinzani nchini ni wasioelewa mambo

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kwanza nitoe maana ya neno ujinga kua ni kutoelewa tu kitu flani kwa Uvivu wa kutotaka kuelewa.



Hivi mtu anapoomba upinzani ufe kwa maana ya yeye kuendelea kunufaika na mfumo wa chama kimoja ana uzalendo kweli mtu huyu? Binafsi Mimi namuona mtu huyu kama kunguru aliyejivika vazi la manyoya ya kuku.Huyu mtu ni hatari sana na ni wa kuogopwa kama ukoma.


Katika historia ya siasa za nchi hii tuliwahi kua na chama kikuu cha upinzani nchi NCCR mageuzi kikabezwa kinaitwa chama cha hovyo, ikaja CUF nayo ikaitwa chama cha hovyo, sasa Chadema nacho kinaitwa chama cha hovyo! CCM pekee ndicho eti chama safi, chama ambacho kinaongoza kwa ufisadi nchini na hata dunia inatambua.
Sasa wahafidhina hawa wanataka chama kitoke mbinguni ndio kitaitwa chama safi kisichokua cha hovyo? Wanataka viongozi wa upinzani watoke mbingu ipi kama 80% ya viongozi wa upinzani walitoka CCM? Hawa hawa wapinzani ndio waliolelewa ndani ya ccm sio busara kuwaita watu wa hovyo!Huu sio ukosefu wa uelewa ni nini?



Wasiokua na uchungu wa taifa hili pekee ndio hawajui michango ya upinzani nchini, ni wao pekee ndio wanaoamini katika kichwa kimoja tu bila ya kua na mawazo mbadala.Ni ulafi uliopitiliza kwa kulinda tumbo lako ndio unaona ni bora kubaki na mlengo wa chama kimoja ili wewe uendelee kubaki kunufaika.


Tumeshindwa kuelewa kua hata wale wanasiasa walioko upinzani endapo tukafikiria kubaki ndani ya mfumo wa chama kimoja nao watarudi kuja kubanana kwenye hicho chama kimoja? Mnafikiri wao nao kama wamezaliwa wakiwa na talent ya siasa wataenda kuongoza wapi kama sio kurudi kuja kusongamana ndani ya Chama hicho kimoja?



Utaratibu wa kua na mawazo mbadala ni tangu Mungu anaiumba dunia, alijua kua mwanadamu ana madhaifu ya kujisahau hivyo akaona ni muhimu kua na mbadala wa kumkosoa.Kama tunakumbuka jinsi ambavyo aliyekua mtawala wa nchi ya Misri Faraoh alivyojisahau na Mungu kuamua kumpeleka Mussa kumkumbusha kua anayoyafanya sio sahihi, hivyo Faraoh pamoja na kuyakataa mawazo mbadala ya Mussa lakini siku ya mwisho aliyakubaluli akiwa ndani ya bahari Mwili mzima kichwa juu ya maji.
Kwahiyo wachumia tumbo ndio wataendelea kutamani kubaki kubaki ndani ya utawala wa Farao bila ya kua na mawazo ya kina Mussa lakini haitawezekana! Wapinzani wataendelea kuwepo tu liwake jua au lizame jua.



Wachumia tumbo ndio watakaobaki kulia na kutamani upinzani ufe ili kuendelea kufaidisha matumbo yao.Rata mataifa makubwa na yenye nguvu kubwa kiuchumi yalishakubali mawazo mbadala siku nyingi na yanaendelea kusonga mbele sisi pamoja na kua na rasirimali lukuki tutaendelea kwenda kupiga magoti kwao. Kama tuliikata misingi ya kijamaa aliyoanzisha mwalimu tukakubali mifumo ya kibebari ni lazima tuyakubali mawazo mbadala tu hatuna namna! Nchi yeyote duniani iliyopiga hatua za kimaendeleo chini ya mfumo wa chama kimoja ni lazima inaamini katika mfumo wa kijamaa kitu ambacho sisi kwetu haiwezekani.


Ni bora kuona demokrasia inatamalaki nchini na ustawi wa upinzani kuimarika ili kuendelea kuwapa changamoto watawala wasijisahau.
 
Nguvu za hoja zitaleta maendeleo ya nchi, huu ubabe unaoendelea sasa tutarudi enzi za mwalimu.
 
Back
Top Bottom