MKONGA
JF-Expert Member
- Feb 19, 2015
- 667
- 453
Habari zenu wote humu ndani wakuu, nimejaribu kutafakari kwa kina, na kuwaza juu ya ulipaji kodi hapa nchini kwetu, na kubaini wale wafanyakazi karibu wote wa TRA, Na mamlaka nyinginezo za ushuru na kodi. Hawana uzoefu na biashara wanazo toza kodi au mapato.
Nimeona niandike ili nao waweze kusoma na kufanya tafiti za kutosha juu ya mwenendo wa biashara zetu, zote na za madaraja yote. Kwa mfano; gharama halisi za uendeshaji biashara hizo. Aina ya biashara inayotakiwa kulipa kodi au mapato. Na pia sehemu biashara ilipo.
Zipo biashara zina kodi zaidi ya moja na uendeshaji wake ni mgumu kulingana na faida inayopatikana.
Mfano namba moja ni biashara ya daladala au gari za biashara. Biashara ile ina kodi nyingi pamoja na faini zisizo na maana angali ni biashara inayotoa huduma kwa jamii.
Ningeshauri biashara zote ziangaliwe upya kwa jinsi ambavyo wananchi wanavyo nufaika na huduma zake; halafu zipewe unafuu wa kodi na si kuzikamua kiasi kwamba huonekana si biashara yenye kumwinua mwananchi tena.
Kuna Tra hupata sehemu ya mapato kutoka ktk vyombo hivi vya usafiri, kuna Trafic nao faini wanazopiga; hutokana na faida ya biashara hii; kuna Sumatra, nao faini zao hutokana na faida ya mapato ya biashara hii. Zaidi kuna kodi serikali inazo pata kutoka ktk Mafuta; spea; n.k.
Ukitazama kwa makini hii imegeuka kuwa biashara inayo kimbiwa na watu wengi kwa kasi kwa kuwa inajiendesha kwa hasara sana.
Tuna shauri serikali na vyombo husika vinvyo itazama sekta hii ya biashara usafiri kuifikiri upya ktk swala la kodi; na mambo mengine kwa kuwa ni sekta muhimu ktk jamii yetu.
Ikiwezekana, TRA wanunue mabasi ya kutoa huduma kama hii, kwa muda ili waweze kufanya utafiti wa kutosha namna bora ya kuiokoa nayo iwe sehemu ya biashara yenye faida.
Zipo biashara nyingi zenye makodi mengi kama vile baa na hotel. Lakini leo nimeona nisemee ile biashara ninayoijua kwa undani.
Naomba kuwasilisha kwenu nami nipate maoni yenu. Pia unaweza kuanisha ni biashara ipi unafikiri ingekuwa vyema mamlaka yetu ya Mapato ingeingalia upya ktk kurekebisha kodi zake ziwe ndogo zenye kunufaisha pande zote mbili?