Wanaotakiwa waachie ngazi ndani ya CCM wanaweza kujifunza kwa marehemu Kawawa

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Mwanzoni mwa miaka ya 1980 halmashauri kuu ya CCM iliagiza serikali kuwachukulia hatua kali wale wote iliowahita wahujumu uchumi.

Hata hivyo kabla ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo, iliamriwa ya kuwa wajumbe wa halimashauri hiyo wakutane chini ya uenyekiti wa mzee Aboud Njumbe, ambaye kwa wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, na kujichunguze wao wenyewe, ili kubaini kama kulikuwa na yeyote miongoni mwao ambaye alikuwa mhujumi uchumi.

Pamoja na azma hiyo, wajumbe wa halmashauri hiyo walishindwa kujichunguza wao wenyewe kwakuwa wakati wa kuanza kwa kikao hicho marehemu Rashid Kawawa ambaye ndiye alikuwa anapashwa aanze kujadiliwa alikataa kutoka nje kwa madai kwamba kwakuwa kila mtu alikuwa anajua madhambi ya wengine ingelikuwa vyema mjadala huo ukaendeshwa wakati wote wapo ili ipatikane fursa nzuri ya kusemana vilivyo.

Hoja hiyo ilizua mjadala mkali, na iliposhindikana kufikia muafaka suala hilo lilibidi lipelekwe kwa Mwalimu aliyekata shauri ya kusitisha zoezi hilo.

Vivyo hivyo, hao wanaoshinikizwa kujihengua ndani ya CCM kwa madai ya ufisadi wanaweza kuzima shinikizo hizo wakiomba uitishwe mkutano wa vikao husika ili wasemane wote.
 
Back
Top Bottom