Wanaotaka wengine walipe kodi hawana biashara, na hawajui uchungu wa kulipa kodi

Umeongea jambo la kweli. Kwa mwenye hela na anataka kufanya biashara afikirie mara mbili mbili. Kodi ya frem, manispaa, service levy na TRA ambazo zote hulipwa kabla ya kuaza biashara. Uzoefu wangu umeonesha kuwa watu wanapishana kwenye frem kila baada ya miezi 6 au 12, na mwenye frem anapiga hela tu. Kama una hela nakushauri ukalime.

Hapo ni kweli kabisa; umenena. Kwa hali ya sasa kazi ama biashara ya kujiajiri yenye uhakika wa kesho hakuna, hata hiyo kulima yenyewe mazingira ya hali ya hewa si ya uhakika kabisa.
 
Back
Top Bottom